kipara kipya
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 20,142
- 24,447
Lema anasahau maisha yanakwenda kasi!
Sio chadema ndo wamejenga dhanaRais ameshajenga dhana kuwa CHADEMA ni maadui zake, hii itampa shida sana
Kwa sasa inavyoonekana Meya wa Jiji la Arusha kwa tiketi ya CHADEMA, Calist Lazaro yuko karibu sana kiutendaji na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ukilinganisha na Godbless Lema.
Kauli iliyotolewa na Rais Magufuli kuhusu Meya wa Jiji la Arusha inatoa picha hasi katika mahusiano ya kikazi kati yake na Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema.
Wakati akiongea na wananchi wa viunga vya Mkoa wa Arusha, Rais Magufuli amesikika akisema anampongeza sana Meya wa Jiji la Arusha kwa sababu ni mpenda maendeleo bila kujali utofauti wa itikadi za kisiasa.
Meya Calist Lazaro amekuwa na Rais Magufuli kwenye msafara katika ziara yake mkoani Arusha.
Rais alienda mbali zaidi na kusema alipokea ujumbe kutoka kwa Meya Calist Lazaro ukimuomba amtembelee lakini Rais akamjibu na kumwambia akifanya hivyo atafukuzwa CHADEMA.
Hii inaonyesha baadhi ya watu au wanasiasa wa CHADEMA mkoa wa Arusha wameanza kukaa kando ya siasa za Lema ambazo wanadhani hazina manufaa kwao au wananchi wengi. Wameanza kukubaliana na msemo wa Waingereza unaosema, "If you can't beat them, join them'.
Siasa za Lema ni kutoshirikiana na uongozi wa mkoa na pia Rais Magufuli.
Hii sio hali nzuri kisiasa kwa Lema kwa sababu nguvu zake za kisiasa katika Mkoa wa Arusha zinapunguzwa kadri siku zinavyokwenda.
Kwa sasa ameanza kupata wapinzani ndani ya CHADEMA mkoani Arusha ambao inaonekana watapambana naye kwenye nafasi ya uongozi na ubunge.
Lema hajatambua kuwa mazingira ya siasa katika mkoa wa Arusha yamebadilika na kwa mantiki hiyo kuendelea kufanya siasa zilezile kwa kutumia mbinu zilezile za mwaka 2010 ni kujichimbia kaburi la kisiasa.
Inaonekana wajanja wameanza kumkimbia!
Video kuhusu alichokiongea Rais Magufuli kwa Meya wa Jiji la Arusha.
Hebu tueleze sisi wa Nanjilinji hatujuiWewe na huyo rais wako hamjaelewa kitu kuhusu Arusha
CHADEMA baada ya uchaguzi walijua wamempata rais wa JMT kumbe ni rais wa wakiompigia kura tu. maeneo yenye wana CHADEMA wengi ndiyo yalipitiwa na bomoa bomoa huku rais kwa kauli yake alisema Mwanza wasibomolewe kwani wamempigia kura.Sio chadema ndo wamejenga dhana
Ni bora kujitia kitanzi kuliko kuunga mkono siasa za kijinga za awamu hii upande wa CCM. Na kusema ukweli, si ule 'ukweli wako na yule mwenzako', CCM inaliangamiza sana taifa hili!Huwezi kufanya manunuzi kama hakuna bidhaa!
Siasa zinabadilika ndio maana nimesema kuendelea kufanya siasa zilezile kwa kutumia mbinu zilezile ni kujitia kitanzi.
Muongeze Dozi huyooo msemajiuwongoPale ' MsemajiUkweli ' anapokuwa ' MsemajiUwongo ' naomba niishie hapa tafadhali.
Kamuulize Polepole mkiwa kwenye vikao vyenu atakufafanuliaHebu tueleze sisi wa Nanjilinji hatujui
HahahahahahaKamuulize Polepole mkiwa kwenye vikao vyenu atakufafanulia
Mnyooshaji anaponyooka mwenyewe ndio maana kila kukicha vichomi kuzindua sebule 31 kwa mkuu wa nchi ni aibu sanaHahahahahaha
Mtanyooka tuuu
Lakini chadema ndo walioanzisha pingapinga ili wapate umaarufu wa kisiasa baada ya kushauri kwa utaratibuCHADEMA baada ya uchaguzi wakijua wamempata rais wa JMT kumbe ni rais wa wakiompigia kura tu. maeneo yenye wana CHADEMA wengi ndiyo yalipapitiwa na bomoa bomoa huku rais kwa kauli yake alisema Mwanza wasibomolewe kwani wamempigia kura.
Hawa na huyo mkubwa wao wote ni masho--!! Eti "Tangu jana ananiandikia meseji niende kwake!!" hiyo statement ya kipunga kabisa!! Yaani mnamfanya mayor ni punguani amwandikie rais meseji ya kumwita nyumbani kwake? Mwambieni huyo msuKuma aache kuchufulia watu heshima zao! Last time kwenye ziara ya magufuli mlimnyima Lema nafasi ya kuzungumza/kusalimia! Mkampiga na majungu akiwa hapo hapo uwanjani!! Sasa hata ingekuwa ni wewe ungeendelea kuungana na mashetwani ya namna hiyoMuongeze Dozi huyooo msemajiuwongo
Ova
yangekuwa yanazungumzwa yoote wanayofanya nadhani ni vigumu kushirikiana na hao wanaojiita wapenda maendeleoTatizo linaanzia hapa kwamba mtu kushiriki tu amehasi chama chake hapo mnatoa taswira gani kwa viongozi