Meremeta & TANGOLD Revealed!

Mimi siku zote nilikuwa najua Meremeta ni kampuni ya jeshi na walikuwa, ubia na kampuni moja kutoka nje na Gen Mboma baada ya kustaafu jeshini nadhani alikuwa mkurugenzi wa hiyo Meremeta.
 
Duh! na kuzungumzia biashara ya jeshi equally kuingilia masuala nyeti ya kiulinzi na kiusalama, na hivyo hayapaswi kuwa hadharani. BTW hivi Meremeta iliingizia kiasi gani jeshi letu na mapato hayo yaliingizwa kwenye bajeti ya serikali?
 
Mafuchila, shughuli za jeshi ni za Ulinzi hivyo chochote kilichofanywa na kampuni hiyo ni kusaidia shughuli za Ulinzi na hivyo ni za usalama wa TAifa. Hivyo kuulizia mchango wa Meremeta ni kuingilia siri za serikali.
 
Je, umekwisha gundua nani yupo nyuma ya hizi deal zote chafu?
 
Je, umekwisha gundua nani yupo nyuma ya hizi deal zote chafu?

Dua,
Hapo ndipo Jaji Bomani anapowaomba kina Mgonja na Karamagi wasiende Mahakamani, kwani wakienda tutajua nani yupo nyuma ya hizi dili chafu.
 
hivi kama hakuna wa kwenda mahakamani ni nini kitafuatia baada ya hapo,masikini wabunge wa ccm aibu hii wataiweka wapi sijui.
 
Je, umekwisha gundua nani yupo nyuma ya hizi deal zote chafu?


Dua, Pandora alikatazwa na miungu ya kigiriki kutofungua kisanduku kimoja ingawa alikuwa na uhuru wa kufanya mambo mengine mengi. Wakati huo wote ulimwengu ulikuwa unaishi kwa amani na furaha na maovu yoyote hayakuwemo. Hakukuwa na misiba na huzuni. Lakini kutokana na udadisi wake mwingine, wakati hakuna mtu aliyemuona.. pandora akaamua kufungua kile kisanduku alichokatazwa... matokeo yake yaliyotoka humo haiwezekani tena kuyarudisha.... CCM haiko tayari kufungua sanduku la pandora.. kwani likifunguliwa vilivyomo haviwezi kurudishwa tena!
 
..in my other posting niliuliza isije kuwa Dr.Slaa ameibuka na mafaili asiyopaswa kuwa nayo. wasije tu wakambana kama walivyombana Seif Sharrif Hamad.

..upande mwingine inawezekana kuna ulaji,wizi,jinai imetokea katika hiyo account ya meremeta. sasa kumbana Dr.Slaa itakuwa ni kumuumiza mtu mwenye nia njema na taifa letu.

..CCM wanaweza kuamua kuuchuna kuhusu Buzwagi, wakangangana na hili suala la account za Meremeta kwamba ni suala la Usalama.
 
Wale wote wanaoshauri mafisadi wasiende mahakamani wanaogopa kuumbuliwa. Including Judge Bomani. Mmesahau lile sakata za maeneo ya uwindaji? Familia ya Bomani ilitajwa kule. This issue is not going away anytime soon.
 
Mimi siku zote nilikuwa najua Meremeta ni kampuni ya jeshi na walikuwa, ubia na kampuni moja kutoka nje na Gen Mboma baada ya kustaafu jeshini nadhani alikuwa mkurugenzi wa hiyo Meremeta.

Huo ulikuwa mpango wa kumnyamazisha Mboma na other senior Soldiers who matter, baada ya Nkapa kuwa fisadi, so kwa usalama wake ndio hivyo, na zaidi ya hapo mboma alipewa machimbo merereani
 
mwaka huu ccm kazi kweli kweli bado nasubiri kombora funga mwaka linalokuja hivi karibuni nafikiri Dr.slaa akitoka ulaya. nahisi litakuwa funga mwaka hasa kwa jinsi linavyosubiriwa kwa hamu ninachoomba tu nataka JK naye awepo asisubiri kusimuliwa maana amezungukwa na mashushu ambao hawampi tarifa zote.
 
Let it be, if Pandora box opening will result to the end of udhalimu, Uhujumu and Ufisadi, i would rather see tha take place than Amani, Mshikamano na Utulivu that encourages Uhujumu with no fear that there are 90% of Tanzanians who live in abject poverty.

Revolution will not be televised!
 

Great job trying to figure out this shenanigan Mister Kishoka! The above scenario sounds quite convincing and I would say even plausible.

And if you are searching for answers to the two questions you've posed in your posting, then you need look no further than the sentence right next to your second question, namely the generals at JWTZ ate up everything!!

Tanzanians don't and never ever will have the professional expertise to run a capital intensive, and not least organizationally and technologically demanding project of the magnitude and size as this projected gold mine. So basically they fucked up everything and eventually the generals fleeced the company.
 
  • Mystery company that received billions from BoT, then filed for bankruptcy and voluntary liquidation: The SA connection

  • All listed directors based in South Africa, one linked to top SA bank

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam


A MYSTERY company associated with the now defunct Meremeta Gold company, Deep Green Finance, has now been inextricably linked to directors of a major South African bank which was a recipient of billions of shillings from the Bank of Tanzania.

According to THISDAY’s latest findings, official records list the directors or managers of Deep Green Finance as Mark Ross Weston (a New Zealand national), Anton Taljaard and Rudolph van Schalkwyk (both South African nationals).

Schalkwyk is also the head of the structured trade and commodity finance unit at Nedbank Limited, one of South Africa’s biggest commercial banks.

All three listed directors of Deep Green Finance Co. Limited, which received up to 8bn/- in BoT payments under dubious circumstances, are residents of South Africa.

It has already been verified that the relatively obscure company was registered in March 2005, and by August of the same year had already landed a payment cheque in US dollars equivalent to 1,546,778,778.92/- from the central bank.

And between September and December of the same year (2005), Deep Green Finance Co. Ltd was given further ’financial support’ from the central bank totalling more than 6bn/-.

Well-placed sources have asserted that Deep Green Finance was directly involved with both Meremeta Gold Limited and Tangold Limited, local companies which at one time operated the Buhemba gold mine in Musoma, Mara Region.

Before being liquidated some time ago, Meremeta Gold was registered as a joint venture company owned on a 50-50 basis by the Tanzanian Government and a private South African company called Trinnex (Pty) Limited.

The assets and liabilities of Meremeta Gold - including the Buhemba gold mine ? were later transferred to Tangold Limited, being a new company ostensibly wholly owned by the government.

Both Meremeta Gold and Tangold have also been the beneficiaries of questionable BoT payments to the tune of over $130m (approx. 160bn/-) through accounts at various banks.

In the case of Meremeta Gold, investigations by THISDAY have already established that the central bank made a payment of over $118m (approx. 150bn/-) to Nedbank ? the same South African bank where one of the Deep Green Finance directors is a senior officer - through the New York-based HSB Bank.

This payment was apparently made to liquidate a loan issued to Meremeta Gold after it had filed for bankruptcy. Official audit queries have since been raised as to why the government -- through the central bank -- decided to clear the loan on behalf of Meremeta Gold after it became bankrupt, instead of Nedbank itself filing its claim directly to the liquidator.

It has been further revealed that BoT paid an additional $13.34m (approx. 17bn/-) to another bank account under the name of Tangold Limited, at the National Bank of Commerce Limited corporate branch in Dar es Salaam.

Government sources have told THISDAY that in order to effect the payments to Meremeta Gold and Tangold, BoT purchased a huge 155bn/- Treasury bond and later exchanged the amount into US dollar currency.

Meanwhile, a Deep Green Finance company financial statement filed by the end of November last year shows that the firm had recorded an estimated surplus of $7,880 (approx. 10m/-) after paying all debts in full.

Like Meremeta Gold, Deep Green Finance had also filed for voluntary liquidation. But in the case of the latter, the bankruptcy was filed hardly two years after its official establishment and having already received billions of shillings from BoT within its relatively short lifespan.

Deep Green Finance filed for ’member’s voluntary winding-u’? on April 24 this year, declaring that board members not identified in the document had appointed Protase Rwezahura Gervas Ishengoma as liquidator with effect from July 27 this year.

Ishengoma, a partner with the prominent Dar es Salaam law firm IMMA Advocates, was named as subscriber and first shareholder of Deep Green Finance Co. Ltd. The voluntary winding-up has been filed under section 360 of the Companies Act of 2002, as stated in the notice delivered to the Business Registration and Licensing Authority (BRELA).

Source: ThisDay
 
Hiki bila shaka ndio kinawafanya hawa jamaa washindwe kumpeleka DR. SLAA mahakamani.

Kumbe kuuzwa kwa NBC kulikuwa ni ili kuweza kuwafanya hawa jamaa kiuweza kufanya money loundaring eheee......

Watetezi wa ufisadi mko hapo?
 
...kama wanashindwa auditing ya pale hazina tuu je hawa watawapata wapi ili warudishe hizo pesa? tushaumizwa hapo na hakuna kitu tunaweza kufanya na muungwana naona speed za safari zimeongezeka tena,kazi ipo na kila mtu atajijua mana viongozi wetu wanajijua wenyewe tuu
 
Was it the South African who borrowed money or it was repayment of their investment in the joint venture with JWTZ/TPDF which was 50% owner of Meremeta and Tangold who had land and SA had capital?

Tutapiga chenga sana, lakini we need to ge back to the local shafreholders who failed to run the companies forcing the Government to bail them out through BOT in the name of Amani, Utulivu and Mshikamano.

Rejeeni maandishi yangu ya "On Meremeta"!
 
Great job trying to figure out this shenanigan Mister Kishoka! The above scenario sounds quite convincing and I would say even plausible.

And if you are searching for answers to the two questions you've posed in your posting, then you need look no further than the sentence right next to your second question, namely the generals at JWTZ ate up everything!!

Tanzanians don't and never ever will have the professional expertise to run a capital intensive, and not least organizationally and technologically demanding project of the magnitude and size as this projected gold mine. So basically they fucked up everything and eventually the generals fleeced the company.

It is interesting to see how we have at least 15 pages talking about Dr. Balali's health and tuhuma za Ulaji BOT, his green card status and all other issues.

The truth about BOT money is that to justify expenses, someone has been forced to cook books to cover up the "necessary" expenses that were result of primary shareholders of Meremeta, Tangold and Mwananchi Green failing to produce an ounce of any product (dhahabu, mchanga) on this whole scheme!

Balali will be accountable for allowing Serikali to bulldoze him to cook books to cover up covert operations of Jeshi and CCM who were the main benefactors of all this money claimed Debt Services and Minara ya Benki!

Nendeni Ulinzi, Hazina na Madini! has anyone ever wonder why viongozi wa Serikali are now listed board of directors on Meremeta and Tangold? it is not due to their personam ambitions to be investors like Mkapa and Yona on Kiwira, but it is due to their official capacities in tyhe government.

Kufilisika kwa Meremeta na Tangold si makosa ya SA waliotoa mtaji, bali ni hao majemedari wetu walipewa dhamana na ardhi kule Buhemba!
 
Mkono atuhumu kampuni ya Meremeta kuchota mabilioni BoT

Ramadhan Semtawa Dar na Beldina Nyakeke, Musoma

MBUNGE wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono ameituhumu Kampuni ya Meremeta kuwa ni ya kitapeli na kwamba ilijichotea mabilioni ya shilingi kwa mgongo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa madai ya kununua dhahabu katika Mgodi wa Buhemba (BGM).

Mkono alitoa madai hayo wakati akitoa maoni yake kwenye Kamati ya Kuchunguza Mikataba ya Madini iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete, mwishoni mwa mwaka na kuwa chini ya uwenyekiti wa Jaji Paul Bomani.

Akitoa maoni yake, alipendekeza kuwa mikataba yote ya madini nchini ifumuliwe upya ili iwanufaishe Watanzania wote, kuliko hivi sasa ambapo mapato ya madini yanaishia mikononi mwa watu wachache.

Alifafanua kwamba, Kampuni ya Meremeta ilichota fedha kwa ajili ya kununua dhahabu katika mgodi wa Buhemba, lakini kila ilipofikisha mzigo Afrika Kusini, ilidai ya kuwa imeibiwa.

Aliitaka Mkono kamati hiyo kwenda Afrika Kusini kuchunguza ili kupata ukweli kama dhahabu hiyo iliibwa.

Alisema kiasia cha gawaio cha Sh 250 milioni kwa mwaka kutoka kwa baadhi ya makampuni, ni kidogo kwani hakiwanufaishi Watanzania walio wengi iliinganishwa na faida wanayopata wawekezaji wa kwenye sekta hiyo.

Mbunge huyo alifafanua kwamba, dhana ya 'Maisha bora kwa kila Mtanzania' imekuwa ni ndoto kwa wakazi wa Kata ya Buhemba kutokana na kuzorota kwa huduma za jamii kulikosababishwa na mgodi huo.

Kwa upande wao, wananchi wengine waliohojiwa walisema mgodi huo unamilikiwa na vigogo ambao ni watuhumiwa wa ufisadi katika Serikali ya Awamu ya Tatu na iliyopo madarakani, tofauti na inavyoelezwa kwamba unamilikiwa na serikali.

Wakazi wa Kata ya Buhemba walisema hayo wakati wakitoa maoni yao kwa kamati hiyo ambayo ujumbe wake uliongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto kabwe.

Walisema kutokana na mgodi huo kumilikiwa na mafisadi kwa maslahi yao binafsi, hali za wakazi wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo zinazidi kuwa duni kufuatia huduma muhimu za kijamii kukosekana katika kata hiyo.

Walifafanua kuwa huduma mbalimbali za kijamii zilizokuwa zikipatikana katika vijiji hivyo kabla ya kuwepo kwa mgodi huo, hivi sasa hazipo baada ya kuvunjwa na kuharibiwa kabisa na uongozi wa mgodi.

Huduma hizo ni pamoja na maji, elimu, barabara na afya ambazo kwa pamoja zilibomolewa na mgodi kwa maelezo kuwa wangepatiwa huduma bora zadi ya zilizokuwepo awali.

"Awali tulikuwa na vyanzo tisa vya maji vya asili, lakini mgodi ulipokuja uliviharibu vyote kwa vile vilikuwa ndani ya eneo la uchimbaji," alisema mkazi wa kijiji cha Biatika, Simon Chacha na kuongeza:

"Zahanati yetu tuliyokuwa tukiitegemea kwa ajili ya huduma za kiafya hasa kwa wajawazito, pia ilivunjwa kwa ahadi ya kujengewa nyingine ya kisasa, lakini tuliambulia ramani tu."

Naye Mchungaji wa Kanisa Anglikana Buhemba, Samwel Nyakarungu alisema:, "Tumefanyiwa hujuma kwani tunasikia kwamba hata viongozi wetu wakuu wa Wilaya ya Musoma na mkoani Mara, wana maslahi kwenye mgodini huo, hivyo katika suala hili tunaamini kwamba hawatweza kututatua kero zetu."

Mchungaji huyo aliendelea kusema: "Hii hali imechangia kwa kiasi kikubwa wakazi wa Kata ya Buhemba kuendelea kutumnia maji ya sumu kutoka kwenye mashimo yaliyokuwa yakitumika kuchimba dhahabu".

Alisema wananchi wa Kata hiyo wanaishi katika lindi la umasikini ktuokana na kutokuwa na shughuli za kufanya, kwa ajili ya kujiletea maendeleo kufuatia ardhi waliyokuwa wakiitegemea kwa ajili ya kilimo kuchukuliwa na mgodi.

Mchungaji huyo alifafanua kuwa wakati hali ikiwa ni hivyo bado hakuna mrahaba unaotolewa na uongozi wa mgodi huo kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika kata hiyo.

Wananchi waliitaka Kamati hiyo kuwahoji viongozi hao wa wilaya na mkoa juu ya mmiliki halisi wa mgodi huo ambao sasa umefungwa. Mgodi huo ulianza uzalishaji mwaka 2002 na kufungwa Januari, mwaka huu.

Kampuni ya Meremeta imejaa utata kutokana na kuelezwa kwamba ni ya serikalini, lakini huku nafasi ya serikali ikwa haijulikani.

Kampuni ya Meremeta imehusishwa na aliyekuwa Gavana wa BoT Daud Ballali, ambaye mkewe Anna Muganda na vigogo mbalimbali wa serikali iliyopo na iliyopita akiwemo Andrew Chenge.

Kamati ya Madini iliundwa na Rais Kikwete mapema mwishoni mwaka uliopita, kama moja ya hatua za kuhakikisha madini yanayochimbwa yananufaisha nchi na watu wake.


Source:
Mwananchi
 
Back
Top Bottom