Methali hii ina maana gani?

Wakuu,methali hii imekua ikinitatiza kujua maana yake 'Kata pua uunge wajihi'
Ahsanteni.
Katika maisha ya mwanadamu,mara kadhaa hukabiliwa na hali ambapo hupaswa kukiharibu au kukiacha kiharibike chenyewe kimoja kwa kutengeneza kingine,
Mwanadamu huchagua lipi la kuliharibu kwa minajili ya kulitengeneza jengine lililo muhimu zaidi,

Mfano labda unataka kujenga nyumba na kununua gari na una uwezo wa kufanya kimoja tu kwa wakati huo,hapo utazingatia kilicho muhimu zaidi kwako, wajihi/uso
 
Nashukuru kwa ufafanuzi mkuu,kwahio wajihi hapo ina maana gani?yaani ukate pua uunge 'wajihi' hio wajihi ni kitu gani km unajua.
 
Jibu lako limenikuna
Katika maisha ya mwanadamu,mara kadhaa hukabiliwa na hali ambapo hupaswa kukiharibu au kukiacha kiharibike chenyewe kimoja kwa kutengeneza kingine,
Mwanadamu huchagua lipi la kuliharibu kwa minajili ya kulitengeneza jengine lililo muhimu zaidi,

Mfano labda unataka kujenga nyumba na kununua gari na una uwezo wa kufanya kimoja tu kwa wakati huo,hapo utazingatia kilicho muhimu zaidi kwako, wajihi/uso
 
"Kata pua uunge wajihi" ni kuchagua kufanya jambo ambalo lina athari hasi lakini linaleta manufaa, yaani manufaa yake ni makubwa kuliko athari zake hasi. Ni kama kusema "bora nipoteze pua niponye uso (sura). Kwa mfano, unauza nyumba pekee uliyo nayo ili usome. Utalala nje au kuhangaika kwenye nyumba za kupanga, lakini unajua kesho nikimaliza kusoma nitarudisha vyote. Hapo umekata pua ukaunga wajihi.
 
Asante kwa elimu mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom