Meseji (SMS) za dawa za Kiganga: Je, hawa ni matapeli? TCRA mko wapi? Namba wanatoa wapi?

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,428
Wakuu ni kama Mara 3 hivi napokea meseji kwenye simu yangu inayoelezea masuala ya dawa za kiganga hasa mambo ya "Ndagu" na zindiko la biashara.

Meseji ya kwanza nliyowahi kutumiwa ilikua inasema hivi:-

"Mjukuu wa KISIRE naona biashara ya mabasi sasa inatosha umeshanunua mabasi mengi, sasa uje tena sumbawanga nikupe dawa ya kusafisha nyota na ya ndagu Mimi ni babu yako wa Sumbawanga"

Leo nimetumiwa hii:-

" Ile Dawa Ya Kusafisha nyota Yako Nazindiko Lamalizako Tayali Nimekamilisha Mjuku Wang Uje Uchukue Nashukulu Pia Kama Ndagu Imeaza Kufanya Kazi"

Je hawa ni matapeli!!? Kwa anaejua suala hili atuambie.

TCRA na Serikali wanatulindaje wananchi? Kwanini namba zimesajiliwa na watu wanaendelea kufanya uhalifu huu?

Sampuli za SMS na namba kadhaa zinazotumiwa:














Habari zaidi, soma=>ONYO LA POLISI: Ujumbe wa simu kutumiwa fedha, kuwasiliana na mganga ama kushinda bahati nasibu
 
Kumekuwa na utapeli ambao mtu hutuma sms kujifanya kumsifia mganga wake wa kienyeji akishukuru kupata mari au kwa wanawake akisifiwa kuweka ndoa vizur mwanzo niliaanza kupata sms mimi nikajuwa aiza nimtu alikuwa akikosea sasa sms izo zimeanza kuingia kwenye simu ya mke wangu zikiwa na ulagai wamaswara ya ndoa je nawewe umesha pata sms kama hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie washatuma sana mojawapo ni hii

Sent from Ili iweje
 

Attachments

  • Screenshot_20170726-183156.png
    18.9 KB · Views: 312
Hivi kuna watu huwa wanawaamini hawa matapeli kweli?

Sent from Ili iweje
 

Attachments

  • Screenshot_20170809-191204.png
    12.1 KB · Views: 242
  • Screenshot_20170809-191135.png
    12.1 KB · Views: 223
Namba si wanakisia tu, alimradi mtu ana salio au mesej za bure utaipata tu
 
Wanatuma sana..walinitumia kwa mara ya kwanza nikawa sijajua kama ni magumashi kwakua simu yangu huwa inaguswa na vjana hapa home nikaona ngoja nimpigie kujua ni nani alikua anawasiliana nae..nikaona anaongea kama msukuma hv nikamwambia mwaweja lolo
 

Hawa kichwani hakuna kitu wanatapeli ivi Je wangekua na akili kama Chenge naamini wangeuza nchi kabisa wakatokomea Duniani uko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…