Kwa faida ya watoto waliozaliwa miaka ya themanini na tisini na kuendelea: Nyerere alijenga uchumi wenye nguvu sana chini ya ujamaa na Kujitegemea!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,663
18,036
Vijana wengi waliozaliwa miaka ya themanini na kuendelea huwa wanakejeli sana siasa ya mwalimu Nyerere ya ujamaa na kujitegemea!! Hawajui kama Tanzania ilikuwa inaheshimika sana duniani kote! Wengi wanaamini kuwa hali ngumu ya kiuchumi ya Tanzania ilisababishwa na ubovu wa siasa ya ujamaa na kujitegemea!! Leo nitatumia kigezo cha thamani ya pesa ili kuakisi kiwango cha uchumi wa Tanzania kuanzia mwaka 1961 baada ya uhurui hadi mwaka 2020.
THAMANI YA SHILINGI YA TANZANIA NA ILE YA KENYA TOKA 1962 HADI 2022 DHIDI YA DOLA YA MAREKANI​

MWAKAUSDTSHKSHREMARKS
196117.147.14Mwanzo wa Nyerere
196217.147.14
196517.147.14
197017.147.14
197517.377.34
197817.717.73Mwanzo wa vita ya Kagera
198018.227.42Mwisho wa vita ya Kagera
1985117.4716.43Mwisho wa Nyerere na mwanzo wa Mwinyi
19901195.6022.91
19951574.7651.43Mwisho wa Mwinyi na mwanzo waq Mkapa
20001800.4176.18
200511128.9375.55Mwisho wa Mkapa na mwanzo wa Kikwete
201011395.6379.23
201511991.3998.18Mwisho wa Kikwete na mwanzo wa Magufuli
202012294.15106.45

Jedwali hapo linaonesha kuwa tangu Rais Nyerere alipoipokea Tanganyika (1961) hadi Tanzania mwaka 1978 shilingi ya Tanzania ndio ilikuwa na nguvu kuliko pesa za Kenya na Uganda, Dola 1 ilikuwa sawa na Tsh 7.71. Huo mwaqka wa 1978 vilifumuka vita vya kagera. Iddi Amin alivamia nchi yetu. Nyerere akatangaza vita dhidi ya Amin na vita ile tulishinda lakini ilikomba na kuharibu kabisa uchumi wetu!

Vita ya Kagera iliisha mwaka 1980 na hapo ndio tunaona shilingi yetu inaporomoka na kuwa dola 1 = Tsh 8.22 na ndipo walipoanza kutupiga gepu watu wa kenya. Kwa hiyo vijana mjue siyo ujamaa na kujitegemea uliotuporomosha bali ni vita ya kagera.

Kama ujamaa ungetuporomosha tungeona hasa poromoja hilo kuanzia mwaka 1967 baada ya kutangazwa kwa azimio la Arusha. Lakini hali ya kiuchumi haikutetereka kwa kuanzishwa kwa azimio la Arusha badala yake uchumi uliimarika sana. Tulikuwa na viwanda vingi na tulikuwa tunasafirisha sana mazao nchi za nje kama pamba, katani, kahawa, korosho nk.

Mwaka 84 kukawa na ukame wa kutisha sana na kukawa na njaa kubwa kiasi cha kupewa msaada wa unga toka marekani (almaarufu kama unga wa yanga maana ulikuwa wa njano). Hilo likawa ni tukio lingine la kutuporomosha!

Sasa mwaka 1985 akapokea mzee Ruksa (Mwinyi) dola ikiwa ni Tsh 17.47. Sera za mzee huyu ziliporomosha pesa yetu kwa asilimia 1119% (toka Tsh 17.47 hadi Tsh 195.60 kwa dola moja ya marekani). Kipindi hiki pesa yetu ilikosa kabisa thamani!! Vijana walikuwa wanatembea na maburungutu ya fedha ambazo hazikuweza kuwafikisha popote! Wafanyakazi walidharaulika sana kipindi hiki! Hadi awamu ya Mwinyi inamalizika dola moja ilikuwa na thamani ya Tsh 574.76. Tangu mwanzo wa awamu ya pili mwaka 1985 hadi mwisho wa awamu hiyo ya mzaa ruksa mwaka 1995 fedha yetu iliporomoka thamani kwa asilimia 5579.6%.

Mkapa alianza awamu yake ya tatu mwaka 1995 dola moja ikiwa ni Tsh 574.76 na alimaliza awamu yake mwaka 2005 dola moja ikiwa ni Tsh 1128.93. Kwa kipindi cha Mkapa shilingi yetu iliporomoka thamani kwa asilimia 196.42%. Pamoja na lawama kwa Mkapa ya kuuza mashirika yetu kwa bei ya kutupa na yeye mwenyewe kujiuzia kiwanda cha chuma kwa bei ya kuchekesha, lakini alizuia sana kasi ya kuporomoka kwa thamani ya shilingi yetu!! Wafanyakazi walianza kupata tena heshima kipindi cha Mkapa!!

Kikwete alianza awamu yake ya nne mwaka 2005 dola moja ikiwa ni Tsh 574.76 na alimaliza awamu yake mwaka 2015 dola moja ikiwa ni Tsh 1991.39. Kwa kipindi cha Kikwete shilingi yetu iliporomoka thamani kwa asilimia 346.47%. Hapa tunaona tena ongezeko la kushuka kwa thamani ya shilingi yetu lakini si kama kipindi cha mzee Ruksa! Wafanyakazi walifaidi sana kipindi cha Kikwente maana alikuwa anaongeza mshahara kila mwaka kwenda sambamba na thamani ya pesa!

Magufuli alianza awamu yake ya tano mwaka 2015 dola moja ikiwa na thamani ya Tsh 1991.39 na alimaliza sehemu ya kwanza ya awamu yake mwaka 2020 dola ikiwa na thamani ya Tsh 2294.15. Kwa kipindi cha Magufuli sehemu ya kwanza ya awamu ya sita shilingi yetu iliporomoka thamani kwa asilimia 115.2%. Wafanyakazi walifunga mkanda kipindi hiki maana hawakuongezewa kabisa mshahara na walipitia kipindi kigumu lakini kwa MATUMAINI kuwa uchumi unajengwa kwanza hatimaye mishahara iongezwe!

Ukiwalinganisha marais wote waliopita kwa ufanisi wao kwa miaka kumi ya mwanzo utapata kama ifuatavyo:
1. Nyerere atabakia kinara ambapo kwa miaka 10 ya mwanzo uchumi uliimarika sana kupitia kilimo na viwanda na thamani ya pesa yetu haikushuka hata kidogo badala yake ilipanda kidogo mwaka 1972 na kuwa dola 1 sawa na Tsh 7.02 hivyo kuwa na ongezeko la thamani la asilimia 1.68%.

2. Magufuli anamfuatia Nyerere akiwa ambapo kwa kipindi chake (bahati mbaya ni miaka 5 tu) pesa yetu iliporomoka kwa asilimia ndogo zaidi yaani asilimia 115.2%

3. Mkapa ni wa tatu ambapo alijitahidi kupunguza kasi ya anguko la pesa yetu. kKipindi chake pesa yetu iliporomoka thamani kwa asilimia 196.42%.

4. Wa nne kwenye foleni ni Kikwete ambaye kipindi chake pesa yetu iliporomoka thamani kwa asilimia 346.47%. Wa mwisho anayeshika mkia na kinara wa kuporomosha thamani ya pesa yetu ni mzee Mwinyi. Kipindi chake pesa yetu iliporomoka thamani kwa asilimia 5579.6%.

Kwa kifupi awamu ya kwanza ndiyo awamu pekee iliyoweza kutunza upinzani kiuchumi hapa afrika ya mashariki na pesa yetu ndiyo ilikuwa na nguvu na ni awamu pekee ambayo pesa yetu iliongezeka thamani angalau kwa hizo asilimia 1.68%. Awamu zote zilizofuatia pesa yetu iliporomoka thamani japo kwa viwango tofauti> Mporomoko wa kutisha ni wa mzee Mwinyi.

Kwa ufafanuzi huu unaotumia data watoto na vijana wanaomkejeli mwalimu Nyerere bila shaka mtashika adabu!!
 
Huwezi kuamini kuwa hadi mwaka 1980 shilingi ya Uganda ilikuwa na thamani kubwa kuliko dola ya marekani, na ndiyo ilikuwa kinara wa pesa yenye thamani kubwa afrika ya mashariki. Lakini baada ya mwaka 1980 shilingi ya uganda iliporomoka kwa kasi na tunavyozungumza sasa dola moja ya marekani ni sawa na zaidi ya Ush 3590. Mwaka 1980 dola 1 ilikuwa sawa na Ush 0.07
 
Uchumi ulijengwa na Nyerere au Mkoloni ?

Azimio la Arusha labda
Wakoloni waliondoka madarakani mwaka 1961. Maendeleo ya kiuchumi tokea hapo yalisimamiwa na Nyerere chini ya TANU. Sera za kiuchumi zilizofuatwa ni za TANU. Nyerere alikuwa mwalimu kwa taaluma lakini alikuwa amesomea pia uchumi. Alirasimisha siasa ya ujamaa na kujitegemea mwaka 1967 chini ya azimio la arusha.
 
Thamani ya pesa si kipimo kizuri Cha uchumi,pesa ya Oman ni zaidi ya Dola ya marekani..nyerere mwenyewe alikiri ujamaa ulishindwa,angefanikiwa mwinyi asingekuta nchi ya hovyo
Omani ni matajiri kuliko Marekani! kwa kigezo cha maliasili walizonazo ukilinganisha na idadi ndogo ya watu wao. Ukubali usikubali, thamani ya pesa ni kigezo muhimu sana cha uchumi wa nchi, japo si kigezo pekee. Ujue thamani ya pesa inabebwa na kiasi cha bidhaa na huduma ambayo nchi hutoa kwenye soko la dunia!!
 
Tanzania ya ujamaa wa nyerere ni ngumu kurudi, Tz imekuwa nchi ya wafanyabiashara na wakulima. Mjamaa akipewa nchi sidhani kama atafanikiwa, Labda wafanyabiashara wote wauwawe ama kufukuzwa nchini jambo ambalo si jepesi. Uhalisia ni kwamba serikali ya ccm na upinzani ambao una nguvu kiasi hawapo tayari kuruhusu ujamaa wa kiwango cha kipindi cha nyerere. Hii ni historia ambayo sidhani kama itajirudia kwa miaka mingi ijayo.
 
Omani ni matajiri kuliko Marekani! kwa kigezo cha maliasili walizonazo ukilinganisha na idadi ndogo ya watu wao. Ukubali usikubali, thamani ya pesa ni kigezo muhimu sana cha uchumi wa nchi, japo si kigezo pekee. Ujue thamani ya pesa inabebwa na kiasi cha bidhaa na huduma ambayo nchi hutoa kwenye soko la dunia!!
Huo ndio ukweli
 
Nyerere alifanya kwa uweza wake ingawa mda ulikuwa hauruhusu. .

Kama ningeweza kuchagua yupi aanze kutawala, mie ningeanza kwa mpangilio huu:
1: Samia - Angependeza sana kuwa mama wa taifa, kwani angewafurahisha sana wazungu waliokuwa na kinyongo kuiachia nchi
2: Kikwete - Angependeza sana kuendelea kazi aliyofanya mama, kwani wazungu wangependa kuwa na mtu anayeendeleza wale waliyoacha akiendeleza mama
3: Mwinyi - Huyu angekuja kukuza demokrasia na kuboresha mifumo iliyomtangulia
4: Mkapa - Huyu angekuja kufanya mapinduzi makubwa kwenye nchi yetu ikiwepo UBINAFSISHAJI wa makampuni ya serikali na viwanda
5: Nyerere - Huyu angekuja kuwanyang'anya vitu vyote vilivyo binafshishwa na kuleta siasa za ujamaa na kujitegemea
6:JPM - Huyu angepokea nchi ikiwa teyari kwenye mfumo wa chama kimoja na angeweza kuleta maendelea makubwa yenye tija, leo hii hela yetu ingekuwa na thamani nzuri ukilinganisha na dollar. .
 
Omani ni matajiri kuliko Marekani! kwa kigezo cha maliasili walizonazo ukilinganisha na idadi ndogo ya watu wao. Ukubali usikubali, thamani ya pesa ni kigezo muhimu sana cha uchumi wa nchi, japo si kigezo pekee. Ujue thamani ya pesa inabebwa na kiasi cha bidhaa na huduma ambayo nchi hutoa kwenye soko la dunia!!
So burundi nao wanatuzid kiuchumi?
Maana hela yao ni kubwa kuliko yetu.

Afu wingi wa rasilimali ndo nini maana DRC ina rasilimali nying kuliko nchi zote Africa je ndo uchumi mkubwa Afrika?

Au kenya ina uchumi mkubwa kuliko japan? Maana Ksh is more valuable kuliko Japanese yen.

Au uingereza ni zaid ya marekani kiuchumi?maana pound ni more valuable kuliko dollar.

Uchumi sio porojo za kisiasa una indicators zake.
 
Toka miaka ya 1980's mpaka leo ni muda ulitosha kabisa turudi kwenye mstari, niseme tu kuwa weupe vichwani pia imesaidia na inaendelea kusaidia sarafu yetu kuzidi kushuka thamani na bado itafika mpaka 1usd = 10000 tshs.
 
So burundi nao wanatuzid kiuchumi?
Maana hela yao ni kubwa kuliko yetu.

Afu wingi wa rasilimali ndo nini maana DRC ina rasilimali nying kuliko nchi zote Africa je ndo uchumi mkubwa Afrika?

Au kenya ina uchumi mkubwa kuliko japan? Maana Ksh is more valuable kuliko Japanese yen.

Au uingereza ni zaid ya marekani kiuchumi?maana pound ni more valuable kuliko dollar.

Uchumi sio porojo za kisiasa una indicators zake.
DRC wana maliasili lakini haziwezi kuchangia kwenye uchumi wao kwa sasa kwa sababu hawana uwezo wa kuingiza hizo maliasili kwenye soko la dunia kwa sasa! Nimesema thamani ya fedha ni kigezo muhimu na kikubwa japo siyo kigezo pekee kwenye kupima uchumi wa nchi!! Thamani ya pesa ni mojawapo ya hizo indicator, ukibisha hilo utakuwa wa ajabu sana!!
Thamani ya pesa inawakilisha uwezo wa manunuzi wa pesa husika! huwezi kubeza thamani ya pesa hata kidogo. Ninakumbuka kaka yangu alichaguliwa kwenda Mazengo sekondari mwaka 1971. Shilingi 100 (noti ya masai) ilitosha kufanya shopping yote kwa maana ya sanduku, mashuka mawili , ya shule kuanzia viatu, soksi, kaptura na shati (mbili mbili), mto, pamoja na nauli (ya msindikizaji maana wakati huo wanafunzi walikuwa iwanasafiri kwa kutumia warrant ) na pocket money! Na kumbuka ukiwa na shilingi moja unaenda kununua vitu dukani unarudi na change!!
 
Mwinyi kipindi chake shilingi yetu iliporomoka thamani kwa asilimia
1 USD = 134 Japanese Yen
1 USD = 117 Kenyan Shillings
1 USD = 11 Botswana Pula

Kwa akili za Wajamaa watakwambia uchumi wa Kenya na Botswana una nguvu kuliko wa Japan.
Nimesema moja ya vigezo vikubwa vya uchumi ni thamani ya pesa japo hicho siyo kigezo pekee. Kwa upande wetu miaka hiyo ya 70 thamani ya pesa yetu ilikuwa inaakisi thamani ya bidhaa tunazouza kwenye soko la dunia ikiwemo mazao muhimu kama pamba, katani, kahawa nk. Pia tulikuwa tunauza sana almasi. Thamani ya pesa yetu ilifanya watanzania wawe na higher parchasing power! Hilo halikanushiki!! Leta hoja kama unayo itakayoonesha kuwa uchumi wetu haukuwa mkubwa na bora miaka ile ya 60 na 70 kabla ya vita vya kagera.

Botswana uchumi wao ni mzuri sana! Mishahara ya $4000- $5000 huko ni ya kawaida. Watanzania wengi wako huko na hawana mpango wa kurudi Tz. Kenya uchumi wao ni mzuri kama Taifa japo kuna shida ya umaskini wa kupundukia kwa watu wengi kwa ajili ya uchumi huo kushikiliwa na watu wachache!! Hali kadhalika Marekani kama Taifa uchumi wake ni mkubwa sana lakini kuna maskini wengi sana huko!!
 
Kiwango cha umaskini Kenya ni asilimia ngapi na Tanzania ni ngapi?

Kipindi cha Mwinyi pesa yetu iliporomoka kwa asilimia 5579.6%. Lakini Mwinyi alishuhudia kwa karibu jinsi uchumi ulivyokuwa imara kipindi chote cha mwalimu Nyerere. Ndiyo maana akijilinganisha na mwalimu Nyerere Mwinyi alisema yeye ni kama kichuguu na Mwinyi ni kama mlima kilimanjaro.
 
Huwezi kuamini kuwa hadi mwaka 1980 shilingi ya Uganda ilikuwa na thamani kubwa kuliko dola ya marekani, na ndiyo ilikuwa kinara wa pesa yenye thamani kubwa afrika ya mashariki. Lakini baada ya mwaka 1980 shilingi ya uganda iliporomoka kwa kasi na tunavyozungumza sasa dola moja ya marekani ni sawa na zaidi ya Ush 3590. Mwaka 1980 dola 1 ilikuwa sawa na Ush 0.07
Baada ya kuingia dikteta Museven
 
Kipindi cha Mwinyi pesa yetu iliporomoka kwa asilimia 5579.6%. Lakini Mwinyi alishuhudia kwa karibu jinsi uchumi ulivyokuwa imara kipindi chote cha mwalimu Nyerere. Ndiyo maana akijilinganisha na mwalimu Nyerere Mwinyi alisema yeye ni kama kichuguu na Mwinyi ni kama mlima kilimanjaro.
Kwanini Mwinyi asikamatwe kwa uhujumu uchumi?
 
Mwinyi kipindi chake shilingi yetu iliporomoka thamani kwa asilimia

Nimesema moja ya vigezo vikubwa vya uchumi ni thamani ya pesa japo hicho siyo kigezo pekee. Kwa upande wetu miaka hiyo ya 70 thamani ya pesa yetu ilikuwa inaakisi thamani ya bidhaa tunazouza kwenye soko la dunia ikiwemo mazao muhimu kama pamba, katani, kahawa nk. Pia tulikuwa tunauza sana almasi. Thamani ya pesa yetu ilifanya watanzania wawe na higher parchasing power! Hilo halikanushiki!! Leta hoja kama unayo itakayoonesha kuwa uchumi wetu haukuwa mkubwa na bora miaka ile ya 60 na 70 kabla ya vita vya kagera.

Botswana uchumi wao ni mzuri sana! Mishahara ya $4000- $5000 huko ni ya kawaida. Watanzania wengi wako huko na hawana mpango wa kurudi Tz. Kenya uchumi wao ni mzuri kama Taifa japo kuna shida ya umaskini wa kupundukia kwa watu wengi kwa ajili ya uchumi huo kushikiliwa na watu wachache!! Hali kadhalika Marekani kama Taifa uchumi wake ni mkubwa sana lakini kuna maskini wengi sana huko!!

Hiyo purchasing power yetu ilikuwa ngapi hiyo miaka ya 60 na 70? Lete data. Umeongea mengi bila kuweka ushahidi zaidi ya huo wa thamani ya TSHS kwa USD.

Halafu Wajamaa mnapenda sana kutumia vita ya Kagera kama kisingizio cha kuharibu uchumi wakati Wahutu na Watusi walichinjana na baadaye wakaweza kuinua uchumi wao. Wakenya hao wanapigana na Wasomali mpaka leo, uchumi wao wameinua. Nyie bado mnamlaumu Idi Amini kwa Ujamaa wenu kufeli. Ujamaa ni sera mbovu sana.
 
Back
Top Bottom