zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 19,066
- 28,714
- Thread starter
- #761
Nashukuru kwa insight zako makini, lakini utusaidie kuhusu huu mstari kama basis ya Hoja.zitto junior kwanza hongera kwa utafiti uliofanya,umefukua sehemu nyingi sana. Ila nakataa hoja yako.
1. Wanefili walikua nusu malaika nusu binadamu na hakuna alieponyoka gharika. Wengine walijivua miili ya kibinadamu na kurudi mbinguni na wengine waliangamizwa.
2. Baada ya gharika dunia ilikuwa na wanadamu 8 tu. Unaweza kupitia tena Mwanzo sura 6 na ya 7 inatosha kabisa kukupa jibu.
3. Mfalme Ogu alikuwa Mrefaimu (kabila)kuna tofauti na wanefili na warefaimu. Warefaimu walikuwa warefu kiasili hata Goliathi alikuwa na asili hiyo.
Natamani sana kujadiliana mengi na wewe, inaonekana unaijua biblia kwa kiasi niPM kama vip
Hesabu 13:33
33 Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.
Assuming wote walikufa kwa gharika iliwezekana vipi hawa wana wa Yakobo wawaone tena kule Canaan?
Kuhusu watu 8 kupona unajua its tricky bible ikisema WATU specific inaweza kuwa ni walengwa tu..... Mfano
YUDA
14 Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu
Lakini ukisoma mwanzo utagundua Cain alishazaa vizazi vingi mpaka seth anazaliwa ambaye ndio lineage ya Henoko. So haiwezekani akwa literally mtu wa 7 kama Yuda anavyosema? So naweza adress hivo hiyo nadharia ya watu 8 kupona kwamba ili focus kwa context ya eneo hilo.