Mfahamu Meja Jenerali Muhiddin Kimario. Ukisikia mzalendo ndio huyu

moyafricatz

JF-Expert Member
Nov 27, 2015
2,900
4,865
Marehemu Major Gen. Muhiddin Kimario, mmoja ya mawaziri wawili tu wa Mambo ya Ndani katika historia ya Tanzania kuwahi kudumu katika nafasi hiyo kwa zaidi ya miaka 5.

Alitumwa na Mwl Nyerere kuwaaga wanajeshi kwenda kumng'oa Nduli Idd Amin, akiwa anahutubia katika uwanja wa Nyamagana ghafla akajivua Uwaziri na yeye akaenda vitani.

" Mkuu wa mkoa naomba ufikishe taarifa hii kwa Mh Rais kwamba najivua Uwaziri na naamuwa kurudi Jeshini kuungana na wenzangu leo kwenda kumshikisha Adabu Amin"

Alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na pia mara mbili alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Aidha, alipata kuwa Mkuu wa Mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza na pia alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu, Dodoma – CDA. Vile vile, alikuwa Mbunge wa Moshi Mjini kwa vipindi vitatu mfululizo kati ya 1975 na 1990.

Marehemu alijiunga na TPDF Januari 10, Mwaka 1963 na alistaafu utumishi wa Jeshi Desemba 28, 1992, baada ya kulitumikia TPDF kwa miaka 29, miezi 11 na siku 17
IMG-20180718-WA0009.jpg
 
Huyu si ndiye aliifilisi CDA? Yeye na akina Feruzi na Aden Rage? Anaweza kasema ni mzarendo kwa kuipigania nchi yake, vipi kuliibia taifa kisa mjeda, haiingii akilini, hayupo kwenye kundi la mashujaa
 
Huyu si ndiye aliifilisi CDA? Yeye na akina Feruzi na Aden Rage? Anaweza kasema ni mzarendo kwa kuipigania nchi yake, vipi kuliibia taifa kisa mjeda, haiingii akilini, hayupo kwenye kundi la mashujaa
. Hiyo audit report ya mwaka gani ? Inayosema hivyo
 
Back
Top Bottom