Mfahamu mkuu wa mkoa wa Mtwara

Mfahamu mkuu wa mkoa wa Mtwara

kalifanyia nini Taifa letu?
Alisimama Bega kwa Bega kuhakikisha walanguzi wa zao la korosho wanatokomezwa. Ili mkulima apate stahiki yake. Na hata ambao walikuwa wananufaika na walanguzi hao, walipojaribu kukwamisha jitihada zake, bila woga aliwashughulikia ili tu mkulima afaidike na jasho lake.
 
Kaolewa? Tafadhali tuwekee namba yake ya simu tumjulie hali dada yetu mpendwa.
 
Huyu mama nilikuwa nampendaga tangu akiwa Mpwapwa, mimi nikisoma mifugo hapo hapo Mpwapwa. Nikazidiwa ujanja na dereva wake aliyekuwa anakula mzigo! Daa,,, Halima wewe!! Tutakutana hata huko ukubwani! maana ng'ombe hazeeki maini!!
 
hata mi binafsi namkubali sn huyu mama, kiukweli ni mchapakazi sana na wanamtwara wengi sana wameonyesha kumkubali.......kwa miaka ya karibuni hakuna sehemu ngumu kiutawala kama masasi na tandahimba kwa mkoa wa mtwara, lakini huyu mama kakubalika sehemu zote hizo!!!
 
mkuu mbona unamvua nguo Rc wakati mleta mada kasema ni kiongozi alietukuka??
 
Hahaaa mleta mada umetutega unataka tufunguke hapana hatufunguki.Huyu Mather ngoja tumstahi kama ulivyomstahi ww.
 
MFAHAMU MHE. HALIMA DENDEGO (RC-MTWARA).

Mhe. Halima Dendego kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Mtwara. Safari yake ya uongozi na harakati za kutetea haki za wananchi na raia wa Tanzania, zilianza tangu akiwa chuo kikuu cha Dar-es-salaam (UDBS-University of Dar-es-salaam Business School). Enzi hizo ilikuwa inajulikana kama Faculty of Commerce. Alikuwa miuongoni mwa wanaharakati machachali sana wa DARUSO kutokea fass kuanzia miaka ya 2001 mpaka alipomaliza elimu yake ya chuo kikuu.

Nyota yake na shauku ya kuwapigania watanzania bado iliendelea kung'aa kiasi kwamba akateuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa. Huko alijulikana sana kwa jinsi alivyokuwa karibu na wananchi ili kuhakikisha shughuli za maendeleo zinasonga mbele. Hakuona kuwa mkuu wa wilaya kuwa ni fahari kwake bali alipigania haki ya kila mwanampwapwa kwa nguvu zake zote.

Baada ya hapo alihamishiwa kilosa kwa nafasi hiyo hiyo ya ukuu wa wilaya. Ambako nako alikumbana na changamoto nyingi, kubwa ilikuwa ni vita na migogoro kati ya wafugaji na wakulima. Alitumia utashi wake kadiri alivyoweza kuweka hali sawa.

Baada ya kutoka kilosa akahamishiwa Tanga. Kabla ya kuteuliwa na Raisi kuwa mkuu wa mkoa wa Mtwara, ambako anatumikia mpaka sasa.

Falsafa yake ya kushirikiana na wananchi bega kwa bega bado aliendelea nayo. Ikumbukwe kuwa kwa kipindi ambacho aliingia mkoani mtwara ilikuwa ni kipindi kifupi tu kimepita tangu fujo zilizosabishwa na mzozo wa gesi na ujenzi wa Bomba la mafuta kuelekea DSM. Lakini hilo halikumvunja moyo, bali alihakikisha amani inaendelea kudumu ili shughuli za maendeleo zisonge mbele.

Akiwa mkuu wa mkoa wa Mtwara amefanya mambo mengi na mazuri jambo ambayo kila mwanamtwara anajivunia kuhusiana na huyu Mama. Zao la korosho amelibeba vilivyo kiasi kwamba sasa hivi tunajua thamani ya korosho jinsi ilivyo. Hakuna asiyefahamu jinsi Mhe. Halima Dendego alivyopambana na unyonyaji ambao ulikuwa unafanyika hasa kwenye hili zao la korosho, ama kwa hakika amejitoa mhanga juu ya jambo hili. Wanamtwara tushirikiane na kushikamana na mkuu wetu wa mkoa Jemedari wetu.

Mtwara ni yetu,
Nitasimama na mkuu wa mkoa wangu.View attachment 591754

Sema anatetea tumbo lake na si wananchi, Tundu lissu ndo mtetezi pekee wa wananchi aliebaki.
 
Another bullshit story.... Sijaona chochote alofanya. Maslahi binafsi tu!
 
Haraka mbeleee tembea! Kwa kwa kwa kwa pinda kulia! Duh promo za kibongo ni tabu tubu. Nakumbuka Tibaijuka alikuwa anajipa promo humu hadi server zetu zikawa zinajaa alikuwa anajiita raisi mtarajiwa. Naona Tulia Akson naye anapambana kutafuta ubunge Rungwe asichojua ni kuwa Unyakyusani huwezi kukaa mbele ya wanaume ni Lyabhi lyako.
 
MFAHAMU MHE. HALIMA DENDEGO (RC-MTWARA).

Mhe. Halima Dendego kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Mtwara. Safari yake ya uongozi na harakati za kutetea haki za wananchi na raia wa Tanzania, zilianza tangu akiwa chuo kikuu cha Dar-es-salaam (UDBS-University of Dar-es-salaam Business School). Enzi hizo ilikuwa inajulikana kama Faculty of Commerce. Alikuwa miuongoni mwa wanaharakati machachali sana wa DARUSO kutokea fass kuanzia miaka ya 2001 mpaka alipomaliza elimu yake ya chuo kikuu.

Nyota yake na shauku ya kuwapigania watanzania bado iliendelea kung'aa kiasi kwamba akateuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa. Huko alijulikana sana kwa jinsi alivyokuwa karibu na wananchi ili kuhakikisha shughuli za maendeleo zinasonga mbele. Hakuona kuwa mkuu wa wilaya kuwa ni fahari kwake bali alipigania haki ya kila mwanampwapwa kwa nguvu zake zote.

Baada ya hapo alihamishiwa kilosa kwa nafasi hiyo hiyo ya ukuu wa wilaya. Ambako nako alikumbana na changamoto nyingi, kubwa ilikuwa ni vita na migogoro kati ya wafugaji na wakulima. Alitumia utashi wake kadiri alivyoweza kuweka hali sawa.

Baada ya kutoka kilosa akahamishiwa Tanga. Kabla ya kuteuliwa na Raisi kuwa mkuu wa mkoa wa Mtwara, ambako anatumikia mpaka sasa.

Falsafa yake ya kushirikiana na wananchi bega kwa bega bado aliendelea nayo. Ikumbukwe kuwa kwa kipindi ambacho aliingia mkoani mtwara ilikuwa ni kipindi kifupi tu kimepita tangu fujo zilizosabishwa na mzozo wa gesi na ujenzi wa Bomba la mafuta kuelekea DSM. Lakini hilo halikumvunja moyo, bali alihakikisha amani inaendelea kudumu ili shughuli za maendeleo zisonge mbele.

Akiwa mkuu wa mkoa wa Mtwara amefanya mambo mengi na mazuri jambo ambayo kila mwanamtwara anajivunia kuhusiana na huyu Mama. Zao la korosho amelibeba vilivyo kiasi kwamba sasa hivi tunajua thamani ya korosho jinsi ilivyo. Hakuna asiyefahamu jinsi Mhe. Halima Dendego alivyopambana na unyonyaji ambao ulikuwa unafanyika hasa kwenye hili zao la korosho, ama kwa hakika amejitoa mhanga juu ya jambo hili. Wanamtwara tushirikiane na kushikamana na mkuu wetu wa mkoa Jemedari wetu.

Mtwara ni yetu,
Nitasimama na mkuu wa mkoa wangu.View attachment 591754
Mwaka huu kweli namba zinasomwa kwa habari za kapet sikuna....
 
Alisimama Bega kwa Bega kuhakikisha walanguzi wa zao la korosho wanatokomezwa. Ili mkulima apate stahiki yake. Na hata ambao walikuwa wananufaika na walanguzi hao, walipojaribu kukwamisha jitihada zake, bila woga aliwashughulikia ili tu mkulima afaidike na jasho lake.
Wapi walanguzi wa korosho wametokomezwa
 
Kwa tulio ishi nae kitaani pande za kinondoni tunamuelewa vizuri huyo sista wetu..kikubwa ni mtu mwenye upendo sana hususani kwa wanawake..alifanikiwa kuwaweka pamoja wamama wa kitaa..lakini alikuwa akikupa kimemo enzi hizo tukiwa nae uraiani basi ujue umepata kazi..live longer dada
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom