MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,185
- 24,055
Kwa sasa inavyoonekana Meya wa Jiji la Arusha kwa tiketi ya CHADEMA, Calist Lazaro yuko karibu sana kiutendaji na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ukilinganisha na Godbless Lema.
Kauli iliyotolewa na Rais Magufuli kuhusu Meya wa Jiji la Arusha inatoa picha hasi katika mahusiano ya kikazi kati yake na Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema.
Wakati akiongea na wananchi wa viunga vya Mkoa wa Arusha, Rais Magufuli amesikika akisema anampongeza sana Meya wa Jiji la Arusha kwa sababu ni mpenda maendeleo bila kujali utofauti wa itikadi za kisiasa.
Meya Calist Lazaro amekuwa na Rais Magufuli kwenye msafara katika ziara yake mkoani Arusha.
Rais alienda mbali zaidi na kusema alipokea ujumbe kutoka kwa Meya Calist Lazaro ukimuomba amtembelee lakini Rais akamjibu na kumwambia akifanya hivyo atafukuzwa CHADEMA.
Hii inaonyesha baadhi ya watu au wanasiasa wa CHADEMA mkoa wa Arusha wameanza kukaa kando ya siasa za Lema ambazo wanadhani hazina manufaa kwao au wananchi wengi. Wameanza kukubaliana na msemo wa Waingereza unaosema, "If you can't beat them, join them'.
Siasa za Lema ni kutoshirikiana na uongozi wa mkoa na pia Rais Magufuli.
Hii sio hali nzuri kisiasa kwa Lema kwa sababu nguvu zake za kisiasa katika Mkoa wa Arusha zinapunguzwa kadri siku zinavyokwenda.
Kwa sasa ameanza kupata wapinzani ndani ya CHADEMA mkoani Arusha ambao inaonekana watapambana naye kwenye nafasi ya uongozi na ubunge.
Lema hajatambua kuwa mazingira ya siasa katika mkoa wa Arusha yamebadilika na kwa mantiki hiyo kuendelea kufanya siasa zilezile kwa kutumia mbinu zilezile za mwaka 2010 ni kujichimbia kaburi la kisiasa.
Inaonekana wajanja wameanza kumkimbia!
Video kuhusu alichokiongea Rais Magufuli kwa Meya wa Jiji la Arusha.