Mfanyabiashara Manji sasa ataka kituo cha ITV kifungiwe wiki moja

Makaayamawe

JF-Expert Member
Feb 21, 2009
341
9
Mfanyabiashara Manji sasa ataka kituo cha ITV kifungiwe wiki moja

manjihoi.jpg

Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji, ambaye yupo katika malumbano marefu na mfanyabiashara pia maarufu Reginald Mengi, akitaka kitu chake cha televisheni kifungwe kwa wiki moja.Na Fredy Azzah

MGOGORO wa wafanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Reginald Mengi na Yusufu Manji umeingia katika sura mpya, baada ya Manji kupeleka malalamiko kwa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), kutaka kituo cha Televisheni cha ITV, kifungiwe kwa wiki moja.

Malalamiko hayo ya Manji yanahusu habari iliyosomwa na ITV Aprili 23, mwaka huu, saa mbili usiku na kufuatiwa na kipindi maalum kilichorushwa siku hiyo hiyo.

Shauri la malalamiko hayo liliwasilishwa jana TCRA na kuanza kufanyiwa kazi siku hiyo hiyo.

Wakili anayemtetea Manji, John Kamugisha alidai mteja wake ameamua kuwasilisha shauri hilo TCRA baada ya kuona kuwa hakutendewa haki katika kipindi maalum cha nusu saa kilichorushwa na ITV.

Katika kipindi hicho Mengi aliwataja wafanyabiashara watano akiwatuhumu kuhusika na vitendo vya ufisadi na kuwaita kuwa ‘mafisadi Papa’.

“Tunaamini haki itatendeka hapa. Kimsingi tumependekeza kituo hicho kifungiwe kwa angalau wiki moja,” alisema.

Alisema, mteja wake hakutendewa haki kwa sababu hakupewa nafasi ya kutoa maoni yake kama sheria ya utangazaji na maadili ya habari nchini yanavyotaka.

Wakati wa kuwasilisha malalamiko hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Redio One, Joyce Mhavile na Wakili wa Mengi, Michael Ngalo pia walikuwepo TCRA.

Kwa mujibu wa Kifungu namba 28 cha Sheria ya Utangazaji ya mwaka 2005, mtu yeyote atakayekiuka taratibu za utangazaji, kama hakuna adhabu iliyotajwa kwenye kifungu husika, atatakiwa kulipa faini ya Sh5milioni.
 
Last edited by a moderator:
wachemfu hawa mafisadi papa! warudi makwao sijui india uko au wapi wakasote ka wenzao!
 
And the drama continues. It is now like a long running soap opera doing everything it can to increase its rating.
 
Ila mafisadi papa wao wanayo mamlaka ya kuwasema wenzao na hata kupanga adhabu wanazo stahili kupewa wale wanao wagusa, kama siyo Yuko wapi Mkuchika na Sofia Simba?
 
Sasa fisadi Manji kama hajatendewa haki, ITV ikifungiwa kwa just 1 week haki yake itapatikana au? si aende mahakamani akadai fidia!!!!!!!!!!
 
anawasilisha malalamiko au anawasilisha hukumu?
kufungiwa wiki moja ni malalamiko au hukumu
mengi haruhusiwi kuhukumu yeye anaruhusiwa kuhukumu
 
Jamani watanzania kwa kusahau, mmh. Kampuni ya kwanza kurusha matangazo ya TV Tanzania bara ilikuwa CTN - sasa ngoja niwasimulie stori ya hawa wahindi (anayetaka kuniita mbaguzi - karibu). CTN walifunga mitambo isiyokubalika nchini na kama tayari ulikuwa na TV ili upate matangazo yake ilibidi uwapelekee wakufungie kitu kinachoitwa "filter" uweze kupata sauti. Huu ulikuwa ni mpango wa makusudi kabisa wa kuwaibia wananchi kwa sababu hizo "filter" ilikuwa tayari wanazo "in stock".

Kufunga hicho kidude ambacho kwa gharama yake halisi ungeweza kupata kumi kwa dola moja, watu walikuwa wanalipa zaidi ya Tshs. 2,000/- waweze kufungiwa. Walichofanya hawa wahindi ndicho kilikuwa kibaya zaidi - badala ya kuifunga sambamba na ile "filter" ya zamani, wao waliondoa ile ya zamani na kufunga mpya. Walivyo wajanja hawakukurudishia ya zamani kwani walijua kuwa kuna siku utahitaji tena kurudi kwao.

ITV ilipoanzishwa kwa kuzingatia mitambo inayokubalika kwenye eneo la bara letu, wenye TV tayari walikuta hawawezi kupokea sauti. Ilibidi wapeleke TV zao zibadilishwe "filter" waweze kupokea sauti na sehemu pa kuzipata ikawa ni kwa wahindi hao hao. Nina hakika waliishia kununua zile zile filter zao zilizotolewa mwanzoni na ikawagharimu tena kiasi kile kile. Nakumbuka ITV walivyojitahidi kuwaonya waliokuwa wananunua TV mpya kutokuzifanyia marekebisho yoyote.

Tendo la ITV kujaribu kuwanusuru wananchi na hila za wahindi ndicho kilizaa uhasama ambao umeendelea hadi leo. Swali lililowaumiza wananchi ni kuwa ilikuwakuwaje CTN wakaruhusiwa kufunga mitambo isiyoendana na mfumo unaokubalika eneo hili ? Serikali ya wakati huo chini ya Ali Hasan Mwinyi iliweza kufumbia macho huu wizi na mimi ni shahidi kama moja wa walioathirika.

Kingine kilicholeta ugomvi ni kuwa CTN walikuwa na mpango wa kuwalipisha watu kuona matangazo yao, lakini ITV ikaamua kuonyesha matangazo yake bure. Pia wakati huo vituo vingine kama DTV vilikuwa njiani kufunguliwa na hicho kitendo cha ITV hakikuwafurahisha hata kidogo. Jamani, inawezekana wengine hawana kumbu kumbu, wanakumbuka tu magomvi ya baadaye. Wahindi ninaowasema ni wale waliohusika tu na kamwe si wote - poleni ambao hawahusiki.
Habari ndiyo hiyo
 
2w2etqq.jpg

sasa tuombe tuuu

hivi mnakumbuka ile ya MALIMA vs MENGI?

mnajua kama aliyemprotect mengi kwenye ile kamati alikuwa ni ROSTAM kupitia mgongo wa SPIKA HII HAMJAJIULIZA KWA NINI RIPOTI YA ILE KAMATI HAIPO PUBLIC?
 
Thanks GT;

Hii ni exciting info.... Sasa ulikuwa wapi kuisema tangu zamani??? Hebu donoa zaidi labda na sisi tutafunguka na kuacha bias zetu
 
Hah hah! si kweli.... ni ITV ilipokuja ndio tulitakiwa tununue "crystal" ili kupata sauti. Walipoanza CTN hakukuwa na kitu kama hiyo... Hata hivyo suala la ITV halikuwa hila bali ni mfumo wa tu wa Ma TV ya kizamani yale ya "fomeka" kutoenda sanjari na mitambo ya kisasa ya ITV.

Tafuta spin nyingine hii hapana....
 
2w2etqq.jpg

sasa tuombe tuuu

hivi mnakumbuka ile ya MALIMA vs MENGI?

mnajua kama aliyemprotect mengi kwenye ile kamati alikuwa ni ROSTAM kupitia mgongo wa SPIKA HII HAMJAJIULIZA KWA NINI RIPOTI YA ILE KAMATI HAIPO PUBLIC?

Game siku nyingine bwana! hebu zilete nzima nzima basi,
 
hao wazee wa DATAZ wa JF wanajua kilichotokea na kwa nini ile kamati haikuwa PUBLIC lakini jamaa walishamweka MENGI kwenye corner na he was so humiliated na alimshukuru sana ROSTAM kwa kumsaidia through SITTA

By the way nashangaa wazee wa DATAZ wa JF nashangaa wako kimya kuhusus press conference ya KUBENEA juzi na cha ajabu hamjambiwa kwa nini haikufanyika

anyway endeleeni na episodes zenu za kudandia dandia

The bottom line MENGI na ROSTAM walikuwa maswahiba wakubwa sana na sioni sababu gani urafiki wao usirudi kama watakuwa na common interest
 
Back
Top Bottom