Mfahamu kahaba mkuu wa Ufunuo 17

mimi ni ROMAN CATHOLIC na sitoacha kwenda kanisani sababu ya nyie manabii watu kwa sababu namuomba Mungu huko huko RC na nnabarikiwa sababu hiyo....so bro endelea kutafuta wakukuletea sadaka mi umenikosaa

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
Unafundishwa ukweli unakomaza shingo

Utakuja kukumbuka muda umeshakwenda

Usinifananishe na walokole hao ni vitukuu wa roman catholic

Endelea kushupaza shingo



YHWH IS GOOD
 
Kazi ya wasabato kuwashambulia wakatoliki..

Sent from my TECNO-W3 using JamiiForums mobile app
Mkiambiwa ukweli mnadai mnashambiliwa,

Hata Luther aliambiwa hivo hivo , na aligundua MAOVU NA MADANGANYO 95

Je leo yatakuwa mangapi?

Achana na ibada za sanamu, ibada za wafu, na upuuzi mwingine

YHWH IS GOOD
 
Unafundishwa ukweli unakomaza shingo

Utakuja kukumbuka muda umeshakwenda

Usinifananishe na walokole hao ni vitukuu wa roman catholic

Endelea kushupaza shingo



YHWH IS GOOD
Trust me wewe unayejifanya kanisa lako ni la kweli kuliko Mengine..jehanamu inakusubiri acha mimi na rais Wang JPM tuendelee kuinyoosha nchi ili tukawe malaika hata huko mbinguni..nyie mnaotafuta wafuasi kwa nguvu endeleeni.

NB..USHAURI WA BURE
kaka kizuri chajitangaza kibaya chajiuza
fanyakazi acha kujifanya malaika na umekamirika. hakuna binadamu wa kumhukumu binadamu ni Mungu tu

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
 
Trust me wewe unayejifanya kanisa lako ni la kweli kuliko Mengine..jehanamu inakusubiri acha mimi na rais Wang JPM tuendelee kuinyoosha nchi ili tukawe malaika hata huko mbinguni..nyie mnaotafuta wafuasi kwa nguvu endeleeni.

NB..USHAURI WA BURE
kaka kizuri chajitangaza kibaya chajiuza
fanyakazi acha kujifanya malaika na umekamirika. hakuna binadamu wa kumhukumu binadamu ni Mungu tu

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
Huyo ni Msabato...Msabato siyo Mkristo...
 
Kuna watu wameuliza maswali kuhusu kipindi cha miezi 42 kinaanza lini, kinaisha lini na kinamhusu nani. Biblia haikutuacha gizani, hebu fuatana nami.

Sasa tuangalie ile miezi 42 au miaka 3.5 au siku 1260

Ufunuo 11:1-2: “Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja akaniambia, Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wasujuduo humo. Na behewa iliyo nje ya hekalu uiache nje wala usiipime, kwa maana Mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arobaini na miwili.”

Huyo Mnyama alikuwa na nguvu kwa miezi 42 (Ufunuo 13,5.7) “Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.” Makufuru hapa ni pale mwanadamu anapojifananisha na Mungu.

Daniel 7:23-25: Akanena hivi, Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande. Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu. Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati ( yaani miaka mitatu na nusu).

Kibiblia mwezi una siku 30, mwaka wa kibiblia ni siku 360. Kwa hiyo miezi 42 = miaka 3.5 au siku 1,260. Katika hatua hii ni muhimu kutambua kwamba wakati wa unabii wa Biblia unasemwa kwa mifano, hivyo siku moja inawakilisha mwaka mmoja wa unabii wa kweli. (Ezekieli 4:6) Mungu anasema: "... Tena utakapozitimiza hizo, utalala kwa ubavu wako wa kuume, nawe utauchukua uovu wa nyumba ya Yuda; siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagizia.”

Kwa ujumla aya hizi zote huzungumzia suala moja nalo ni kipindi cha zama za giza. Kipindi amabacho kweli ya Neno la Mungu ilikanyagwa chini (Ufunuo 11:1-20). Hiki ni kipindi ambacho upapa ulipewa mamlaka ya dini na kiserikali kutoka utawala wa Rumi. Ufunuo 13:4. “ Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? “ . Hapa kila Taifa lilisalimu amri chini ya papa.


Utawala wa kirumi uliendelza mateso kwa mitume wa Yesu Kristo, lakini kadri walivyozidisha mateso ndivyo injili ilivyozidi kuenea. Baadae tunaona Shetani akibadili mbinu - kutoka mateso kwa Wakristo na kupitishwa kwa desturi za kipagani na ushirikina, kanisani kwa kumtumia mfalme Constantine mnamo karne ya 4. Huyu Constantine alijifanya ameongoka ma kuacha mateso kwa Wakristo. Furaja ikatawala miongoni mwa waumini kwani mtesaji amekuwa mmoja wao. Lakini lengo lake haukuwa uongofu wa kweli, bali kupata ushwawishi zaidi kwa kutumia dini. Hivyo akatumia ushawishi wake kuleta ibada za kipagani kanisani. mafundisho kama vile ubatizo wa watoto wachanga, ubatizo wa kunyunyizia maji kichwani badala ya kuzamisha majini kama Yesu alivyobatizwa, mafundisho ya kutokufa kwa roho, sala kwa ajili ya wafu na ibada ya sanduku, maombi ya kujurudia kutumia rozari, mateso ya purgatory na moto wa milele kuzimu, mafundisho ya wokovu kupitia matendo, uhalali wa hazina ya "watakatifu" wafu, Misa, maadhimisho ya Jumapili, n.k. Haya yote yalichukuliwa moja kwa moja kutoka Babeli ya kale. Katika muda mfupi - wakati wa karne ya 4 Constantine alichanganya upagani na Ukristo, alifungua mlango wa mafundisho ya uongo hatua kwa hatua na hatimaye kufanikiwa kabisa.

Mwaka 476 AD Mfalme Justnian wa rumi akaamua kumpa askofu mkuu wa Roma mamlaka ya kidini na kiserikali. Hapa tunaona unabii wa Ufunuo 13:4 ukitimia. Ukristo ukawa dini ya serikali na mamlaka ya kidini chini ya upapa. Hivyo upapa ukapata nguvu zaidi na kuanza kulazimisha utii kwa nguvu na kuwatesa wale waliokataa kumtambua mkuu wa kanisa la roma yaani papa. Kipindi cha upapa kutesa wakristo waaminifu kinaanzia mwaka 538 AD-1798 AD (miaka 1260 iliyosemwa na Biblia) wakati Mfalme Napoleon wa Ufaransa alipokataa kumtii papa na kumchukua mateka na kumuua . Ufunuo 13:10. “Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu.”

Ni papa gani alichukuliwa mateka na kuawa? Free Encyclopedia inamtaja Papa Pius VI (25 December 1717 – 29 August 1799), jina lake la kuzaliwa ni Giovanni Angelo Braschi, alitawala kama papa kuanzia 15 February 1775 hadi 1799 alipofariki.


Katika kipindi hiki cha miaka 1260. Kanisa la roma chini ya papa liliua watu wengi sana. Ukweli unabakia kuwa upapa uliua takriban watu milioni 100, ambao waliuawa kikatili kwa sababu walikataa kukubali mamlaka ya Kanisa Katoliki. Miaka ya hivi karibuni. Papa Yohane Paulo II alikiri kanisa katoliki kuhusika na mauaji haya. Jarida la Europe Rationalism Vol.2 Uk. Wa 32 huzungumzia mauaji haya kama ifuatavyo; "Kanisa Katoliki lilimwaga damu isiyo na hatia zaidi kuliko taasisi nyingine yoyote iliyowahi kuwepo duniani."

Mateso haya yalikoma rasmi mwaka 1798. Historia iko wazi. Manamo 10 Machi 1798, hasa baada ya miaka 1,260 uwezo wa kipapa ulikoma, baada ya Napoleon Bonaparte aliyemtuma mkuu wake wa majeshi Louis Alexandre Berthier kumpiga papa na jeshi la roma. Papa alikamatwa baada ya miezi 18 na kufa uhamishoni nchini Ufaransa Valencia. Tukio hilo lilihitimisha mamlaka ya kipapa.Na Biblia inaita tukio hili jeraha la mauti ambalo baadae lilipona. Ufuno 13:3 “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.”

Mwaka 1929 Serikali ya Italia ikaamua kuufanya mji wa vatican kama nchi huru . Papa tena akawa kiongozi wa kisiasa. Machi 9, 1929 alisema: "Watu wote ulimwenguni wako pamoja na sisi." Mfalme Mussolini na Gaspar wakasaini mkataba wa kihistoria na kutamka kuwa “jeraha la muda mrefu limepona."

Hivi ndivyo siku 1260 au miaka 1260 ilivyohitimishwa na kuibuka tena, na nguvu hii inatenda kazi sasa ili kurudisha mamalaka iliyopoteza enzi zake. Ndio maana Biblia hutuonya tuepuke kupokea alama na chapa ya mnyama huyu yaani ibada yake ya uongo (sanamu ya mnyama) yaani Jumapili, hata ikibidi kufa. Uwe mwaminifu hata kufa.

Ufunuo 13 :15-18 :Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;
tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.”
 
Hapa pazuri kwangu ngoja nifuatilie kwanza

Sent from my HUAWEI Y300-0100 using JamiiForums mobile app
 
Uliyoandika hapa yanahusianaje na niliyosema hapo juu? Na kwa nini una-assume kuwa kila mtu anayehojiana nanyi ni Mkatoliki? Mimi siyo Mkatoliki ila nimekulia katika Usabato na nimesoma kila uchafu wa Ellen mpaka nilipong'amua kuwa kumbe nilikuwa nafuata cult inayofuata mafundisho ya nabii feki tena mwehu mwenye matatizo ya ubongo, na kwamba mafundisho yake mengi ni ya kishetani japo yamepambwa kwa lugha tamu iliyojaa taswira za kutisha na njozi za kupumbaza. Kokotaneni na huyu nabii wenu mwenye hallucinations huku mkidanganyana kuwa mtakwenda mbinguni kwa kuwa tu eti mnasali Jumamosi. Blind fools!
Acha uongo wewe,wewe utakuwa ni kibaka tu wa mitaani,unaongea utumbo mtupu,bila shaka hujawahi kanyaga kanisa lolote,kama ulikaa kwa wasabato kisha ukatoka basi wewe una mtindio wa ubongo,huelewi na huta elewa kamwe

Sent from my SM-N910F using JamiiForums mobile app
 
Biblia ni kazi ya mikono ya Kanisa Katoliki...Hii hata mtoto mdogo anafahamu...usipende kujitoa ufahamu
Unaweza kusema ivo tu endapo ubongo wako wa mbele[cerebrum] una matatizo,kanisa linalobadili maneno ya Mungu,linalomrekebisha Mungu alichosema kwenye maandiko,linalosubutu kuandika"kwa mamlaka ya kanisa tumeamua kubadili amri hii".Biblia ni kazi ya Mungu,si mwanadamu,si kanisa fulani

Sent from my SM-N910F using JamiiForums mobile app
 
Acha uongo wewe,wewe utakuwa ni kibaka tu wa mitaani,unaongea utumbo mtupu,bila shaka hujawahi kanyaga kanisa lolote,kama ulikaa kwa wasabato kisha ukatoka basi wewe una mtindio wa ubongo,huelewi na huta elewa kamwe

Sent from my SM-N910F using JamiiForums mobile app
Tulia wewe...We ni Msabato...??
 
Unaweza kusema ivo tu endapo ubongo wako wa mbele[cerebrum] una matatizo,kanisa linalobadili maneno ya Mungu,linalomrekebisha Mungu alichosema kwenye maandiko,linalosubutu kuandika"kwa mamlaka ya kanisa tumeamua kubadili amri hii".Biblia ni kazi ya Mungu,si mwanadamu,si kanisa fulani

Sent from my SM-N910F using JamiiForums mobile app
Sijui ni weke kwa lugha gani..Jamani Biblia imekuwa Compiled na Kanisa Katoliki...Kanisa ndio limeipa Biblia dunia...hata wewe msabato ambaye siyo Mkristo unatumia Biblia...
 
Huwezi kukomaa na kamstari kamoja tu

Huo mji mkubwa ni Vatican

Na hiyo mistari ya ufunuo 17:1-17

Inamuelezea huyo mwanamke ambaye biblia inamtafsir ni kanisa

Sasa jiulize

Hapo vatican kuna kanisa gani

NA NDIO MAANA NIMEKUOMBA UJENGE HOJA AYA KWA AYA

Sasa unakimbilia aya moja ,unaacha aya 16

Upo seriously kweli wewe!

YHWH IS GOOD
Huyu anawapotezea muda tu ndugu sbb nlishamjengea hoja ambayo akakimbia na maswal hajajibu mpka leo pamoja na wenzie...leo kahaba katoka kua ukatoliki kawa mji wa vatican...hv unahisi wte n watoto kma ww kua unaeza kutuchanganyia maneno!hata hajui anatetea nini kaambiwa biblia inasema n mji kahama kutoka ukatolik kua mji...hya mbele ya mistari hyo kuna mistari inasema mji huo uko kati ya vilima saba yaani wafalme saba wamekaa...tukikwambia utaje utaweza..
 
Mbona unajitia mjuaji

Kwanini usipinge hoja zangu kwa maandiko

Toka karne ya 15 kina john huss

Martin luther, knox, sir isack newton walisema wazi wazi UFUNUO 13,. 17 , PEMBE NDOGO INALIHUSU KANISA KATOLIKI DHAHIRI

SASA WEW UNAPINGA BILA ANY EVIDENCE

HUSEMI HIYO PEMBE NDOGO AU HUYO KAHABA MKUU NI NANI

umebaki kulalamika tu

Sema ni nani, nianze aya moja moja unithibitishie inahusika vipi


MBONA MIMI NIMEKUONESHA KAHABA MKUU WA UF 17 NI KANISA KATOLIKI

TENA NIMETHIBITISHA AYA KWA AYA

unakimbilia aya ya 18

Huo mji ni VATICAN tena biblia inasema katika hiyo sura HUO MJI UPO KTK VILIMA 7 na ndio anakalia huyo mwanamke

Bado tu hufunguki?

Hujui ROMA VATICAN IMEZUNGUKWA NA VILIMA 7 ?

Au nikutajie kwa majina?


haya NJOO NA POROJO ZAKO

YHWH IS GOOD
Ukisema karne ya 15 unamaanisha miaka ya 1400-1499 ss je marthin luther alikuepo kipin hiki au unataka kutudanganya pia...mna unajaribu kuleta kila unachoweza il kujarbu kuwin na hoja ishakukataa ss...maswal yngu hujbu unakimbia
 
Mkuu acha ujuaji

Wewe njoo kuhusu hiyo pembe ndogo , maana mm nishaeleza,

Wewe si uje tuone nani atashindwa asubuhi kuliko kulalama tu, haitakusaidia kitu

YHWH IS GOOD
Tizama ijumaa na jumamos nmekuachia maswal ya kuhusu pembe ndogo umeruka hujajibu unakuja kuchanganya watu tena
 
uwe unaweka MAANDIKO sio kuropoka tu,



Ngoja nikuoneshe mfano , hii ni INTRODUCTION

Ndio maana andiko linasema : "Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI".
UFUNUO 17 : 5
Unaona hapo juu kwenye fungu, yani jina BABELI NI LA SIRI, hii ikimaanisha, Babeli hii itafanya kazi kwa namna ya kujificha na kutotaka ijulikane kuwa ndio Babeli yenyewe.
HEBU TUISOME KWANZA KATIKA MAANDIKO TUONE BIBLIA INACHOTUAMBIA KUHUSU BABELI HUYO MKUU NA MAMA WA MAKAHABA.
"Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;
2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.
3 Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.
5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.
UFUNUO 17 : 1 - 6
Hapo tunaona Yesu akimfunulia mtumishi wake Yohana juu ya ujio mpya wa BABELI duniani. Haya matukio Yohana alifunuliwa kama matukio yaliyo mbele, yani yajayo baada ya siku zake. Yesu alifunua kuwa itaibuka tena BABELI lakini kwa sura tofauti kabisa na Babeli ile iliyozoeleka.
Kwa kutumia lugha ya mafumbo Yesu anamfunua BABELI huyo mkuu na MAMA WA MAKAHABA.
Sasa tunataka tumjue KAHABA HUYU MKUU NA AMBAYE NI MAMA WA MAKAHABA PIA, AITWAYE BABELI MKUU NI NANI?
Kwa kuwa haya ni mafumbo ya kimbingu, hatupaswi kujaribu kuyafumbua kibinadamu, tutaliacha Neno la Mungu litufunulie BABELI HUYU MKUU NA MAMA WA MAKAHABA ni nani?
BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA NI NANI AU NI NINI?
Biblia inamfunua..
1. Kwanza tunaona BABELI MKUU huyu ameonyeshwa kuwa ni mwanamke, maana anaitwa "mama" sote tunaelewa sifa ya mama ni ya jinsi ya kike.
Je, kwa mujibu wa Biblia mwanamke hutumika kuwakilisha nini anapotumika kama kielelezo?
- Katika Biblia "mwanamke" hutumika kuwakilisha "JAMII YA WATU WA MUNGU" ambao katika agano la kale watu hao walikuwa ni taifa la "ISRAELI"
Tunaona katika Hosea Mungu akiongea na watu wake kama aongeae na mwanamke
Nami nitakuposa uwe wangu kwa milele; naam, nitakuposa kwa haki, na kwa hukumu, na kwa ufadhili, na kwa rehema.
HOSEA 2 : 19
"Rudini, enyi watoto wenye kuasi, asema BWANA; maana mimi ni mume wenu; nami nitatwaa mtu mmoja wa mji mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami nitawaleta hata Sayuni;
YEREMIA 3 : 14.
Katika zama za agani jipya, ambapo hakuna tofauti tena kati ya Myahudi na asiye Myahudi, mwanamke anawakilisha watu wa Mungu kwa maana ya "KANISA"
Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.
2 KORINTHO 11 : 2
Kwa sababu BABELI MKUU atatokea wakati wa Agano jipya, basi BABELI huyo ATAJITOJEZA KATIKA SURA YA KANISA!
Tumejua sasa KAHABA MKUU ni kanisa kumbe.
Tuendelee...,
KWA MAANA HIYO KUMBE, KATIKA KUMSEMA BABELI MKUU YESU ALIKUWA AKIFUNUA KUHUSU KUTOKEA KWA KANISA FULANI KATIKA SIKU ZA BAADAE TOKA KATIKA SIKU HIZO ZA YOHANA WA PATMO.
2. MWANAMKE HUYO BABELI MKUU ANAONEKANA ANA SIFA YA ZIADA MBALI YA UANAMKE WAKE, ANA SIFA YA "UKAHABA"
Hii maana yake ni nini?
Katika Maandiko, mahusiano baina ya Mungu na watu wake yamefananishwa na "MAHUSIANO YA NDOA"
rejea Yeremia 3 : 14, na 2 Wakorintho 11 : 2.
Yani kanisa ni mke wa Kristo, kwa maana hiyo UKAHABA NI TENDO LA KANISA KUTOKUWA NA UAMINIFU KWA KRISTO.
Hapo tunaona KANISA HILO (Babeli mkuu) litakuwa ni kanisa lisilo na uaminifu kwa KRISTO, yani litakuwa na mabwana wengine, na waume wengine tofauti na Kristo
Lakini pia katika Hosea 3 : 1 inaonyesha UKAHABA WA WATU WA MUNGU NI KUABUDU MIUNGU WENGINE, TOFAUTI NA MUNGU WAO.
Hivyo kanisa hilo litakuwa linachanganya ibada ya Mungu Muumbaji, na ibada za miungu wengine, HUO NDIO UKAHABA WA KANISA HILO.
BABELI MKUU ALIKUWA AMEKETI JUU YA MAJI MENGI.
Maji mengi ni nini?
"Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha".
UFUNUO 17 : 5
Hii inaonyesha kuwa kanisa hilo, litasambaa dunia nzima, kwenye kila makutano, kila kabila, kila lugha na kila jamaa litakuwepo.
Lakini pia, inaonyesha kanisa hili, litakuwa ni kanisa la WATU WENGI, litakuwa ni kanisa kubwa na lenye kila aina ya watu ndani yake, kwa idadi kubwa sana.
3. BABELI MKUU (kanisa) ALIKUWA AMEPANDA MNYAMA.
Mnyama anapotumika kama kielelezo huwakilisha "FALME au TAWALA.
Soma Daniel 7 : 17 na Daniel 7 : 23
"Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea dunian".
DANIEL 7 : 17.
Kama ambavyo mtoto aliyebebwa anavyomtegemea aliyembeba, ndivyo kanisa hilo (BABELI MKUU). litakavyokuwa linategemezwa na serikali za kidunia. Nguvu zake, ustawi wake utatokana na kusaidiwa na mataifa au serikali za kidunia.
4. BABELI MKUU (kanisa) ATAZINI NA WAFALME.
Hii ina maana sawa na kubebwa juu ya mnyama, lakini imeongeza uzito wa kitendo chenyewe, neno KUZINI ina maana kanisa hilo litajitegemeza kwa wafalme wa dunia na kushikamana nao, kana kwamba wao ndio wenye kanisa. Nafasi ya Kristo itaondolewa na kama matokeo ya Kristo kwa kanisa hilo itatwaliwa na wafalme hao.
5. BABELI MKUU (kanisa) AMEWALEVYA WAKAAO JUU YA NCHI KWA MVINYO WA UASHERATI WAKE.
Kwanza kabisa tuliona UASHERATI WA KANISA HILO NI KUTANGA MBALI NA KRISTO, PIA KUABUDU VINGINE VISVYO MUNGU MUUMBAJI.
Sasa hapa twafunuliwa kuwa, KANISA HILO LITAWAAMBUKIZA WALIMWENGU UASHERATI WAKE, KWA NJIA YA MAFUNDISHO YA UONGO.
MAFUNDISHO YA UONGO ndio mvinyo wa uasherati wake. Watu wataabudishwa ibada zisizokubalika kimaandiko na kanisa hilo, watu watapiga magoti mbele ya miungu ya kigeni kwa maelekezo ya kanisa hilo.
Kulewa ni kuondolewa utambuzi, jambo ambalo ukiwa na akili timamu huwezi kukubali kulifanya, ukilewa unalifanya vzr tu.
Ndivyo itakavyokuwa kwa watu hao, kama wasingenyweshwa (wasingedanganywa) mvinyo (mafundisho ya uongo) wangetambua kuwa ibada hizo ni batili na hazikubaliki.
Lakini akili hiyo ya utamuzi imeondolewa na mvinyo huo wa uasherati wa kanisa hilo.
Na Biblia inathibitisha kuwa MAFUNDISHO YA UONGO YANALEVYA, Isaya 29 : 9, 10
6. ALIKUWA NA MAJINA YA MAKUFULU KATIKA KICHWA CHAKE.
Zingatia majina hayo hayakuwa mguuni, tumboni wala mgongoni, bali yalikuwa kichwani..,
Hii maana yake ni kuwa VIONGOZI WA KANISA HILO WATAJIPA MAJINA YANAYOMSTAHILI MUNGU.
7.BABELI MKUU ALIKUWA AMEVAA NGUO YA ZAMBARAU NA NYEKUNDU.
Hii nguo maana yake nini?
Tunaposoma maandiko, tunaona RANGI NYEKUNDU MAANA YAKE NI DHAMBI, Soma Isaya 1 : 18
"Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
ISAYA 1 : 18
Katika BIBLIA za lugha zingine mfano Biblia ya lugha ya kinyarwanda, imetaja kabisa na rangi ya zambarau pia katika fungu hilo la ISAYA.
Hivyo mavazi hayo yanaonyesha DHAMBI za kanisa. Litakuwa ni kanisa linalounga mkono dhambi, litakuwa ni kanisa ambalo lenyewe limeifanya dhambi kuwa ndio kanuni yake ya utendaji.
8. BABELI MKUU AMEPAMBWA KWA VITO, NA LULU
Hii inamaanisha nini?
Hizi, ni ishara za utajiri!
Kanisa hilo, litakuwa ni kanisa tajiri mno, lenye kuonekana wazi kwa utajiri wake, sawa na mapambo ya mwanamke yanavyoonekana wazi.
Litakuwa ni kanisa tajiri sana!
9.KIKOMBE CHA DHAHABU KILICHOJAA MACHUKIZO.
hii ina maanisha nini?
Dhahabu inaonyesha UPENDO., hili litakuwa ni kanisa ambalo litaonekana kuwa na matendo ya upendo.
Lakini kama ambavyo kikombe hicho cha dhahabu ndani kilivyokuwa na machukizo, kadhalika ndani ya hayo yatakayoonekana ni matendo ya Upendo kutakuwa na hila ya kuwaingiza watu katika kufanya MACHUKIZO dhidi ya Mungu.
10.AMELEWA KWA DAMU YA WATAKATIFU
Hii maana yake ni nini?
Kanisa hilo litawaua watu wa Mungu. Litamwaga damu ya watu ambao watakataa kushiriki uchafu wake.
11. Ana jina la siri "BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
Hii inamaanisha nini?
Kwanza tunaona hilo ni jina la siri, jina ambalo hakutaka lifahamike. Ndio maana akaja kwa sura ya mwanamke, yani alitaka afahamike kama mwanamke, kumbe hasa si mwanamke bali ni BABELI MKUU!
umeelewa mchezo?
Tuonane katika sehemu inayofuata kwa ufafanuzi wa mbinu hiyo ya kuficha jina, kuna mambo ya muhimu na nyeti sana tupaswayo kuyafahamu

YHWH IS GOOD
Unamfahamu mfalme Nimrod aliyekaa babeli na kuleta kuabudu miungu...au hujui kma ibada zte za miungu zlianzia babeli?au hujui Israeli yakaa ikizungukwa na mataifa ya babeli yaliyokua yakiabudu miungu...au hata upagan wa warumi na mashariki ya kati yte hujui ulitokea wap?au bx hujui hata miji iliyokua inatengeneza ufalme wa babeli(babeli ya nebukadreza)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom