Meseji za baba yangu zinanikwaza

Meseji za baba yangu zinanikwaza

Baba yangu akiwa anatoka kazini anajua mi nakua nipo nyumbani. Ananiuliza nyumbani nini hakuna namuandika kwa meseji anapitia supermarket ananunua analeta nyumbani.

Leo siku ya nne anakosea kutuma meseji badala atume kwa mama anatuma kwangu. Meseji sio nzuri, ni meseji za mapenzi na nyingine matusi. I find it really disrespectful, sitakiwi kujua mambo wanayofanya wakiwa wenyewe.

Je nimwambie kama anakosea kutuma au ninyamaze maana mi sitaki kuona meseji zake kama hizi.

Nifanye nini?
ameandikaje labda ili tupate kukusaidia. pengine hata sio za matusi.
 
Wewe Unajua anakosea kutuma sasa badala ya kuzifuta haraka unazihifadhi na kuzirudia rudia kuzisoma hizo msg zinakusisimua? Basi sema ukweli kama unamtaka babaako ushauriwe cha kufanya hapa
Kumbe ni kosa lake kutumiwa msg na babake!?
 
Akituma izo msg zirudishe kwake na mwisho edit umwambie anakosea.. Kama kwel anakosea hatarudia tena...
 
Mwambie kwa kumrushia hizo text na chini yake muulize hii meseji inanihusu kama unaogopa mpe simu mama yako muonyeshe hizo meseji wamalizane wenyewe
Hapana huu utakuwa uchonganishi
Mtoto kama mtoto asimamie nafasi yake asiwe kikwazo kwa wazazi wake

Kwanza amwambie baba yake kama atakuwa amekosea naamini atajirekebisha kwa kuwa makini pindi atumapo msg kwa mkewe

Kama anafanya kusudi pia naamini ataendelea na tabia hiyo tena zaidi ya awali

Akiendelea mwambie kuwa hutaki tabia hiyo inakukera na huipendi hivyo aache kwani wewe ni nwanawe si mkewe, pia mwambie akiendelea utamwambia mama

Ili uwe na ushahidi wa kutosha yote hayo Fanya kwa njia ya meseji na usizifute

Kama ataendelea basi mwambie mama juu ya jambo hilo ili aongee na mumewe

Epuka kuwa chanzo cha wazazi kugombana.
Yangu ni hayo akili yakuambiwa changanya na yako
 
Mwambie kwa kumrushia hizo text na chini yake muulize hii meseji inanihusu kama unaogopa mpe simu mama yako muonyeshe hizo meseji wamalizane wenyewe
Amrudishie tu izo msg pale anapozituma, atakua anakosea maana anasema nyingine za matusi..... Asimpe mama kwanza aisee itamuua sana
 
Baba yangu akiwa anatoka kazini anajua mi nakua nipo nyumbani. Ananiuliza nyumbani nini hakuna namuandika kwa meseji anapitia supermarket ananunua analeta nyumbani.

Leo siku ya nne anakosea kutuma meseji badala atume kwa mama anatuma kwangu. Meseji sio nzuri, ni meseji za mapenzi na nyingine matusi. I find it really disrespectful, sitakiwi kujua mambo wanayofanya wakiwa wenyewe.

Je nimwambie kama anakosea kutuma au ninyamaze maana mi sitaki kuona meseji zake kama hizi.

Nifanye nini?
Kaa kimya na wala usijaribu kufungua bakuli lako, sorry i mean puuuuuuuuuuuuuu.........zia hizo sms.
 
Huyo afrit ni gia yake hiyo kujifanya kakosea kumbe anakuringishia (doli doli doli samora )ili umuone kuwa fundi bonge la mido (kiungo )anachukua kule anatupa huku hiyo mbinu ya kizamani sana anayotumia mwanaume mwenzagu
 
Iko hivi ndugu, katika majaribio kadhaa niliyowahi kusikia wazazi wanaanzaje na baba zao ni mbinu mojawapo walizitumia na ukijifanya kulegeza unaliwa mchan kweupe, nakuhakikishia baba amedhamiria huwa tunakosea mara moja lakini sio mara mbili tatu! Na si ajabu ameanza ushirikina kaa chonjo utaliwa.

Duuuh.. Kwa mujibu wa uzinwake mpya ashaliwa tayari
 
Back
Top Bottom