Meya wa Jiji la Arusha amemchoka Godbless Lema?

Meya wa Jiji la Arusha amemchoka Godbless Lema?

Kwa sasa inavyoonekana Meya wa Jiji la Arusha kwa tiketi ya CHADEMA, Calist Lazaro yuko karibu sana kiutendaji na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ukilinganisha na Godbless Lema.

Kauli iliyotolewa na Rais Magufuli kuhusu Meya wa Jiji la Arusha inatoa picha hasi katika mahusiano ya kikazi kati yake na Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema.

Wakati akiongea na wananchi wa viunga vya Mkoa wa Arusha, Rais Magufuli amesikika akisema anampongeza sana Meya wa Jiji la Arusha kwa sababu ni mpenda maendeleo bila kujali utofauti wa itikadi za kisiasa.

Meya Calist Lazaro amekuwa na Rais Magufuli kwenye msafara katika ziara yake mkoani Arusha.

Rais alienda mbali zaidi na kusema alipokea ujumbe kutoka kwa Meya Calist Lazaro ukimuomba amtembelee lakini Rais akamjibu na kumwambia akifanya hivyo atafukuzwa CHADEMA.

Hii inaonyesha baadhi ya watu au wanasiasa wa CHADEMA mkoa wa Arusha wameanza kukaa kando ya siasa za Lema ambazo wanadhani hazina manufaa kwao au wananchi wengi. Wameanza kukubaliana na msemo wa Waingereza unaosema, "If you can't beat them, join them'.

Siasa za Lema ni kutoshirikiana na uongozi wa mkoa na pia Rais Magufuli.

Hii sio hali nzuri kisiasa kwa Lema kwa sababu nguvu zake za kisiasa katika Mkoa wa Arusha zinapunguzwa kadri siku zinavyokwenda.

Kwa sasa ameanza kupata wapinzani ndani ya CHADEMA mkoani Arusha ambao inaonekana watapambana naye kwenye nafasi ya uongozi na ubunge.

Lema hajatambua kuwa mazingira ya siasa katika mkoa wa Arusha yamebadilika na kwa mantiki hiyo kuendelea kufanya siasa zilezile kwa kutumia mbinu zilezile za mwaka 2010 ni kujichimbia kaburi la kisiasa.

Inaonekana wajanja wameanza kumkimbia!

Video kuhusu alichokiongea Rais Magufuli kwa Meya wa Jiji la Arusha.

Hanunuliki huyo mtasumbuka bure..
Meya oyee[emoji89] [emoji87]
 
Kwa mujibu wa maneno yako ni kwamba wamefanya makosa ambayo wanastahili kuuliwa kwa mapanga na kushambuliwa kwa silaha za kivita?
Sasa hapo Ni kwa mujibu wako mi sijasema


Ila muwakumbushe kusoma alama za nyakati
 
Kama amemchoka, mwambie akuoe wewe.
 
Rais ameshajenga dhana kuwa CHADEMA ni maadui zake, hii itampa shida sana
WaTanzania wengi ni kama mna shida sana kichwani.ukitazama kwa umakini unagundua kua chadema ndiyo imejenga dhana ya uadui na CCM.kila siku ni mabaya tu kwao.sasa jana Lema ni kama kasusia ugeni wa Rais.anatetea wananchi gani sasa hapo mjini,aliyekuja ndiyo Rais na ikiwezekana angeonekana na kutoa kero zake pale mbele ya mkuu na angejibiwa.ukitazama unaona roho mbaya wanazo chadema za uchu na wivu wa madaraka.uadui uko kwao na si kwa Rais na chama chake

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Lema ameachia fursa adhimu ya kuonana na Rais wke kumpa kero za wana Arusha.
Ni vigumu sana kwa Lema kurudi,chadema inaweza kurudi Arusha lakini sio lema
 
lema sasa hivi hana chakuongea zaidi ccm imemzdi ujanja hapa mjn,anafkria ni zama za ni heshima kubwa kwa mungu kumzomea mwizi fisadi kama lowasa, sasa hivi hana akiba ya maneno kila siku anahubiri demokrasia na kuonekana kwenye camera akizika mbwa wa nasar,arusha haturudii makosa tena
 
Ataisoma namba 2020,si kila jambo ni kutumia nguvu tu
 
Hizo siasa tu,jpm aliwahi kumcifia mbowe pale hai lkn kiualisia kla MTU unajua hawa watu walvyo....aliwahi kumcifia zito pale bungeni wkt ukawa wana toka nje,je zito yuko upande wa Lumumba...kwa hyo ucje shangaa mayor anashawishi watu wagome kwenda kufyeka bangi kwani hlo c jukumu lao....
 
Back
Top Bottom