Mshindo
JF-Expert Member
- Mar 5, 2009
- 478
- 186
Jerry Silaa ni mfano mzuri wa kiburi (arrogance) ambayo aghalabu huwanyemelea binadamu waliopata ngekewa ya mafanikio kidogo. Ironically hawa binadamu wanaopata "mafanikio" ya haraka haraka kwa njia za mashaka ndio wanaoonesha zaidi kiburi cha namna hiyo. Mifano ipo mingi. Unakutana na kijana amehonga-honga all his/her way up, akishafika sasa, simply kwasababu anaweza kusimama mbele za watu wakamsikiliza basi nasaha zake zitakua: "....vijana wasikae tu kulia lia oh serikali hili serikali lile...watu wajitume, wafanye kazi kwa bidii watafanikiwa tu...kama mimi!!" ukweli wa mambo wa "kujituma" kwake "anausahau" kidogo. Kwa sie wengine tunaojua ukweli wa harakati za watu kama hao tunapata shida kweli...
Last edited by a moderator: