LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 15,121
- 27,128
John Mgandu alikuwa mtunzi hodari wa nyimbo za kikatoliki. Binafsi ni mpenzi mkubwa wa nyimbo zilizotungwa na John Mgandu. Ifuatayo ni orodha ya midi za nyimbo zilizo tungwa na John Mgandu.
Songs by John Mgandu
----
SALUTE COMRADE
kwa wale wapenzi/walimu au wanafunzi wa Muziki wa kikatiliki baasi jina la JOHN MGANDU sio geni, kwa ufupi..
Alikua Mmoja kati ya watunzi ambao walijitahidi kutumia karama zao katika kuwasaidia waamini kusali vizuri kwa njia ya uimbaji ni Mwalimu John Stephano Mgandu.Yeye alizaliwa Oktoba 8, 1940 kijijini Busondo, katika Parokia ya Ndala-Nzega, mkoani Tabora.
Alipata elimu katika Shule ya Msingi Puge (1951-1953), kisha Seminari ya Lububu (1954 – 1955), baadaye Seminari ya Itaga (1956 – 1959) na Seminari ya Kipalapala 1964. Mwaka 1960 hadi 1970 alikuwa katika Chuo cha Ualimu cha Chang’ombe.
Elimu ya muziki aliipata katika Chuo Kikuu cha Toronto nchini Canada ambako alisomea Shahada ya Muziki (Bsc – Music) 1972 – 1976, na baadaye Chuo Kikuu cha Dar es salaam akisomea Shahada ya Uzamili (MA – Music) 1987.
Amewahi kufanya kazi katika maeneo mbalimbali pamoja na Benki ya NBC tawi la Masdo (1968), Shule ya Sekondari ya Kibasila (1970), Shule ya Sekondari ya Mirambo (1971), Shule ya Sekondari ya wavulana Tabora (1976 – 1978), Taasisi ya Elimu (1978 – 1980) na kisha Chuo Kikuu cha Dar es salaam katika Idara ya Sanaa na maonyesho (Julai 1980 – Julai 2008)
Alifunga ndoa na Elizabeth Kulwa Binti Constatino Ngelegi, na kupata watoto wawili, wa kiume na wa kike. Licha ya kuwa mtunzi, Mwalimu Mgandu alikuwa mpiga kinanda, filimbi na ala nyingine nyingi. Pia alikuwa mwalimu na muongozaji wa muziki na kwaya mbalimbali.
Ikumbukwe kuwa mwaka 2002 Mwalimu Mgandu alishinda tuzo ya kuwa Mpiga Kinanda Bora Tanzania (Tanzania Kilimanjaro Music Awards). Alifariki Julai 10 mwaka 2008.
Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa nguli huyu wa muziki mtakatifu, moja kati ya mengi ni taaluma ya muziki mtakatifu.
Mwalimu Mgandu alikuwa mwanamuziki aliye na taaluma hata kuwa na Shahada ya uzamili (Masters) ya muziki. Cha ajabu watunzi wengi siku hizi huridhika kujifunza muziki mtakatifu kwa kuunga unga. Hii hupelekea kuzorota kwa taaluma hii, kwani kilichobaki kwa sasa ni watu kurithishana na kufundishana kienyeji tu.
Hii itukumbushe pia umuhimu wa kufufua madarasa ya muziki Mtakatifu katika Seminari, nyumba za malezi, vyuo vikuu vya kanisa ili tupate wataalamu wa kutosha.
Lakini kubwa zaidi, pamoja na kuwa na elimu kubwa mwalimu Mgandu daima tungo zake zilizingatia liturujia na alitumia maandiko matakatifu kama rejea ya nyimbo zake. Sasa watunzi wa leo wanaotunga nyimbo kama ‘chenga ya mwili’, ‘gari la shetani’ nk, wamejifunza wapi mambo hayo.
Kwa upande wangu!
Nimeanza kujifunza Elimu ya muziki yaani upangiliaji wa nota, sauti, funguo za muziki miaka mitano iliyopita japo sikuendelea sana kusoma kutokana na ubize wa shule ndipo nilipoanza kumwelewa huyu mtuu uwezo wake aliokua nao wa kutunga nyimbo,kupangilia nota vizuri (Actually am a former Catholic sgospel singer at BMM choir kigoma). kiukweli sijaona mwingine tena katika orodha ya watunzi/walimu bora wa nyimbo za kikatoliki hapa Tanzania akifuatiwa na Mwarabu
waliobaki ambao naona wanajitahidi sana kwa upande wangu ni..
Frolian E Nyanza- Mwanza
mwarabu
Makoye
B. Mukasa
Creddo Mbogoye Bmm kigma
Stephen mnyonge gungu kigoma
Pius Paul- kigoma
nk. nk
The Catholic Diocese of Kigoma
https://www.google.com/url?sa=t&rct...hn-mgandu/94&usg=AOvVaw3hLAbt6F-U1qOuz9CUMYnd
credit: TEC