Mfahamu mkuu wa mkoa wa Mtwara

Mbesigwe

Member
Sep 27, 2016
51
54
MFAHAMU MHE. HALIMA DENDEGO (RC-MTWARA).

Mhe. Halima Dendego kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Mtwara. Safari yake ya uongozi na harakati za kutetea haki za wananchi na raia wa Tanzania, zilianza tangu akiwa chuo kikuu cha Dar-es-salaam (UDBS-University of Dar-es-salaam Business School). Enzi hizo ilikuwa inajulikana kama Faculty of Commerce. Alikuwa miuongoni mwa wanaharakati machachali sana wa DARUSO kutokea fass kuanzia miaka ya 2001 mpaka alipomaliza elimu yake ya chuo kikuu.

Nyota yake na shauku ya kuwapigania watanzania bado iliendelea kung'aa kiasi kwamba akateuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa. Huko alijulikana sana kwa jinsi alivyokuwa karibu na wananchi ili kuhakikisha shughuli za maendeleo zinasonga mbele. Hakuona kuwa mkuu wa wilaya kuwa ni fahari kwake bali alipigania haki ya kila mwanampwapwa kwa nguvu zake zote.

Baada ya hapo alihamishiwa kilosa kwa nafasi hiyo hiyo ya ukuu wa wilaya. Ambako nako alikumbana na changamoto nyingi, kubwa ilikuwa ni vita na migogoro kati ya wafugaji na wakulima. Alitumia utashi wake kadiri alivyoweza kuweka hali sawa.

Baada ya kutoka kilosa akahamishiwa Tanga. Kabla ya kuteuliwa na Raisi kuwa mkuu wa mkoa wa Mtwara, ambako anatumikia mpaka sasa.

Falsafa yake ya kushirikiana na wananchi bega kwa bega bado aliendelea nayo. Ikumbukwe kuwa kwa kipindi ambacho aliingia mkoani mtwara ilikuwa ni kipindi kifupi tu kimepita tangu fujo zilizosabishwa na mzozo wa gesi na ujenzi wa Bomba la mafuta kuelekea DSM. Lakini hilo halikumvunja moyo, bali alihakikisha amani inaendelea kudumu ili shughuli za maendeleo zisonge mbele.

Akiwa mkuu wa mkoa wa Mtwara amefanya mambo mengi na mazuri jambo ambayo kila mwanamtwara anajivunia kuhusiana na huyu Mama. Zao la korosho amelibeba vilivyo kiasi kwamba sasa hivi tunajua thamani ya korosho jinsi ilivyo. Hakuna asiyefahamu jinsi Mhe. Halima Dendego alivyopambana na unyonyaji ambao ulikuwa unafanyika hasa kwenye hili zao la korosho, ama kwa hakika amejitoa mhanga juu ya jambo hili. Wanamtwara tushirikiane na kushikamana na mkuu wetu wa mkoa Jemedari wetu.

Mtwara ni yetu,
Nitasimama na mkuu wa mkoa wangu.
IMG_20170919_180346_783.jpg
 
Nitasimama na mkuu wa mkoa wangu.View attachment 591754
Tunajua alikuwa bibi mdogo wa mfalme wa Mshoga na mkuu wa sijui wilaya sijui mkoa hawezi kuwa mtetezi wa wananchi.Huyu ni mtawala atawatetea wananchi dhidi ya nani anyewaonea? Yeye ni sehemu ya anayewaonea,hii itakuwa contrary to nemo judex in causa sua.
 
Yes anazosifa Nzuri za Uongozi hasa Uthubutu pia ana huruma nimeona kwa macho yangu akiwasaidua wenye shida pia anafikika in fact she is a True leader Over all RC's in recent years she has done a lot mm nafanya naye kazi I know what I mean Keep it up
 
Mabavicha ndio wa kwanza kuomba cv za watu,jana mliomba cv nya Namia,leo mtu amewarahisihia kazi ili tu muweke kwa matumizi ya kunyuka baadae,mnaponda aliewaroga kafa
 
ana kipi cha ziada labda?
Ni jasiri na mwenye kushirikisha sana anaowaongoza katika kifanya maamuzi. Hafanyi mambo kwa kukurupuka wala kwa kubahafisha. Nadhani kama ni mfuatiliaji unaweza ukafatilia vizuri jinsi soko la korosho kwa msimu uliopita ulivyokuwa.
 
Yes anazosifa Nzuri za Uongozi hasa Uthubutu pia ana huruma nimeona kwa macho yangu akiwasaidua wenye shida pia anafikika in fact she is a True leader Over all RC's in recent years she has done a lot mm nafanya naye kazi I know what I mean Keep it up
Ni kweli kabisa huwezi jua kama mboga inachumvi au haina kwa kuingalia. Sisi (wanamtwara) tunaelewa nini huyu mama anafanya. Tuko pamoja
 
Back
Top Bottom