Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,533
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,533 2,000
king-og_11-jpg.758692

Mfalme OG anatajwa kwenye vitabu vya dini kuu tatu za mashariki ya kati i.e uislam,ukristo na uyahudi....

Inaelezwa alikuwa ni mfalme aliyetawala eneo la Canaan (palestina/israel ama jordan ya sasa )katika ulimwengu wa kale takriban miaka zaidi ya 6000 iliopita.... Na inaelezwa ndio mwanadamu aliyeishi zaidi kutokana na kuwa na mwili mkubwa sana aliishi zaidi ya miaka 3500!!! Alikuwa ni mfalme aliyeogopeka sana mashariki ya kati maana alikuwa jitu lenye nguvu na mrefu zaidi ya minazi kama anavyoelezwa na Nabii Amos

Amos 2:9
9 Lakini nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini naliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini.

Umaarufu wa Mfalme Ogu wa bashan umekuja baada ya historia kubainisha kwamba ndio binadam pekee aliyesalia kwenye gharika nje ya Nuhu na familia yake!!

JE ALIPONAJE GHARIKA

1. Nadharia ya kwanza inasema alikuwa mrefu sana kiasi kwamba maji ya gharika yalimfikia kiunoni!!!!

2. Nadharia ya pili inasema kuwa alikuwa na ukaribu sana na Nuhu hivyo alipewa kazi ya kuiangalia safina kwa nje kuhakikisha haigongi mwamba au mawe makubwa ambayo yangeweza kuipasua safina na hiyo ndio ikawa pona yake!!! Inadaiwa alijishikiza pembeni ya safina ya nuhu ivo hakubebwa na maji ya gharika. Nadharia hii ina mashiko sababu hata baada ya gharika tunaona safina hii ilitua palepale ilipokuwa kabla ya gharika yaani haikuenda mbali kabisa kitu ambacho hakiwezekana kama nguvu ya mafuriko ikizingatiwa lazima boti ingesukumwa maili kadhaa mbele. Kingine kwa akili ya kawaida tu dunia nzima izame alafu ww pekee uwe kwenye boti hivi wanaokufa watakuacha kweli?? Lazima wangetaka kuivamia boti waingia na ukizingatia yalikuwa majitu marefu yangeweza kuipasua pasua ila kwa uwepo wa OG walishindwa maana wangekutana na kipigo cha mbwa mwizi!!

3. Nadharia ya tatu inasema kipindi cha gharika Ogu alikuwa bado hajazaliwa ila mimba yake ilikuwa imeshatungwa na mama yake aliekuwa mke wa Ham hivyo ham asingeweza kumuacha nyuma ingawa inadaiwa mimba hiyo haikuwa ya Ham bali ya Malaika aliyeitwa shamael!! Hivyo damu ya wanefili ikaweza kuvuka gharika kwa staili hiyo kupitia mtoto aliyezaliwa yaani mflame ogu ama canaan ambae watoto wake kwenye biblia wanatajwa kma majitu makubwa ambayo yaliona wanadamu kma panzi!!! Mfano amori aruba anak hivi gilgal amoni yebusi n.k

4. Nadharia ya tatu inasema alienda milimani hivyo gharika haikumkuta. Biblia iko wazi kuwa maji yalifunika MILIMA mirefu kwa futi 15 kwenda juu ina maana kma hyu OG alikuwa na futi zaidi ya 13 pengine 28 kama inavyoelezwa kwenye biblia ina maana kama alipanda milima mrefu zaidi basi hakuweza kumalizwa na gharika!! Simple logic

Mwanzo 7
20 Maji yakapata nguvu, hata ikafunikwa milima kiasi cha mikono kumi na mitano.

Najua kufikia hapa wengi mtasema ni upotoshaji na kwamba ni stori za kijiweni ila hoja hii inapata mashiko kupitia biblia kuwa mfalme OGU alikuwa ndio mnefili pekee aliyepona gharika.

Kumbukumbu la torati 3:11
11 (Kwani aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama, kitanda chake kilikuwa kitanda cha chuma; kitanda hicho je! Hakiko Raba kwa wana wa Amoni? Urefu wake ulikuwa ni mikono kenda, na upana wake mikono minne, kwa mfano wa mkono wa mtu).

hapa biblia inasema OG NI MREFAI ALIYESALIA tafsiri ya kiingereza inasema LAST OF THE REPHAIMS ikimaanisha ni mnefili pekee aliyesalia baada ya gharika!!!!

BAADA YA GHARIKA
Kupitia vitabu vya dini na kihistoria tunaelezwa kuwa baada ya gharika aliendelea kutawala maeneo ya mashariki ya kati eneo la bashan huko Canaan walipoishi majitu mengine kma wayebusi waamori waamaleki wagilgashite n.k na inasemekana aliishi miaka 3500!! Yaani alikuwepo toka kizazi cha adam hadi kipindi wana wa israel wanarudi canaan !!

MWISHO WAKE
Vitabu vya kidini na historia vinasema mfalme OG au UJ BIN ANAQ kiarabu.... Alipambana na waisraeli waliokuwa wametoka misri kuelekea canaan na katika vita hiyo inaelezwa mfalme Og aliweza kunyanyua mlima mzima!!!! Na kutaka kuutupa kwenye kambi ya waisraeli lakini Inadaiwa kwa bahati mbaya au nzuri mlima ukavunjika katikati hivyo ukamnyima balance akaangukiwa na kipande cha mlima hivo kuumia vibaya na ndipo musa akapata fursa ya kumchoma na mkuki na vita ikawa kma imemalizwa na wanajeshi wake kwa hofu wakakimbia huku na kule na waliobaki wakamalizwa na waisraeli

Kumbukumbu la torati 3
1 Ndipo tukageuka, tukakwea njia ya Bashani; na Ogu, mfalme wa Bashani, akatutokea juu yetu, yeye na watu wake wote, kuja kupigana huko Edrei.
2 BWANA akaniambia, Usimwogope; kwa kuwa nimemtia mkononi mwako, yeye na watu wake wote na nchi yake; nawe utamtenda mfano wa ulivyomtenda Sihoni, mfalme wa Waamori, aliyekuwa akikaa Heshboni.
3 Basi BWANA, Mungu wetu, akamtia mikononi mwetu na Ogu mfalme wa Bashani, na watu wake wote; tukampiga, asisaziwe cho chote.
4 Tukatwaa miji yake yote wakati huo; hapakuwa na mji tusiotwaa kwao miji sitini, nchi yote ya Argobu, ndio ufalme wa Ogu ulio katika Bashani.


NB:kwenye vitabu vya kiyahudi vinadai Mungu wao Israel yaani YHWH alishusha nzige/nyuki wakaula ule mlima kutokea katikati ndio ukagawanyika nusu ila najiuliza nyuki waule mlima ndani ya dakika??? Aseee!!!

Anyway hicho ndio kifo cha mfalme huyu aliyetikisa dunia kwa miaka yake na mpaka leo waisraeli wanatambua ushindi ule kma mkubwa kabisa kwenye historia ya taifa lao!! Hata amos na mfalme daudi huwa wanakikumbuka kisa hiko miaka zaidi ya 600 baadae!!!

Amos 2:9
9 Lakini nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini naliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini.

Zaburi 135:
10 Aliwapiga mataifa mengi,Akawaua wafalme wenye nguvu;
11 Sihoni, mfalme wa Waamori,Na Ogu, mfalme wa Bashani,Na falme zote za Kanaani


USHAHIDI WA KISAYANSI/KIHISTORIA

Rujm-El hiri or Circle of the rephaites
ogs-palace-jpg.758680

Hii inaelezwa ndio ilikuwa kasri au jumba la ibada la mfalme ogu na mpaka leo masalia yapo huko golan heights, syria (linakaliwa kimabavu na israel).... Mawe yaliyobaki kwa sasa ni zaidi ya 40,000 yamepangwa hadi futi 15 kwenda juu je kuna mtu wa miaka ile angeweza kupanga mawe mazito kwa urefu wa zaidi ya futi 50 kwa wakati huo kama hakua JITU la mfano wa OGU.

2. Karne ya 20 mwanzoni watafiti wa kijerumani waligundua makaburi makubwa ya mawe ambayo yanafanana na hesabu zilizopigwa kuhusu urefu wa mfalme ogu kwenye kitabu cha kumbukumbu la torati..... Kaburi hilo lilipatikana eneo la mto Jabbok, Bashan ambako ndipo mfalme ogu alifia. Na kwa hesabu zao kaburi hilo lina umri wa zaidi ya miaka 6000!!! Muda ambao ndio inasemekana og aliishi hapa duniani
ogs-bed-jpg.758687


3. Mfalme ogu pia alifanikiwa kuandika kitabu chenye sura 7 ambacho kilipatikana takriban miaka 1400 kabla ya kristo ila kilifichwa huko maktaba ya vatican kuaniza karne ya 5 ila baadae kilivujishwa je huu ni ushahidi mwingine kuwa JITU hili liliexist kweli na kuutesa ulimwengu!!!

Karibuni wanajukwaa kwa michango
Naomba kuwasilisha

cyclops_by_douzen-d7dvdf7-jpg.758716
 

Attachments:

zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,533
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,533 2,000
Cc hearly impongo Mchawi Mkuu Malcom Lumumba Elungata Da'Vinci Mshana Jr Palantir Eiyer Kudo900 Vi rendra N J subi Bujibuji Kipanga boy Kiranga Ziroseventytwo Che mittoga Ip man 3 SALA NA KAZI MSEZA MKULU na wanajukwa wotee
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,533
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,533 2,000
Hivi kwanni mods mnatumia muda mrefu kumoderate thread za JF intelligence ilihali majukwaa mengine kma MMU watu wanaweka mada tu bila kuwa moderated tena mada za ajabu kabisa zikijadili vibamia na makalio!!!! Seriously hii inakatisha sana tamaa kufungua nyuzi humu na cjui kwanni malalamiko yetu hamfanyii kazi au kuna watu flani ndio wanaskilizwa tu humu wengine sisi commoners tunapotezewa tu

Maxence Melo Rider Reserved Innovator
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,533
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,533 2,000
Naona wameuachia sasa.... Wadau karibuni tukumbushane historia za kale

NB: Uzi huu sio wa kidini hivyo tujadili kihistoria zaidi kuliko kiimani maana kuna wafia dini wao hawataki kabisa kusikia habari tofauti na walizojifunza kwenye nyumba za ibada!!
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,533
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,533 2,000
Sasa kwa ukubwa huo wa wanefili, waliwezaje kugegeda hao wanawake wa enzi hizo kwa hiyo mipododo na vipapuchi vidogo?
Hatujaambiwa walikuwa jinsia gani so huenda kulikuwa na wanefili wa kiume na wakike. Ila uzao wao upo mfano huyu mfalme ogu alikuwa anatawala MAJIJI 60 kwenye himaya ya jamii yake ikimaanisha aliweza kuwa na uzao ingawa hatujaelezwa huyo mke wake alikuwa wa aina gani kma naye ni alikua mnefili ama lah ila kwa kujibu swali lako tuamini tu kuwa kulikuwa na wanawake wanefili pia hivyo walilala nao hao hao
 
stardust JK

stardust JK

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2018
Messages
1,222
Points
2,000
stardust JK

stardust JK

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2018
1,222 2,000
Hawa wanefili ni matokeo ya malaika kuzaa na binadamu na inasemekana waliangamia na hawapo tena
Kwanini hawa malaika waliozaa na binadamu huwa hawashuki tena duniani na kuja kuzaa na mabinti wengine baada ya gharika hadi mpaka sasa?
Nini kimewazuia
 
impongo

impongo

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2015
Messages
6,066
Points
2,000
impongo

impongo

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2015
6,066 2,000
Kwanza kuna kitu hakileti ukweli katika Biblia maana hapa katika maandiko ya mwanzo kuna mkanganyiko inaonyesha WANEFILI WALIKUWEPO KABLA YA BINADAMU

1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,
Mwanzo 6 :1

2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.
Mwanzo 6 :2

4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa.
Mwanzo 6 :4
 
Mr Miller

Mr Miller

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Messages
11,239
Points
2,000
Mr Miller

Mr Miller

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2017
11,239 2,000
Hawa wanefili ni matokeo ya malaika kuzaa na binadamu na inasemekana waliangamia na hawapo tena
Kwanini hawa malaika waliozaa na binadamu huwa hawashuki tena duniani na kuja kuzaa na mabinti wengine baada ya gharika hadi mpaka sasa?
Nini kimewazuia
nilisoma kitu kama hicho mahali fulani, kwamba baada ya malaika kujifanyia mwili wa kibinadamu na kulala na wanawake matokeo ndio hayo majitu....na kile kitabu kilieleza kuwa gharika ilipokuja iliangamiza wote japo malaika waliacha mwili na kuondoka,

Leo nimepata kitu kingine hapa,
Ila kuna hoja moja hapo juu kuhusu mfalme OG kwamba alishikiria boti ya nuhu sijaielewa vizuri.
 

Forum statistics

Threads 1,315,053
Members 505,131
Posts 31,846,577
Top