Mfahamu Baharia wa meli, Idara za meli na nafasi za mabaharia katika meli

Hao wanapaka rangi gani?wapi?
Wanapaka rangi kwenye meli. Rangi wanazopaka ni kwa ajili ya kuzuia kutu sababu meli muda wote ipo kwenye maji.

Kabla ya kupaka kuna kazi ya kugonga nyundo eneo hilo (Chipping) baadae wanasafisha na msasa ndio rangi inapakwa.

Hizi kazi ni kila siku kwa kuwa chombo kipo majini. Ndio maana unaambiwa melini kazi haziishi.
 
Mbona sijaona idara ya wanawake wenye makalio makubwa, wala sijaona idara ya wanyama pori?
Kigwangala njoo utuambie wewe ni baharia wanini, au ungo?
Sijaona hata idara ya michezo Haji aje atuambie nafasi yake ya ubaharia iko wap kwa maelezo hayo???
 
Neno Baharia limekua maarufu sana recent days, lakini nitajaribu kuelezea tabia za Baharia Kwa uelewa wangu. Kwanza baharia ni muhuni asiyefeli hii ntaielezea kupitia mifano

Wakati nasoma o level kuna jamaa alikua muhuni muhuni mvivu hapendi shule, lakin matokeo ya form four alifaulu kuanzia shuleni mtaani mpaka kwao hakun aliyeamin kama amefaulu, na staili hiyo hiyo akamaliza chuo yule ni sawa na Baharia

Kuna jamaa karibia mwaka wote wa form four alikua anaumwa sana na vidonda vya tumbo, lakin jambo la kustaajabisha alipata division 1 form kutoka na hali aliyokua nayo. Sababu hata NECTA alifanya huku anaumwa, yaan baada ya mtihan badala ya kujianda na mtihan ujao anaenda kulala. Kwanin namuita Baharia alikataa katu katu kuhairisha kufanya NECTA japokuwa hali yake ilikua mbaya.

Kuna jamaa tulisoma nae chuo huyu jamaa ulikua unaomba asije kwenye group discussion, Kwa sababu siku hy akija ni story mwanzo mwisho hamna kusoma au kudiscuss. Ikija presentation haji na mwalimu hatagundua na sio kwamba ana honga hapana ni inatokea tu huyu naye alikua Baharia.

Kuna mbaba mmoja yeye kukaa baa mpaka saa nane ni kawaida, ila hutakaa usikie ana mgogoro na mke wake, na kama upo ana umalizia ndani Kwa ndani. Na pia hutakaa usikie watoto wake wamerudishwa ada shule, huyu naye namuweka kwenye kundi la mabaharia.

Baharia mshipa wa uoga au aibu umeshakatwaga na kutupwa uko India, yaani yeye kutongoza mwanamke ni jambo ambalo hajali kukataliwa na huwez mkuta ana lalamika Kwa watu, hata kama ni mbele ya kadamnasi ata msimamisha mwanamke na kumuomba namba na tecno yake ya batani.

Na kuna jamaa yeye ni kuuza mali za uwizi na mirungi, lakin yule jamaa hapajui mahakaman pamefananaje kesi zake zote anazimalizia polisi, huyu naye ni baharia.
 
Kwenye MV Magogoni hivyo vyeo vipo
Kwenye kivuko kunakuwa na Nahodha, Engineer, Oiler na Baharia.

Engineer anakuwa engine room na Oiler au wanatembea na kivuko wakati wote wa zamu yao.

Baharia anakuwa kwenye mlango kazi yake ni kupanga magari,kuangalia usalama wa wanaoingia na kuweka au kutoa Kishikio (Hook) kwenye mlango wa kivuko(Ramp).
 
Na ni kweli kwamba meli ikizama lazima nahodha azame nayo? Na ikitokea amepona ni kweli anatakiwa anyongwe?
Nahodha ndio kila kitu kwenye meli (Chief in Charge) na yeye ndio amekabidhiwa meli. Ni kweli lolote litakalotokea hata kama amefanya mtu mwingine anayehusika kujibu ni nahodha.

Ishu ya kuzama na meli ni chaguo la mtu, kuonekana alifanya uzembe,kuogopa hukumu nzito ya mahakama na kuonekana amedharirisha taaluma yake kubwa aliyokuwa nayo.

Ila hii ya kuzama na meli wazungu ndio walifanya zamani, ila kwa mswahili thubutu anatoroka kusikojulikana au bora aende mahakamani.
 
Nahodha ndio kila kitu kwenye meli (Chief in Charge) na yeye ndio amekabidhiwa meli. Ni kweli lolote litakalotokea hata kama amefanya mtu mwingine anayehusika kujibu ni nahodha.
Ishu ya kuzama na meli ni chaguo la mtu, kuonekana alifanya uzembe,kuogopa hukumu nzito ya mahakama na kuonekana amedharirisha taaluma yake kubwa aliyokuwa nayo.
Ila hii ya kuzama na meli wazungu ndio walifanya zamani, ila kwa mswahili thubutu anatoroka kusikojulikana au bora aende mahakamani.
hahahaaaa shukrani uliposema thubutu anatoroka nikamkumbuka nahodha wa mv spice islanders alivyotoka nduki kali
 
Hivi kumbe huwa hakuna kitengo cha maalumu kwa wale divers wanaenda kutoaga nanga ikizngua n.k
 
Hivi kumbe huwa hakuna kitengo cha maalumu kwa wale divers wanaenda kutoaga nanga ikizngua n.k

Divers wanaajiriwa kulingana na uhitaji wa chombo.
Meli nyingi za abiria huwa wanatembea na Divers kujihami na tahadhari ya mtu kuingia majini( Man overboard).

Kwa meli kubwa Diver hana ubavu wa kutoa nanga ikizingua. Nanga inaweza kuwa na uzito hata wa tani 5 huyo Diver hawezi kufanya lolote.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom