Meya na RC Dar-es-salaam: Huu ni uzembe uliopindukia!

SteveD,
Hoja yako ina mantiki sana. Kupanga mstari wakati wa kupanda bus hata wazee, wagonjwa, walemavu na wasiojiweza wataweza kutendewa haki iwapo kutakuwa na utaratibu mzuri wa kupanda bus. Asante kwa kumbusha enzi za UDA. Yale ma-'Ikarus Kumbakumba' huu ndio ulikuwa wakati wake mwafaka kabisaa. Yakipita mawili matatu kituoni yanaondoa umati mzima. Lakini basi uwepo mwamko uliokuwepo enzi hizo wa kuweza kuwapisha viti watu wazima, wanawake wajawazito, na walemavu. Nakumbuka miaka ya 60 na 70 mwanamke akiingia kwenye bus kama hujapata kiti mwanaume bila kuombwa anasimama kumpisha kiti mwanamke - huo ulikuwa ustaarabu babu kubwa. Leo hii hata mjamzito hapishwi!! Aibu.

Yote haya yanatokana na uongozi mbovu wa walioshika/kukalia viti wanawaza starehe na matumbo yao na watoto wao na ilimradi wao na watoto wao wanapanda magari yenye viyoyozi they don't care a hoot!

Wazee, wagonjwa na na wengine wasiojiweza wananyanyasika sana. Kwa kweli bila magari makubwa yenye hadhi na uwezo wa kupakia abiria wengi na wale wasiojiweza, nchi yetu inajitengenezea wingu zito la kimaadili lisiloweza kurekebishika kwa takribani kizazi kizima. Tabia zinapojengeka tabia hizo kubadilika ni vigumu na huchukua muda.

Kama alivyosema Kibunango, watu wenye vipanya wanaweza wakawekewa mipango ya kununua hisa kwenye kampuni kubwa, sema - tatu au nne hivi zinazoweza kuanzishwa kwa ajili ya usafiri mijini. Mbona Saccos zimewezekana badala ya kila mmoja kuanzisha mfuko wake mwenyewe?! Shirika la UDA lilitufaa sana. Kwenye mabasi kulikuwepo na hewa safi na nafasi za watu kusimama, hata wenye mizigo walikuwa wanaweza kupanda nayo bila matatizo. Leo hii hata begi lako kwenda safari ya karibu tu katika kuunganisha safari ni kero. Mtu inabidi ukodishe teksi.

Ongezeko la vipanya na watu kuvichukia kutokana na kero zake ndiko huko in return kunafanya kuwe na haja ya kila mmoja ajitahidi kununua gari yake. Ambapo hilo nalo linaleta ongezeko la magari na msongamano wa magari usiokuwa na suluhisho maana miundombinu tuliyonayo haikidhi mahitaji. Na panapokuwa na misongamano ya magari, ina maana watu wanachelewa makazini, muda mwingi unatumiwa mabarabarani badala ya kuwa katika uzalishaji, uchafuzi wa mazingira kutokana na moshi wa magari, ongezeko la mahitaji ya mafuta unnecessarily kwenye supply zetu, lakini pia ni ongezeko la kero na chanzo cha hisia chafu (rages and frustrations) miongoni mwa wanajamii, ambapo jambo dogo tu linaweza kusababisha a big revolt dhidi ya watu na serikali.

Jamii nzima inajikuta imeingia kwenye a cycle of poverty kutokana na baadhi ya wachache tu, hususan viongozi kutowajibika katika majukumu yao.

This country deserves better!
 
Jamii nzima inajikuta imeingia kwenye a cycle of poverty kutokana na baadhi ya wachache tu, hususan viongozi kutowajibika katika majukumu yao.

This country deserves better!

Yeah man! This country deserves better! And you are very right, tumeingia kwenye cycle ya poverty kutokana na viongozi na watu wachache walio kwenye key positions kutowajibika ipasavyo. Mfano mzuri ni budget zetu ambazo hutayarishwa na maafisa wa wizara na kuidhinishwa na Makatibu Wakuu na hatimaye kupitishwa kwenye Baraza la Mawaziri mbele ya Rais na Waziri Mkuu wa nchi. Budget zenye kasma za ununuzi wa magari ya bei mbaya sana kila mwaka kwa ajili usafiri wa hao 'cream' bila kujali wananchi wanaoteseka kwa public transport duni mijini, mikoani hadi vijijini.

Namkumbuka sana yule Mzee Nyerere RIP aliyejaa busara za ajabu aliyekuwa akihubiri kwamba Maendeleo lazima yalenge watu na si vitu - PEOPLE-CENTRED DEVELOPMENT. Tuliletewa ma'Ikarus kumbakumba' kwa sababu viongozi walijali WATU waliokuwa wakiwaongoza. Lakini sasa hivi kujenga barabara nyingi za lami na kujenga majengo ya vioo ndio MAENDELEO! Hebu fikiria hata zijengwe barabara zote jijini Dar es Salaam kwa kiwango cha lami, kuna raha gani ama maendeleo gani kwa mwananchi wa kawaida?

Kwa mtazamo wa viongozi, MAENDELEO ni barabara za lami na majengo ya vioo yanayofanya jiji la Dar lionekane kama New York. Wala hakuna anayeumia wala kuguswa na shida wanazopata wananchi. Ilimradi wao na familia zao wanaishi kwa raha mustarehe, nothing matters! And then wanajiita ni wawakilishi wa wananchi!! It is a shame.
 
Kwa mie Lawama Haziishi tu kwa mameya na RC....bali hata kwa Polisi...Think tank yetu bado ipo ndogo sana...Watakaa Wasubiri waambie na RAIS fanyeni hivi au vile...!!!

Hili zoezi Lahitaji kusimamiwa na Polisi....ikiwezekana hata FFU..wasisubiri wakae tu Kambini hadi waitwe...Watu wamekuwa wavivu hata Kufikiria....Watadai eti watanzania Ndio tulivyo....!! Wakati wanashindwa kuweka taratibu na Kuzisimamia!!!

Nafikiri Ndani ya Mwezi 1 tu wakiamua kuweka taratibu za Foleni.."First IN First One to be served" itakuwa vema sana. Hatutakuwa na Vurugu. Pia zitaweka na sheria kuwa Family or Wanawake Kwanza....Hii itapunguza kina Dada kuchelewa kurudi Majumbani..Watawahi kuwalea watoto nk.
 
Sasa naona RC amezinduka...let me hope tutaona mabadiliko hivi mapema.
 
SteveD,
Mkuu wangu kama sikosei mwaka 2001, nilisema makosa makubwa yamefanyika kuruhusu daladala na kuliua shirika la UDA..watu walisema mimi mjamaa na wakasema Daladala hazina taabu kabisa yaani usafiri bomba sio kama wakati wa UDA..
Trust m,e leo hii Dar hali iliyofikia kwa daladala ni sawa na adha tuliyokuwa nayo wakati mbaya wa UDA ilipofika 1985 baada ya kuingia Ubepari..
UDA ni moja ya mashirika tuliyoyaua sisi wenyewe.. mashirka kama NBC, TRC, ATC, Posta na Simu, huduma muhimu za kijamii kama Afya na Elimu.. vyote hivi tuliyaua hata bila aibu kwa Ubepari ulipotujazia mali madukani.. Kuna mshikaji wangu mmoja Mcuba alinambia - U guys sold Ur independence for toothpaste! inachekesha lakini ukifikiria sana ndio ukweli huo leo hii mali feki zimejaa madukani nasikia kuna hata dawa za homa (Panadol) wanapima madukani kwa mzani, kidonge Tsh 10.. ati open economy!
Hakika hunipa wasiwasi sana kama kweli Tanzania ina viongozi wazuri au wananchi wana nia njema na nchi yao..
Hivyo usimlalamikie Maya wala nani ni sisi wenyewe tuliochagua kufika hapa.. Kwa ubishi wetu tulifikiria Ubapari ni raha tupu
 
kaka kero tunayopata sisi tunaotoka posta jioni huwa naifikiria sana. kutokana na usumbufu huu, inanilazimu hata nilale usingizi wa mang'amu ng'amu kwa ajili ya kufikiria foleni. Hunilazimu kila siku kuamka saa 10:30 alfajiri na jiandaa kwenda kwenye shughuli zangu, kwa asubuhi namudu, lakini wakati wa kurudi hapo ndo kimbembe, bila ubavu hupandi gari> yaani ni kero mpaka huwa natamani niamie hata huko mikoani kusiko na vurugu hizo. Inakera sana jamani
 
Watu wanaweza vipi kupamga foleni,hebu nieleze,wakati mabasi ni kidogo. Mabasi yanapita yamejaa. Halafu moja linasimama. Watu wataweza kweli kupanda kistaarabu?
 
Back
Top Bottom