Meya na RC Dar-es-salaam: Huu ni uzembe uliopindukia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Meya na RC Dar-es-salaam: Huu ni uzembe uliopindukia!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Steve Dii, Jul 13, 2009.

 1. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mmeshindwa nini kuhakikisha watu wanapanga foleni (mistari) kwenye vituo vya mabasi?!

  Hamna kitu kinachotia aibu na kunikera kuona watu wanaojiita watu wa mijini wakigombania kupanda mabasi. Yaani ni fujo tupu, ustaarab umepotea kabisa. Jamani hata ng'ombe wanaokwenda kunywa maji hujipanga mstari na kusubiria zamu zao!! Pale wanapoonekana kutokuwa na ustaarabu (kama kwenda kuogeshwa kwenye majosho), hujengewa uzio kuwaongoza.

  Mmeshindwa nini ninyi kama wahusika wakuu kwenye miendenendo ya wakazi wa jiji hili?! Jamani hili nalo mpaka tupate msaada kutoka kwa wahisani na kwenda kwenye warsha?!

  Tafadhali sana, wekeni sheria katika level ya halmashauri kushughulikia hili suala, kweni liko chini yenu. Sheria ziendane na elimu kwa wakazi. Na kwenye vituo vyenye msongamano mkubwa, wekeni uzio wasafiri wajipange kabla ya kupanda mabasi.
   
 2. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu naungana na wewe kuonesha kero ya daladala jijini dsm, lakini sikubaliani na wewe kuwalaumu Meya na RC kwa vile hayo unayoyasema yako nje ya uwezo wao hasa ki-miundombinu.

  We angalia vituo vyenyewe vilivyo na nafasi finyu mfano posta.....sasa huo uzio ndio ujemngwe vipi mkuu? Ok achana na posta nenda buguruni-rozana, nenda vingunguti nk unategemea hiyo miuzio utajengwa vipi?

  Hapa kitu cha msingi ni kupata ufumbuzi wa usafiri wenye tija, ambao utahakikisha idadi ya watu haiwi nyingi kwenye vituo hasa nyakati za asubuhi na jioni. Ukiweka utaratibu huo....i mean vyombo vya kusafiria na miundombinu yake mambo yatakuwa shwari.... suala ni kuwa lini serikali itaipa umuhimu jambo hilo!

  Mkuu pia nashukuru umenikumbusha purukushani katika foleni ya uji nilipokuwa Ilboru enzi hizo. Mstari unakuwa unaenda safi na viranja wako pembeni kudhibiti hili na lile....ghafla ikigundulika uji unakaribia kwisha na watu bado lukuki....mara moja foleni inavurugika...hakuna cha ustaarabu wala nini.....usubiri ustaarabu gani halafu ukose uji??
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kama hajali kuweka UZIO kwenye shimo la barabarani hadi watu wanaziba kwa kuweka TV ya kizamani, unafikiri hili atajali?

  Masatu anasema "...Kama mnawivu kwa Meya, si mjinyonge tu?"

  Masatu hiyo ilikuwa salamu.....
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Wajaribu kubadili aina ya usafiri, hivyo vipanya kwa namna moja vinachangia abiria kutopanga foleni.
   
 5. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  katika mambo yanayokera na kuonyesha uozoo wa kiuongozi Tanzania ni uendeshaji na usimamizi wa jiji la DSM...haiwezekani mlolongoo wote wa viongozi dar wafikirie kwa namna moja tuuuuu na wananchi tunawaangaliaa tuuu kwa kukubali kero za jiji (usafiri, maji, barabara, afya, elimu) kuwa sehemu ya maisha yetuuuu....

  uwezo mdogo na unafiki uliokithiriii wa viongozii (wa kuteuliwa na kuchaguliwaa) ndo uliotukifikishaa hapa tulipoo..

  haiwezekani tume ya jiji iliyokuwepo kwa kipindi kifupi wakafanya mambo mazuri amabayo waliopo na waliokuwepo miaka yote hawajawahi kufikiria hata kufanya..tuna haja gani dsm kuendelea kuwa na aina ya uongozi uliopooo???

  kwa nn tume ya kuendesha jiji isiwepo na ikapewa mamlaka na muda wa kufanya kazi kwa kushughulikia vipaumbele kama usafiri, maji, usafi,barabara kwa kuanziaaaa???

  shame on us dar residents kwa kukubaliii hali hiiii...
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ukweli ni kwamba hawa viongozi wa Jiji la Dar Es Salaam hawana jipya, its time wakuu wa Mikoa wawe wanachaguliwa kwa uchaguzi, akishindwa kazi wanachi wanampiga chini.

  Hii mijitu kazi yao kukaa ofisini kupiga porojo kwenye vikao na kujikweza kwenye viombo vya habari haina lolote ifanyalo. pka JMK awaambie fanyeni hivi ndio inafanya, tazama mataka yalivyojaa Kariakoo, Tazama migari ya taka inavyopita mchana Kariakoo na kufanya foleni zisizo na mpango, kwani haioni? inaona sana lakini ndio upeo wao ulipofikia hawana jipya.

  Sisi tutapiga kelele lakini ukiisikia invyoongea, porojo tupu! hamna action hata moja.
   
 7. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  That was a very good observation mkuu. Especially ulivyo tolea mfano wa ng'ombe.
   
 8. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hili nimeliongelea hapa mwezi uliopita,aliyewahi kupita Nairobi tu wala sio mbali atakuwa ameona watu wanavyoingia kistaarabu ndani ya mabasi hadi raha.Wajawazito,wazee na watoto hawapati taabu.Vitu vingine havihitaji msukumo wa serikali sisi wenyewe tubadilike.
   
  Last edited by a moderator: Jul 13, 2009
 9. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mkuu Lagatege, unajua karibia kila mji hapa duniani unamatatizo yake... lakini utakubaliana nami kuwa kuna aina nyingine ya matatizo usipoweza kutatua moja kwa moja tafsiri yake ni ujinga na ushenzi. Kutopanga mstari sehemu zenye migao na huduma kwenye jamii ni jambo lisilo la kistaarab hata kidogo, ni ujinga na ni ushenzi. Bahati mbaya Taifa letu limebarikiwa kuwa na viongozi weeeengi wa kusimamia na kupunguza ujinga na ushenzi lakini hawatizimi majukumu ya wajibu wao. Hii ni laana kwa kweli, kwanini watu tusiwe na ustaarabu na kuthaminiana kwenye huduma walau kwa kupanga mistari?!
   
 10. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Dar Es Salaam, je unafikiri uchaguzi utasaidia kweli iwapo baadhi ya wengine wengi tuliowachagua kutusaidia hawaonekani kabisa kujali nguvu za kura Bungeni? Uwe uchaguzi wa kila miaka miwili sijui...
   
 11. Kilinzibar

  Kilinzibar Senior Member

  #11
  Jul 16, 2009
  Joined: Mar 6, 2008
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jiji chafu usipime yani kama vile hakuna kiongozi katika hili jiji inasikitisha sana.
   
 12. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hakika hili linaweza kusaidia, tena kwa kiwango kikubwa tu. Nakumbuka minamo ya mid 80s hadi early 90s UDA zilikuwa na timetable tena iliyokuwa inafatwa kwa kiwango kikubwa.

  Kuwepo kwa timetable za mabasi kunafanya watu wasirundikane kwenye vituo hivyo kwenda kwenye vituo katika muda wanaojua basi lao litapita.

  Swala jingine, labda wenye biashara za vipanya walazimishwe kuunganisha biashara zao na kuunda kampuni ambazo zitatumia ticket aina moja na kuwa na mabasi makubwa ili kupunguza utitiri wa vigari vidogovidogo vinavyoleta kero na msongamano wa magari barabarani. Kuwepo na tiketi za aina moja, za siku nzima, wiki na mwenzi kunaweza kurahisisha watu kuwa wanapanda mabasi kwa uharaka milangoni hivyo kupunguza msongamano wa wasafiri kwenye vituo.

  Dar Rapid Transport naona bado imebakia kuwa ndoto. Inazidi kupigwa tarehe mwaka baada ya mwaka. Nadhani wakati umefika na kukubali kuwa ni bora turudie usafiri wa maUDa. Kutokuwepo kwa usafiri mbadala katika mji unaojiita jiji kuu la Tanzania ni aibu kubwa machoni pa mataifa mengine. Transport system ni moja ya basis za maendeleo. Ustaarab kwenye vituo vya mabasi ni moja ya mambo yanayotutambulisha sisi kama Taifa lenye binadamu na siyo mifugo pekee.
   
 13. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kwetu, ni kweli swala la miundombinu ni la Kitaifa. Lakini ukweli wa mambo ni dhahiri kwamba kuna baadhi ya mambo hayahitaji directives kutoka wizarani kuweza kufanyika. Ni mambo ambayo yako mikononi mwa halmashauri za miji na vijiji. Meya na RC kazi zao ni nini hapa mjini, kuhudhuria sherehe za harusi tu na matamasha ya miziki?!! Maana huko ndiyo huwa hawakosekani... Mkuu wangu, pamoja na matatizo yote yaliyopo kiwizara na kitaifa, hawa wakuu hawaoneshi mfano wowote wa dhati katika kukabiliana na maswahib yawakumbayo wakazi wa dar.
   
 14. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Hapo umefafanua vizuri namna ya kumaliza tatizo la abiria kugombania daladala. Zaidi ni kwa Meya wa Jiji kuona atafanya nini katika kuondoa tatizo hili.

  Kwa upande mwingine, wazo la mwenye daladala(vipanya) kuungana na kuanzisha utaratibu ulioutaja ni muhimu. Hii itawafanya wasijaribu kutafuta mbinu za kuzuia kuingia kwa mabasi makubwa.

  Kurudishwa kwa UDA, ni njia mojawapo ya kuondokana na kadhia hii, aidha umiliki wa UDA uwe moja kwa moja chini ya Halmashauri ya Jiji, na wenye daladala waruhusiwe kununua hisa huko.
   
 15. e

  eddy JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2009
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,400
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  SteveD, hili suala halihitaji mkopo wa WB! mfano huku mza kuna vikundi vya usafi vya mtaa hupita namakwama kila siku kukusanya uchafu mitaani mwisho wamwezi unaletewa bili ya elfu tano tu.

  Majengo makubwa kama ya ppf bot na nssf kunamakampuni ya usafi ukipita kwenye korido nyuma mtu anakufuata nadekio lenye detto kitakatisha kila unapokanyaga.

  Ningeshauri pia Mgambo wa jiji wapanue majukumu yao kidogo badala ya kudeal na wamachinga sasa waanze kuwakamata watu wanaokata magogo na kuchimba dawa hovyo, ile kampuni iliyopewa kazi ya kuondoa wapiga debe nadhani lipewe msaada, kazi hii ya kusaidia watu vituo vya mabasi ingefanywa kwa utaalamu tatizo la kupigana vikumbo lingepungua kwa kiasi fulani.

  Hili la vipanya nadhani tufungue kesi ya kikatiba tu dhidi ya serikali, kimsingi hivi vipanya ni ambulance za kubeba mgonjwa mmoja na paramedic wawili iweje zipewe leseni zibebe pax 22? tatizo nikubwa zaidi kwa wenye makalio makubwa.

  Naimani makampuni kama abood, mohamed trans, kugis, Inter-city Goldern coach,Quality group, Alpha group wangeweza kupewa tenda ya DART na kuifanya kwa ufanisi mkubwa.
   
 16. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Eddy unakumbuka stendi ya mabasi ya enzi zile na hata hii mpya hapo Mwanza? Tanganyika Bus tulikuwa tunapanga msitari, vituo vilikuwa vimejengwa kuwafanya wasafiri automatically wajipange mistari, sijui siku za karibuni. Hii yote ni (ilikuwa) bidii ya manispaa. RC na Meya wa Dar ni wazembe, period!
   
 17. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Miaka miwili nyuma ilikuwa hivi:
  [​IMG]

  [​IMG]
  Pichani vijana wakijitolea kusafisha kituo cha mabasi Mwanza
   
 18. e

  eddy JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2009
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,400
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  StiveD, weacha tu, vipanya vyote vimerundikwa mtaa wa rwagasore kunamsongamano hakuna mfano, wapiga debe wanakata magogo na kuchimba dawa nyuma ya vipanya huku mgambo wa jiji wakitizama tu. wapiga debe wanawapora abiria mchana kweupe! achilia matusi ya nguoni ya makonda! yaani nikama jehanamu fulani, nashukuru jk kutuondolea msekela namwomba kandoro asione kuja mwanza ni dimosheni achape tu kazi.

  Stendi unayosema baada ya kutiwa lami kwa fedha nyingi umekuwa uwanja wa kuonyeshana ufahari kwa matajiri wa mwanza, zuberi akipaki range rover yake, gupta anapaki hammer, manjit Lexas V8, mansoor VX V8, Tarimo Lexas harrier, akinamama nao hawako nyuma utaona kila aina ya vi-RAV4! achilia mbali Benz L320 za akina mama Ntale.

  kapuku ukipaki kacorolla utakiona cha mtema kuni, mgambo wa jiji watakuja na minyororo na faini ya elfu hamsini, achilia bili ya break down!
   
 19. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  SteveD,
  Hoja yako ina mantiki sana. Kupanga mstari wakati wa kupanda bus hata wazee, wagonjwa, walemavu na wasiojiweza wataweza kutendewa haki iwapo kutakuwa na utaratibu mzuri wa kupanda bus. Asante kwa kumbusha enzi za UDA. Yale ma-'Ikarus Kumbakumba' huu ndio ulikuwa wakati wake mwafaka kabisaa. Yakipita mawili matatu kituoni yanaondoa umati mzima. Lakini basi uwepo mwamko uliokuwepo enzi hizo wa kuweza kuwapisha viti watu wazima, wanawake wajawazito, na walemavu. Nakumbuka miaka ya 60 na 70 mwanamke akiingia kwenye bus kama hujapata kiti mwanaume bila kuombwa anasimama kumpisha kiti mwanamke - huo ulikuwa ustaarabu babu kubwa. Leo hii hata mjamzito hapishwi!! Aibu.

  Yote haya yanatokana na uongozi mbovu wa walioshika/kukalia viti wanawaza starehe na matumbo yao na watoto wao na ilimradi wao na watoto wao wanapanda magari yenye viyoyozi they don't care a hoot!
   
 20. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #20
  Jul 16, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Inasikitisha....!!:(
   
Loading...