Mfalme Charles

Mfalme au malkia wa Uingereza ana mamlaka yenye mipaka. Hilo ndilo jibu sahihi zaidi.

Mipaka ya mamlaka ya ufalme wa Uingereza ilianza kuwekwa muda mrefu sana hasa baada ya mapinduzi ya mwaka 1688 ambayo ndiyo yaliyozaa muundo wa utawala wa constitutional monarchy uliopo hivi sasa.

Hayo mamlaka yote uliyoyasema hususani kutangaza vita, si mamlaka binafsi ya mfalme au malkia, bali ni mamlaka ambayo hivi sasa yanatekelezwa na serikali ya Uingereza iliyoko chini ya waziri mkuu.

Waziri mkuu ndiye anayeshauri kiti cha ufalme kuhusu nchi kwenda vitani. Ndiye msimamizi wa utekelezaji wa sera za serikali, yeye pamoja na mawaziri wake ndio wanaowajibika katika masuala yote ya kisiasa kutokana na maamuzi yao.

Nafahamu ni vigumu wakati mwingine kuelewa tofauti kati ya absolute na constitutional monarchy lakini ukifuatilia historia ya Uingereza, utafahamu utofauti mkubwa sana.
 

Kwa hivyo Malkia akimkataa waziri mkuu, uchaguzi unarudiwa?.
 
Afadhali hata urusi wanafanya siasa hata kama za kukandamizana kama magu, lkn uk iko wazi kila kitu kinaamuliwa na familia ya kifaulme waziri mkuu ni mtekelezaji tu.

Wewe una matatizo na UK sio Siri. Yani siasa za urusi Unalinganisha na UK?. Urusi hi ambayo Putin anatawala au nyingine. Uingereza demokrasia ni kubwa ndio maana waziri mkuu anaondolewa akileta ujinga.
 
Demokrasia ya uk ni kiini macho tu, hawawezi fanya wala kuamua lolote bila mfalme

Acha kuongopea watu, Malkia yupo Chini ya constitutional monarchy na sio absolute monarchy unayosema. Sema ana nafasi kisheria kumshauri Waziri Mkuu.
 
Kuna kipindi nilisikia waingereza wamechoka na huu utawala wa kifalme, wanasema kasri linatumia pesa nyingi sana za walipa kodi nao wanaona sio sawa. "GOD SAVE THE KING", wimbo wa taifa wa hovyo kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…