Neno Baharia limekua maarufu sana recent days, lakini nitajaribu kuelezea tabia za Baharia Kwa uelewa wangu. Kwanza baharia ni muhuni asiyefeli hii ntaielezea kupitia mifano
Wakati nasoma o level kuna jamaa alikua muhuni muhuni mvivu hapendi shule, lakin matokeo ya form four alifaulu kuanzia shuleni mtaani mpaka kwao hakun aliyeamin kama amefaulu, na staili hiyo hiyo akamaliza chuo yule ni sawa na Baharia
Kuna jamaa karibia mwaka wote wa form four alikua anaumwa sana na vidonda vya tumbo, lakin jambo la kustaajabisha alipata division 1 form kutoka na hali aliyokua nayo. Sababu hata NECTA alifanya huku anaumwa, yaan baada ya mtihan badala ya kujianda na mtihan ujao anaenda kulala. Kwanin namuita Baharia alikataa katu katu kuhairisha kufanya NECTA japokuwa hali yake ilikua mbaya.
Kuna jamaa tulisoma nae chuo huyu jamaa ulikua unaomba asije kwenye group discussion, Kwa sababu siku hy akija ni story mwanzo mwisho hamna kusoma au kudiscuss. Ikija presentation haji na mwalimu hatagundua na sio kwamba ana honga hapana ni inatokea tu huyu naye alikua Baharia.
Kuna mbaba mmoja yeye kukaa baa mpaka saa nane ni kawaida, ila hutakaa usikie ana mgogoro na mke wake, na kama upo ana umalizia ndani Kwa ndani. Na pia hutakaa usikie watoto wake wamerudishwa ada shule, huyu naye namuweka kwenye kundi la mabaharia.
Baharia mshipa wa uoga au aibu umeshakatwaga na kutupwa uko India, yaani yeye kutongoza mwanamke ni jambo ambalo hajali kukataliwa na huwez mkuta ana lalamika Kwa watu, hata kama ni mbele ya kadamnasi ata msimamisha mwanamke na kumuomba namba na tecno yake ya batani.
Na kuna jamaa yeye ni kuuza mali za uwizi na mirungi, lakin yule jamaa hapajui mahakaman pamefananaje kesi zake zote anazimalizia polisi, huyu naye ni baharia.