Mfahamu Generali Evariste Ndayishimiye; Rais mtarajiwa wa Burundi, msiri wa Nkurunziza, mbabe wa vita na mnyenyekevu

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
946
Tarehe 20/5/2020 uchaguzi mkuu wa Burundi ulifanyika na matokeo ya urais yalitangazwa na mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi ndugu Pierre Claver Kazihise, ambapo mgombea wa chama cha CNDD_FDD Generali Evarist Ndayishimiye alipata asilimia 68.7 sawa na kura 3,082,210 huku mpinzani wake wa chama cha CNL naibu spika wa Bunge la Burundi ndugu Agathon Rwasa akipata asilimia 24.19 sawa na kura 1,084,788. Jumla ya wapiga kura millioni tano walijiandikisha huku watu zaidi ya 87534 hawakwenda kupiga kura.

Matokeo ya jumla yatatolewa tarehe 4/6/2020 kuonyesha wabunge na madiwani.

Generali Evarist Ndayishimiye ataapishwa mwezi wa nane kuchukua nafasi ya Pierre Nkurunzinza ambaye amekuwa madarakani kwa miaka kumi na tano tangu mwaka 2005 alipochukua nchi kutoka kwa Domitien Ndayizeye.

Generali Evarist Ndayishimiye ndiye katibu Mkuu wa chama cha CNDD_FDD ambacho ni chama dola nchini Burundi kutokana na kuwa na ushawishi na ushirika mkubwa ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama Burundi.

Generali Evarist Ndayishimiye ni kipenzi cha Pierre Nkurunzinza kwa sababu ya urafiki wao tangu chuo kikuu cha Burundi, mafunzo ya kijeshi nchini Congo, vita vya Burundi na makubaliano ya Arusha kupokezana madaraka mwaka 2004_2005.

Harakati za kumuondoa madarakani Pierre Buyoya nchini Burundi zilifanikiwa kwa ujumla wake kutokana na urafiki kati ya Generali Evarist na Pierre Nkurunzinza kwenye uwanja wa vita. Unyenyekevu, ukarimu na upendo aliouonyesha Generali Evarist Ndayishimiye kwa Raisi Pierre Nkurunzinza ndio sababu kuu ya kupitishwa na chama chake kuwa mgombea wa uraisi wa Burundi na kwa sasa ndio mshindi bado kuapishwa mwezi Agasti.

Generali Evarist jina lake la vitani ni Generali NEVER au NEVA, kutokana na ari yake ya kutokata tamaa kwenye uwanja wa mapambano, na alikuwa anawahamasisha wenzake vitani.

Generali Evarist Ndayishimiye alizaliwa mwaka 1968 jimbo la Gitega kipindi hicho Burundi inatawaliwa na Mbabe wa vita kutoka kabila la Wahutu Generali Michel Micombero(1940_1983) , kipindi hicho kulikuwa na machafuko Burundi ambapo Warundi wengi walikuja Tanzania, kwa sasa hivi wengi wao ni raia tayali.

Gitega ndio mji mkuu wa Burundi kutokana na juhudi za Pierre Nkurunzinza kudumisha amani na utulivu hivyo akaamua kuhamisha makao makuu kutoka Bujumbura mpaka Gitega.

Baada ya mauaji ya kikatili ya muasisi wa demokrasia nchini Burundi Raisi Melchior Ndadaye (1953_1993), ambaye alikuwa Raisi wa Burundi kwa siku tisini tu baada ya kushinda uchaguzi Mkuu wa huru na haki dhidi ya Pierre Buyoya. Machafuko ya kisiasa Burundi yalianza kwa kasi kutokana na wananchi kulishambulia Jeshi la Burundi kwa hatua ya mauaji ya Melchior Ndadaye.

Katika machafuko ya kisiasa Burundi Evarist Ndayishimiye alikoswa kuuawa mwaka 1995 akiwa mwanafunzi wa sheria katika chuo kikuu cha Burundi huku Pierre Nkurunzinza akiwa Mwalimu wa chuo hicho.

Pierre Nkurunzinza na Evarist Ndayishimiye walikimbia Burundi na kwenda Goma nchini Congo kuungana na waasi wa CNDD ili kupanga mipango mizito ya kuikomboa Burundi kutoka kwa mbabe wa vita Pierre Buyoya. Walipata mafunzo ya kijeshi wakiwa marafiki wakubwa chini ya Generali Leonard Nyangoma, ambaye alikuwa Swahiba mkubwa wa Generali Joseph Desire Mobutu Sese Seku Kuku Ngendu Wa Zabanga 1930_1997, ambaye alikuwa Raisi wa pili wa Congo kuanzia mwaka 1965 baada ya kumpindua Joseph Kasavubu mpaka alipopinduliwa mwaka 1997 na operesheni nzito iliyosukwa nchini Tanzania. Mobutu alikuwa anaunga mkono juhudi na mikakati ya Wahutu Burundi na Rwanda ndio maana alikuwa Swahiba mkubwa na Meja Generali Juvenile Habyalimana ambaye alikuwa Raisi wa pili wa Rwanda kuanzia mwaka 1973 mpaka alipouawa mwaka 1994 kwenye ndege akiwa na Rais wa Burundi Cyprian Ntaryamila na baadae kupelekea mauaji ya haraiki Rwanda kati ya Wahutu wa Akazu dhidi ya Watutsi.

Kutokana na kugombea madaraka na kutoaminiana miongoni mwa waasi wa CNDD hivyo mwaka 2000 waasi hao waligawanyika kwenye makundi mawili yaani CNDD chini ya Generali Leonard Nyangoma na CNDD_FDD chini ya Generali Evarist Ndayishimiye, Pierre Nkurunzinza, Hussain Radjabu, Generali Adolphe Nshimirimana, Allain Bunyoni na wengine wengi.

Kwenye makubaliano ya Arusha ili kusitisha vita Burundi Pierre Nkurunzinza alimchagua Evarist Ndayishimiye kwenda Arusha kukutana na wanadiplomasia ambapo Marehemu Nelson Mandela alihudhulia kama mpatanishi. Katika makubaliano hayo miez kumi na nane na utawala wa mpito kati ya Wahutu na Watutsi waliridhiana.

Mwaka 2003 mbabe wa vita Pierre Buyoya alijiuzuru nafasi ya uraisi na Domitien Ndayizeye akawa raisi wa Burundi. Na mwaka 2005 Pierre Nkurunzinza akachukua nchi. Wakati huo Evarist Ndayishimiye akaapishwa kuwa Meja Generali wa Jeshi la Burundi.

Kutokana na uweredi, unyenyekevu, nidhamu na utiifu kwa Raisi Pierre Nkurunzinza ikabidi apewe nafasi mbalimbali na vitengo nyeti vya intelijensia ya Burundi.

Mwaka 2006_2007 Raisi Pierre Nkurunzinza alimchagua Generali Evarist Ndayishimiye kuwa Waziri wa mambo ya ndani na usalama wa raia, wakati huo akiwa mshauri Mkuu wa Raisi kwenye usalama na jeshi la Burundi.

Mwaka 2008_2015 Generali Evarist Ndayishimiye alikuwa mshauri Mkuu wa kijeshi wa Burundi, mchora mipango ya misafara ya Raisi, katibu Mkuu wa chama cha CNDD_FDD, Mkuu wa nidhamu kwenye usalama wa Taifa wa Burundi, mshauri wa mawaziri nchini Burundi.

Mwaka 2015 baada ya Raisi Pierre Nkurunzinza kutangaza kugombea kwa awamu ya tatu huku akikiuka makubaliano ya Arusha, watu wengi waliandamana na uchaguzi wa kibabe ulifanyika na hatimae Pierre Nkurunzinza alishinda kibabe. Watu zaidi ya 1500 walikufa huku zaidi ya 400,000 wakakimbilia Tanzania, Uganda, Rwanda na Congo.

Tarehe 26/1/2020 mkutano Mkuu wa chama cha CNDD_FDD chini ya Raisi Pierre Nkurunzinza ulimpitisha Generali Evarist Ndayishimiye kuwa mgombea uraisi kwenye uchaguzi ambao umefanyika tarehe 20 Mei ambapo Generali Evarist Ndayishimiye ameshinda kwa asilimia 68.7

Mwaka 2005 baada ya Pierre Nkurunzinza kuwa Raisi wa Burundi na hali ya amani kurejea, Generali Evarist Ndayishimiye aliamua kurudi chuoni kumalizia shahada yake ya sheria ambapo mwaka 1995 aliacha akiwa mwaka wa pili kulingana na machafuko ya kisiasa.

Generali Evarist Ndayishimiye anaweza kuongea lugha nne kwa ufasaha ambazo ni Kirundi, Kifaransa, Kiingereza na Kiswahili. Generali Evarist Ndayishimiye ni muumini wa dhehebu la Katoliki na ana watoto sita kutoka kwa mke wake Angelina Ndayubaha.

Vipaumbele na ahadi za Generali Evarist Ndayishimiye kwenye uchaguzi na kampeni zake kwenye majimbo mbalimbali ya Burundi.

Mosi, kudumisha ulinzi na usalama wa Burundi hasa usalama wa raia, mali zao na kupunguza magendo mipakani hasa mipaka ya Burundi na Rwanda, Burundi na Congo na sehemu zingine, kudhibiti uharamia na utekaji ziwa Tanganyika hasa waasi wa Congo.

Pili, Wakimbizi walionchi mbalimbali hasa Tanzania, Uganda, Rwanda, Congo na nchi za ughaibuni wanapaswa kurejea Burundi ili kuijenga nchi yao, hapo atahakikisha amani na mshikamano nchini Burundi.

Tatu, uchumi wa Burundi ni kipaumbele kikubwa kwenye uongozi wake hasa kuzalisha kahawa bora, kupanua zao la michikichi, uvuvi wa kisasa, soko la Rumonge kuwanuliwa ili wafanyabiashara wa samaki waongezeke. Kutanua bandari ya Bujumbura, Rumonge na Kabonga.

Nne, Kuleta mikakati kabambe kudhibiti ukabila, udini na uchama, anasema kila Mrundi anapaswa kufuata sheria za nchi.

Tano, kudumisha uhusiano kati ya Burundi na majirani zake mfano nafasi ya Burundi kwenye mdororo wa jumuia ya Afrika mashariki, uhusiano kati ya Burundi na Rwanda ambao umejaa uongo, upotoshaji na chuki tangu mauaji ya kimbali mwaka 1994.

Sita, kukarabati miundombinu mbalimbali ya kiuchumi na kijamii hasa shule na vyuo vikuu, hospitali, barabara, huduma za mawasiliano, ili kutanua ajira kwa Warundi hii itasaidia kupunguza uasi na uroho.

Saba, utunzaji wa mazingira huku akiahidi kufufua harakati na sera ya kupanda miti iliyoanzishwa na Marehemu Melchior Ndadaye mwaka 1993 sera hiyo ya kupanda miti iliitwa "Ewe Burundi Urambaye "

Hizo ndizo ahadi za Generali Evarist Ndayishimiye kwenye kampeni zake hivyo inabidi Warundi wamuunge mkono na wampe ushirikiano ili aweze kuivusha nchi hiyo kiuchumi, kisiasa na kiitikadi.

Swali la msingi ni kwanini Raisi Pierre Nkurunzinza amemsaidia Generali Evarist Ndayishimiye kuwa Raisi wa Burundi?

Mosi, Generali Evarist Ndayishimiye na Pierre Nkurunzinza na marafiki tangu chuo kikuu cha Burundi wakati Nkurunzinza akiwa muhadhiri huku Evarist Ndayishimiye akiwa mwanafunzi wa sheria.

Pili, Generali Evarist Ndayishimiye alikuwa mlinzi wa Pierre Nkurunzinza wakiwa kwenye mafunzo ya kijeshi nchini Congo chini ya Generali Leonard Nyangoma huko Goma.

Tatu, Generali Evarist Ndayishimiye alikuwa mtiifu, mnyenyekevu na mshauri bora wa Pierre Nkurunzinza kwenye masuala ya ulinzi na usalama wa Burundi.

Nne, Generali Evarist Ndayishimiye aliwatia adhabu kali watu ambao walilenga kuhujumu utawala wa Pierre Nkurunzinza, wengine wanadai kwamba ni muuaji hatari sana kwenye serikali ya Pierre Nkurunzinza hata mauaji ya Generali Aldophe Nshimirimana tarehe 21/8/2015 nyumbani kwake na watu wasiojulikana yalipangwa na Generali Evarist Ndayishimiye. Pia Mwanaharakati Zedi Ferouzi aliuawa mwaka 2015 kwenye uchaguzi wa awamu ya tatu ya Pierre Nkurunzinza. Muasisi wa CNDD Hussain Radjabu alivuliwa uwenyekiti wa chama kutokana na fitina za Evarist Ndayishimiye na baadae kufungwa jela yote hii ni mipango mizito ya Generali Evarist Ndayishimiye kumlinda Pierre Nkurunzinza.

Tano, Generali Evarist Ndayishimiye ndiye aliyemuunganisha Pierre Nkurunzinza kwa Generali Yoweri Kaguta Museveni, Raisi wa Uganda tangu mwaka 1986. Baada ya uhasama kati ya Generali Paul Kagame na Pierre Nkurunzinza ikabidi Generali Evarist Ndayishimiye amuunganishe kwa Museveni kwa sababu Museveni anammudu Kagame kijasusi na intelijensia. Ndio maana Museveni alitangaza Wazi kumuunga mkono Pierre Nkurunzinza.

Sita, Generali Evarist Ndayishimiye, Generali Adolphe Nshimirimana, Generali Emmanuel Ntahomvukiye, Generali Prime Niyongabo na Generali Etienne Ntakirutimana walifanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi ya kijeshi nchini Burundi tarehe 13/5/2015 yaliyotangazwa na Generali Godefroid Niyombare aliyekuwa Waziri wa ulinzi na usalama wa Taifa Burundi. Mapinduzi hayo yalikuwa na mkono wa serikali ya Rwanda chini ya Generali Paul Kagame.

Saba, Generali Evarist Ndayishimiye ndiye anafahamu siri za mali na utajiri wa Raisi Pierre Nkurunzinza hivyo alimpigia upatu wa uraisi ili amlinde baada ya kustaafu mapema mwezi Agasti mwaka huu.

Nane, Raisi Pierre Nkurunzinza ana hofu ya kushitakiwa baada ya mauaji ya mwaka 2015 punde baada ya kutangaza kugombea kwa awamu ya tatu, ambapo zaidi ya watu 1500 waliuawa na jeshi la Burundi huku zaidi ya watu 400,000 wakikimbia nchi hiyo. Hivyo basi Pierre Nkurunzinza akaamua kumchagua Generali Evarist na ili amlinde.

Hitimisho, uchaguzi umekwisha nchini Burundi hivyo basi ni muda kwa Warundi kumpa nguvu Raisi wao mpya Evarist Ndayishimiye ambaye anatazamiwa kuapishwa mapema mwezi Agasti. Ukomavu wa kisiasa kwa wapinzani unahitajika ili kulinda amani na utulivu wa Burundi. Agathon Rwasa anapaswa kujikita kwenye mbinu za kidiplomasia na Majadiliano kudai haki yake kama anavyodai kwamba uchaguzi haukuwa huru na haki.
 
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchaguzi ulijaa hila, ubabe, uonevu, vitisho na ubambikiwaji wa kesi kwa upinzani bila kusahau rushwa....

Hata kama ni mzuri kiasi gani... Uchaguzi kwa jinsi ukivyoenda unamuondolea sifa njema

Jr
Kwa East Africa uchaguzi wa haki ni Kenya pekee huko kwingine ni maigizo ya tume za uchaguzi
 
Hongera kwa general evariste Ndayishimiye ambae pia alipitia mafunzo pale moduli
 
Isingekuwa hivyo KANU ingekuwepo mpaka leo
rejea uchaguzi wa juzi ambao matokeo yalibadilishwa mahakama,na ule uchaguzi wa maigizo ambao kenyata alishinda kwa kishindo.. unaona ulikuwa na todauti gan na ule wa zanzibar?
 
Back
Top Bottom