Hah hah! si kweli.... ni ITV ilipokuja ndio tulitakiwa tununue "crystal" ili kupata sauti. Walipoanza CTN hakukuwa na kitu kama hiyo... Hata hivyo suala la ITV halikuwa hila bali ni mfumo wa tu wa Ma TV ya kizamani yale ya "fomeka" kutoenda sanjari na mitambo ya kisasa ya IT
Tafuta spin nyingine hii hapana....
Wakati mwingine kitu kama hukijui ama hukielewi ni heri kukaa kimya kuliko kuonyesha ujuha kama huu hapo juu. Katika kurusha matangazo,
broadcasting, yawe na
radio au
TV, dunia imegawanywa katika
zones mbali mbali na kila
zone hutumia system ya aina fulani. Popote pale kama unanunua kitu kama TV, ukiwaambia tu kuwa unaipeleka Tanania, moja kwa moja utaambiwa unahitaji
TV ya
system gani. Kwa mfano huwezi kununua
TV yoyote tu Marekani ukaileta Tanzania na ikafanya kazi. Hii haikujali kama
TV ni ya fomeka au ya mbao.
Hata hivyo wenye pesa zaidi walikuwa wanaweza kununua
TV ya
multi system na hii inaweza kutumika popote pale. Lakini linapokuja swali la kurusha matangazo ya
TV, aina ya system inatiliwa mkazo zaidi. Kwa kanda hii ya Afrika, walichofanya
CTN, ingekuwa nchi wanazojali sheria, kamwe hawangeruhusiwa kurusha matangazo. Na kwa faida yako na wengine kama wewe, baadaye baada ya kubanwa ilibidi wabadilishe
system yao na kufuata sheria. Ajabu ni kwamba kwenye hili swala sijui tume ya matangazo ilikuwa imelala wapi - lakini si lolote lawezekana Tz ?
Masatu, najua umezoea kutetea mafisadi kwa sababu unazozijua mwenyewe lakini kwa hili unavuka mpaka unapodai kuwa
ni ITV ilipokuja ndio tulitakiwa tununue "crystal" ili kupata sauti
Ni kwa sababu wananchi waliingizwa mjini na wahindi wa CTN na kwa ufahamisho kwa kutumia neno
crystal, wananchi walitoa hela bila wasi wasi. Kifaa chenyewe kinaitwa
cystal filter lakini kuiita crystal peke yake kuli
sound kama kitu cha maana sana -
na wajinga ndio waliwao. Hebu soma tena maelezo yangu ya mwanzo.