Ki ukweli ni mikasi tu ndie mchangiaji aliekuwa sahihi kuitoa story nzima ya marehemu Method mogella jamaa alijiover dose na alikuwa mgonjwa alirudishwa toka Abu dhab alipokuwa amekwenda na Costantine Kimanda deal liliofanikishwa na Mpondela castro ila cha kuongezea tulipokwenda kuaga mwili wa marehemu Msimbazi center alizikwa na mkufu mkubwa wa Dhahabu wa msalaba kitu kilichopelekea kufukuliwa mwili wake na vibaka ikabidi asubuhi watu wanapita makaburi ya Buguruni wanaukuta mwili wa marehemu upo nje akazikwa tena cha ajabu kifo chake kiliwagusa saana watu ambao nao sasa ni marahemu pia mziray.gaga.bambaga.boli zozo.kizota.stephe mussa na issa athuman ambaye mleta mada anamchanganya kifo chake na method issa athuman mgaya yeye ndie aliefia afrika kusini na kwa taarifa yako tu marehemu wote ukiacha kizota wanasadiiwa walikufa kwa upugufu wa kinga zinazopambana na maradhi nyemelezi
![]()
From Left; Hamisi Thobias Gaga(marehemu), Saidi Mwamba Kizota (marehemu), David Mwakalebela, Method Mogella (marehemu) Abeid Mziba, Ken Mkapa(captain) na Salum kabunda Ninja(marehemu).
Ulimpima ukathibitisha kuwa alikufa kwa ngoma...tujaribu kuwa considerate hasa kwenye rumours.Mogela, alikuwa na uwezo wa kucheza namba zote isipokuwa kipa, l used to love him, nilisikitika sana niliposikia kafa kwa goma
Hakuna.midfielder mzuri ambaye tanzania imewahi kua nae kama marehem method, kwa sasa unaweza mfananisha na inesta
Mwenye dvd za huyu jamaa nione ufundi wake ani inbox plz
Hussein Marsha,Athuman China,Razack Yusuph...hao wote walikuwa kimeo au? Sikatai kuwa Method alikuwa mzuri lakini usiseme kuwa hakuna kama yeye TZ!
Acha masikhara bhana, kwani we ni mgeni na wabongo kwenye records keeping?
Mkuu kipindi kile tvt walikuwa wanarecord kama sikosei siamini kama hakuna kabisa zitakuwepo sema za ubora hafifu
Mkuu hao jamaa walikuwa wazuri lakini sio kwa kiwango cha mogella.Hussein Marsha,Athuman China,Razack Yusuph...hao wote walikuwa kimeo au? Sikatai kuwa Method alikuwa mzuri lakini usiseme kuwa hakuna kama yeye TZ!
Hapo kwenye nyekundu,hivi ni kweli Thom Kipese aliahamia Yanga akitokea Simba eeeh! mkuu acha utani ukweli alitokea Yanga kwenda Simba. kwa kuongezea, Method alichukuliwa Arusha na Meja Rashid Makame ( marehemu) akamleta JKT Pwani na kisha akampeleka katika timu aliyokuwa akiipenda (Makame) Simba lakini moyoni Method hakuwa na mapenzi na Simba.alikuwa kijana mtanashati,mweupe na mrefu wa wastani.
Safari yake ya soka ilianza mwanzoni mwa miaka ya tisini pale chuo cha ufundi arusha technical college.
Alisajiliwa na timu maarufu ya AICC arusha na baadae kuhamia timu ya ndovu ya mjini arusha pia.
Ndovu ambayo ilikuwa ikicheza ligi daraja la kwanza ilimuwezesha kijana huyu kusajiliwa na timu ya simba sc na baada ya misimu kadhaa alichukuliwa na wapinzani wa simba timu ya dar young africans.akiwa yanga alijipatia umaarufu mkubwa kwa uwezo wake uwanjani na alipewa jina la utani ''fundi''
kwa wapenzi wa soka la nje method mogella ungeweza kumfananisha na kiungo kama andre iniesta au xavi wa barcelona fc.
Mara ya mwisho nilikaa na mchezaji huyu kwenye kiosk cha HH nje ya uwanja wa shekh amri abeid,pembeni yake alikuwepo winga machachari aliyehamia yanga kutoka simba.huyu aliitwa thomas kipese aka uncle tom.
Baada ya hapo sikumuona tena method mogella lakini niliendelea kumsikia akiwika kupitia radio tanzania dar es salaam.
Ghafla taarifa za kifo za mwanandinga huyu zilitolewa kwa kusema alifariki huko nchini afrika ya kusini.mazingira ya kifo chake hayakuwekwa wazi mpaka leo hii.
Mwenye historia nzuri ya nguli huyu wa soka tanzania atuwekee kwa faida ya kizazi hiki na kizazi kijacho.
RIP MOGELLA "FUNDI"