Mfanyabiashara maarufu Arusha Olais Metili afia guest

Mfanyabiashara maarufu Arusha Olais Metili afia guest

Arusha Leo

Senior Member
Joined
Mar 12, 2012
Posts
120
Reaction score
72
Metil alifika katika nyumba ya kulala wageni ya diamond Motel iliyopo Salina jijini Arusha, akiwa na Mwanamke na baadae ucku Mwanamke aligundua amekufa akatoweka.

Mfanyabishara Metili amefia kwenye kifua cha hawara, katika hotel ya Diamond Motel iliyopo Sakina, Arusha baada ya kutumia dawa za kuongeza nguvu aiana ya Viagra.

Gari yake aina ya Land Cruaser yakutwa nje ya hoteli, mwili watolewa chini ya ulinzi wa polisi. Ndugu wapagawa kwa kilio.
======================

Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha, Olais Metili amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni..

Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha, Olais Metili mkazi wa Uzunguni jijini hapa, amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni ya Hoteli Diamond Motel iliyopo eneo la Sakina jijini hapa.

Mwili wa mfanyabishara huyo anayemiliki mali mbalimbali ikiwamo mgahawa wa Bite Bite na duka maarufu la vinyago eneo la Kisongo uligundulika jana saa 7:00 mchana, wakati wahudumu wa hoteli hiyo wakitaka kufanya usafi chumba alichokuwa amepanga.

Mfanyabiashara huyo mwenye umri unaokadiriwa kufikia miaka 56 , ilidaiwa aliingia hotelini hapo na mwanamke mmoja ambaye hata hivyo, haikujulikana muda ambao alitoka.

" Metili (Marehemu) alifika katika hoteli hiyo akiwa ameongozana na mwanamke mmoja ambaye hajafahamika na kuingia katika chumba chake na haijulikani aliondoka muda gani huyo mwanamke," alisema mmoja wa wahudumu wa hoteli hiyo.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas hakupatikana jana kuelezea taarifa za awali za uchunguzi wa kifo hicho, lakini maofisa wa polisi waliuchukua mwili huo, wakisema huenda kesho taarifa itatolewa rasmi.

Tukio hili, linakumbusha kifo cha Kada wa CCM, Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya UVCCM Taifa, Benson Mollel ambaye alifariki dunia katika hoteli ya Lash Garden eneo la Jakaranda ambapo pia alidaiwa aliingia katika chumba hicho na mwanamke.

Matukio ya kufa katika nyumba za wageni, katika jiji la Arusha, yanahusisha na matumizi ya pombe kali au dawa za nguvu za kiume kwa wanaume wengi ambapo dawa zimekuwa zikiuzwa katika maeneo mengi jijini hapa bila ya udhibiti mkali

Chanzo: Mwananchi
 
'Millionea mwingine afariki Arusha' Nilitegemea heading hiyo. R.I.P Olais Metili. Millionea wa Arusha alikuwa ktk harakati za kuitendea haki hela yake. Mamillionea wanapukutika A City, machallii arifu wangu kuna nini huko?
 
Bilionea mwingine afia gesti. Arusha hata ukiwa muuza nyanya utaitwa bilionea

Hahaha Nazjaz umeniacha hoi sana kumbe na huyu alikuwa billionea? Basis Arusha kuna mabillionea wengi sana.
 
Last edited by a moderator:
Mfanyabishara Metili amefia kwenye kifua cha hawara,katika hotel ya Diamond Motel iliyopo Sakina,Arusha baada ya kutumia dawa za kuongeza nguvu aiana ya Viagra.Gari yake aina ya Land Cruaser yakutwa nje ya hoteli ,mwili watolewa chini ya ulinzi wa polisi,ndugu wapagawa kwa kilio.

Ndio yule mmiliki wa Ilboru Lodge?
 
Viagra ni tatizo sana si nzuri kutumia pasipo kujua afya yako kama kisukari/pressure etc.
 
NDugu zangu hilo ni zoezi la wakomunisti,tukiana kumcambua kila mtu basi huo ndio utakuwa mwanzo wa mfarakano kwa taifa letu changa.Kumbukeni zoezihilo lilianznzishwa na Sokoine na lilileta matatizo makubwa sana nchini,hizo ni politicsza kukomoana na fitna tupu.kumbukeni serikali yetu inasheria na ni vyema tungefuatilia sheria ,kama kinogozi kavunja sheria kujipatia mali basi sheria itumike mara moja hao wako wengi sana ,watu kama aliyekuwa waziri muu Mr Sumaye ni miongoni mwa wavunjaji wa shria na wamejilimbikizia mali kwa taratibu chafu sana na zinaeleweka na kila mtu hapa.Naomba tuzingatie sheria kabla ya kutoa ushauri mwingine.

peace!!!!!

R.I.P mfanya biashara maarufu.
 
Arusha ya sasa ina mambo kwakweli:
Mabomu kwenye mikusanyiko - Arusha
Ujambazi - Arusha
Kufumaniwa - Arusha
Kufia kwenye vifua - Arusha

Ee Mungu tuondolee laana hii
 
Zile dawa ni mbaya sana hazifai. Tumia njia zawaida kula matunda, mbogamboga weka vitunguu vya kutosha na chunvi ikolee kidogo utapiga bao zako mbili ukalale. We unataka kukomoa mwanamke hakomolewi hata kidogo, mwanamke msingi maji.
 
Kuvamia haya madawa bila kuongea na Dr ili kupata recommendation yake ni hatari sana, wengi wamepoteza maisha katika nchi nyingi duniani na wengine kuwa vipofu. Poleni wafiwa, Muumba wetu ailaze roho ya mareheme mahali pema peponi~AMEN.
 
Sababu ya kifo imetoka baada ya madaktari kufanya uchunguzi au hii imetokana na deductions tu kwamba alikuwa ametumia viagra ?
 
Huyu ndiye yule mmiliki wa Iboru Lodge au tafadhali mtujuze.
 
Back
Top Bottom