Mfahamu mkuu wa mkoa wa Mtwara

Mfahamu mkuu wa mkoa wa Mtwara

Asante kwa kusimamia vizuri bei ya zao la korosho. 2020 utatufaa
 
Tunajua alikuwa bibi mdogo wa mfalme wa Mshoga na mkuu wa sijui wilaya sijui mkoa hawezi kuwa mtetezi wa wananchi.Huyu ni mtawala atawatetea wananchi dhidi ya nani anyewaonea? Yeye ni sehemu ya anayewaonea, hii itakuwa contrary to nemo judex in causa sua.

You are really a great thinker, you read between the lines and see in three dimensions not only that but also think outside the box
 
Binafsi namkubali sana huyu mama, nakumbuka mwaka 2012 mwishoni kipindi ni m/wilaya ya Tanga alitusaidia sana kwenye mgomo wa wanafunzi pale Galanos sec na mpaka leo vijana wanaenjoy tu mema ya nchi.
 
MFAHAMU MHE. HALIMA DENDEGO (RC-MTWARA).

Mhe. Halima Dendego kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Mtwara. Safari yake ya uongozi na harakati za kutetea haki za wananchi na raia wa Tanzania, zilianza tangu akiwa chuo kikuu cha Dar-es-salaam (UDBS-University of Dar-es-salaam Business School). Enzi hizo ilikuwa inajulikana kama Faculty of Commerce. Alikuwa miuongoni mwa wanaharakati machachali sana wa DARUSO kutokea fass kuanzia miaka ya 2001 mpaka alipomaliza elimu yake ya chuo kikuu.

Nyota yake na shauku ya kuwapigania watanzania bado iliendelea kung'aa kiasi kwamba akateuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa. Huko alijulikana sana kwa jinsi alivyokuwa karibu na wananchi ili kuhakikisha shughuli za maendeleo zinasonga mbele. Hakuona kuwa mkuu wa wilaya kuwa ni fahari kwake bali alipigania haki ya kila mwanampwapwa kwa nguvu zake zote.

Baada ya hapo alihamishiwa kilosa kwa nafasi hiyo hiyo ya ukuu wa wilaya. Ambako nako alikumbana na changamoto nyingi, kubwa ilikuwa ni vita na migogoro kati ya wafugaji na wakulima. Alitumia utashi wake kadiri alivyoweza kuweka hali sawa.

Baada ya kutoka kilosa akahamishiwa Tanga. Kabla ya kuteuliwa na Raisi kuwa mkuu wa mkoa wa Mtwara, ambako anatumikia mpaka sasa.

Falsafa yake ya kushirikiana na wananchi bega kwa bega bado aliendelea nayo. Ikumbukwe kuwa kwa kipindi ambacho aliingia mkoani mtwara ilikuwa ni kipindi kifupi tu kimepita tangu fujo zilizosabishwa na mzozo wa gesi na ujenzi wa Bomba la mafuta kuelekea DSM. Lakini hilo halikumvunja moyo, bali alihakikisha amani inaendelea kudumu ili shughuli za maendeleo zisonge mbele.

Akiwa mkuu wa mkoa wa Mtwara amefanya mambo mengi na mazuri jambo ambayo kila mwanamtwara anajivunia kuhusiana na huyu Mama. Zao la korosho amelibeba vilivyo kiasi kwamba sasa hivi tunajua thamani ya korosho jinsi ilivyo. Hakuna asiyefahamu jinsi Mhe. Halima Dendego alivyopambana na unyonyaji ambao ulikuwa unafanyika hasa kwenye hili zao la korosho, ama kwa hakika amejitoa mhanga juu ya jambo hili. Wanamtwara tushirikiane na kushikamana na mkuu wetu wa mkoa Jemedari wetu.

Mtwara ni yetu,
Nitasimama na mkuu wa mkoa wangu.View attachment 591754
ONGEZA NI MTOTO WA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CHAMA MOROGORO
MZEE DENDEGU

NI KWELI ALIFANYA VEMA FASS YA WAKATI ULE WAKATI KINA NANII WAKITAPATAPA NA KUHAMASISHA NA PUNCH NA MOGOMO.
 
Sijaona mchango wake ktk issue za kijamii kabla ya kuwa DC - nadhani ni konekisheni iliyombeba zaidi ya mengine mengi
 
MFAHAMU MHE. HALIMA DENDEGO (RC-MTWARA).

Mhe. Halima Dendego kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Mtwara. Safari yake ya uongozi na harakati za kutetea haki za wananchi na raia wa Tanzania, zilianza tangu akiwa chuo kikuu cha Dar-es-salaam (UDBS-University of Dar-es-salaam Business School). Enzi hizo ilikuwa inajulikana kama Faculty of Commerce. Alikuwa miuongoni mwa wanaharakati machachali sana wa DARUSO kutokea fass kuanzia miaka ya 2001 mpaka alipomaliza elimu yake ya chuo kikuu.

Nyota yake na shauku ya kuwapigania watanzania bado iliendelea kung'aa kiasi kwamba akateuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa. Huko alijulikana sana kwa jinsi alivyokuwa karibu na wananchi ili kuhakikisha shughuli za maendeleo zinasonga mbele. Hakuona kuwa mkuu wa wilaya kuwa ni fahari kwake bali alipigania haki ya kila mwanampwapwa kwa nguvu zake zote.

Baada ya hapo alihamishiwa kilosa kwa nafasi hiyo hiyo ya ukuu wa wilaya. Ambako nako alikumbana na changamoto nyingi, kubwa ilikuwa ni vita na migogoro kati ya wafugaji na wakulima. Alitumia utashi wake kadiri alivyoweza kuweka hali sawa.

Baada ya kutoka kilosa akahamishiwa Tanga. Kabla ya kuteuliwa na Raisi kuwa mkuu wa mkoa wa Mtwara, ambako anatumikia mpaka sasa.

Falsafa yake ya kushirikiana na wananchi bega kwa bega bado aliendelea nayo. Ikumbukwe kuwa kwa kipindi ambacho aliingia mkoani mtwara ilikuwa ni kipindi kifupi tu kimepita tangu fujo zilizosabishwa na mzozo wa gesi na ujenzi wa Bomba la mafuta kuelekea DSM. Lakini hilo halikumvunja moyo, bali alihakikisha amani inaendelea kudumu ili shughuli za maendeleo zisonge mbele.

Akiwa mkuu wa mkoa wa Mtwara amefanya mambo mengi na mazuri jambo ambayo kila mwanamtwara anajivunia kuhusiana na huyu Mama. Zao la korosho amelibeba vilivyo kiasi kwamba sasa hivi tunajua thamani ya korosho jinsi ilivyo. Hakuna asiyefahamu jinsi Mhe. Halima Dendego alivyopambana na unyonyaji ambao ulikuwa unafanyika hasa kwenye hili zao la korosho, ama kwa hakika amejitoa mhanga juu ya jambo hili. Wanamtwara tushirikiane na kushikamana na mkuu wetu wa mkoa Jemedari wetu.

Mtwara ni yetu,
Nitasimama na mkuu wa mkoa wangu.View attachment 591754
Umeuchoka mkoa wa mtwara au vp?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom