Hivi ulishawahi kuona binadamu waliozaliwa na utofauti wa kimaumbile? mfano mtu kua na jicho moja,sehemu za siri mbili yaani za kike na za kiume kwa pamoja, mtu kua na mikono mitatu nk...
Basi unaambiwa kua kuna watoto wengi sana mahospitalini huzaliwa wakiwa na muonekano watofauti na binadamu wa kawaida lakini hukatishiwa uhai.
Leo nakuletea stori ya JOSEPHINE MYRTLE CORBIN huyu alikua ni raia wa marekani alizaliwa akiwa na miguu minne ambayo ilijigawa kwa pande mbili yaani upande wa kushoto ulikua na sehemu yake ya siri vivyo hivyo na kwa upande wa kulia na kila upande ulikua na uwezo wa kushika mimba vizuri bila matatizo.
kutokana na utofauti wake wa kimuonekano alikua akifanya kazi ya kutumbuiza kwenye majukwaa mbalimbali ya matamasha na burudani alijizolea umaarufu na kuteka umati wawatu popote alipoonekana watu walifurahia kumuona na wakishangaa kwa jinsi alivyo.
Alipofikisha miaka 19 aliolewa na daktari mmoja kwa jina JAMES CLINTON BICKNELL hukohuko marekana na kufanikiwa kupata watoto watano,wawili toka upande wa kushoto wa sehemu za uzazi na watatu toka upande wa kulia,alifariki akiwa na miaka 59.Watoto wanne walikua wa kike na mmoja wa kiume.
HISTORIA KWA UFUPI
Alizaliwa May 12, 1868, Lincolin county, USA
Alikufa May 6, 1928, Cleburne texas USA
Mahali alipozikwa :Cleburne
Watoto:5 (2 upande wa kushoto na 3 upande wa kulia)
Mume:JAMES CLINTON BICKWELL
Urefu: futi 5.1