Jackbauer
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,038
- 2,199
alikuwa kijana mtanashati,mweupe na mrefu wa wastani.
Safari yake ya soka ilianza mwanzoni mwa miaka ya tisini pale chuo cha ufundi arusha technical college.
Alisajiliwa na timu maarufu ya AICC arusha na baadae kuhamia timu ya ndovu ya mjini arusha pia.
Ndovu ambayo ilikuwa ikicheza ligi daraja la kwanza ilimuwezesha kijana huyu kusajiliwa na timu ya simba sc na baada ya misimu kadhaa alichukuliwa na wapinzani wa simba timu ya dar young africans.akiwa yanga alijipatia umaarufu mkubwa kwa uwezo wake uwanjani na alipewa jina la utani ''fundi''
kwa wapenzi wa soka la nje method mogella ungeweza kumfananisha na kiungo kama andre iniesta au xavi wa barcelona fc.
Mara ya mwisho nilikaa na mchezaji huyu kwenye kiosk cha HH nje ya uwanja wa shekh amri abeid,pembeni yake alikuwepo winga machachari aliyehamia yanga kutoka simba.huyu aliitwa thomas kipese aka uncle tom.
Baada ya hapo sikumuona tena method mogella lakini niliendelea kumsikia akiwika kupitia radio tanzania dar es salaam.
Ghafla taarifa za kifo za mwanandinga huyu zilitolewa kwa kusema alifariki huko nchini afrika ya kusini.mazingira ya kifo chake hayakuwekwa wazi mpaka leo hii.
Mwenye historia nzuri ya nguli huyu wa soka tanzania atuwekee kwa faida ya kizazi hiki na kizazi kijacho.
RIP MOGELLA "FUNDI"