BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,009
Ikulu ya Ben Mkapa iliibeba Meremeta
Mwandishi Wetu Aprili 9, 2008
Raia Mwema
SASA ni wazi, uongozi wa awamu ya tatu chini ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa ndio ulioshinikiza na kuidhinisha kuanzishwa kwa Kampuni ya Meremeta Gold, inayohusishwa na upotevu wa Sh bilioni 155, ndani ya Benki Kuu (BoT), imefahamika.
Habari za uhakika na nyaraka, zimethibitisha kwamba uongozi huo chini ya Mkapa ulihusika ama kushinikiza moja kwa moja mchakato wa kuanzishwa kwa Meremeta na hatimaye kuitafutia fedha za kufanyia kazi, fedha ambazo hata hivyo sasa zinahofiwa kupotea.
Tayari Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG), Ludovick Utouh, ametamka kwamba ofisi yake haijawahi kukagua hesabu za Meremeta Gold, na kampuni hiyo tata haimo katika orodha ya makampuni yanayomilikiwa na Serikali ama Serikali kuwa na hisa.
Raia Mwema imeiona barua kutoka Ikulu, iliyoandikwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Matern Lumbanga, kwenda benki moja ya Uingereza, ikieleza kwamba Mkapa kupitia kikao cha Baraza la Mawaziri mwaka 2000, ndiye aliyetoa idhini ya kuanzishwa kwa shughuli za uchimbani dhahabu katika eneo la Tembo na Buhemba, mkoani Mara.
Katika hali isiyo ya kawaida, Ikulu ndiyo iliyobeba jukumu la kuithibitisha na kuitambulisha Kampuni ya Meremeta kwa Deutch Bank AG London, iliyoko nchini Uingereza kwa nia ya kupata mkopo wa uendeshaji wa mgodi huo ambao kwa sasa umefungwa na kampuni hiyo kufilisiwa.
Hii ni kuthibitisha kwamba tunafahamu kuwapo kwa hazina kubwa ya dhahabu nchini Tanzania ambayo haijalinufaisha Taifa na Serikali kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, ilianzisha mradi wa Meremeta kwa nia ya kununua dhahabu kwa wachimbaji wadogo.
Baadaye mwaka 2000, Rais (Mkapa) kupitia Baraza la Mawaziri aliazimia uchimbaji mkubwa wa chini ya ardhi katika eneo la Tembo na uchimbaji mwingine wa kawaida katika eneo la Buhemba, kaskazini mwa Tanzania,
inaeleza barua hiyo ambayo kivuli chake kimechapishwa ukurasa wa kwanza wa toleo hili, iliyohitimisha kwa kusema kwamba mradi huo utakuwa na manufaa kwa Taifa.
Hata hivyo, katika barua hiyo inatajwa kampuni ya Nedcor Trade Services Limited ya Afrika Kusini kuwa ndiyo iliyotoa mkopo wa fedha za kuanzishia mradi huo chini ya usimamizi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, iliyokuwa inatajwa sana kuwa mmiliki wa mgodi huo awali kabla ya kubainika kuwapo kwa utata mkubwa.
Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma, Utouh, alisema wazi kwamba Meremeta haimo katika orodha ya makampuni na mashirika ya umma ambayo yamewahi kukaguliwa na ofisi yake, na hivyo kuibua utata mwingine kwa kuwa huko nyuma kampuni hiyo imekuwa ikitajwa kuwa ya umma.
Utata huo unaongezwa na taarifa za kwamba Serikali kupitia Msajili wa Hazina ilitoa cheti ya kuithibitisha Meremeta kuwa kampuni ya umma tokea Oktoba mosi, 1997 baada ya kudaiwa kwamba Serikali ilikuwa na hisa katika kampuni hiyo, hisa zilizokuwa na zinazoendelea kushikiliwa na watendaji wakuu serikalini. Baadhi ya watendaji hao wamo serikalini na wengine sasa wako nje.
Habari zinasema kwamba tayari uchunguzi wa kina umekwisha kuanza kufuatilia hasa zilikokwenda fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni 155/- zikiwa ni nyingi zaidi ya zile zilizochotwa BoT kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA). Sakata la EPA linahusisha Sh bilioni 133/-.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari serikalini, uchunguzi huo umekwenda mbali zaidi baada ya watendaji wakuu ndani ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Wizara ya Ulinzi na JKT, kupata hisia za kuwapo kwa mikono michafu katika mradi wa Meremeta.
Habari zinasema sakata la Meremeta linaweza kuwa kubwa na zito zaidi kutokana na maelezo ya uwezekano wa kuwapo wahusika wanaofahamika duniani katika biashara chafu na hivyo kuibua mjadala mwingine mkubwa utakaovuka nje ya mipaka ya Tanzania.
Kampuni ya Nedcor Trade Services Limited ya Afrika Kusini, inaelezwa kuwa na uhusiano na benki ya Nedbank ya Afrika Kusini ambako sehemu ya fedha hizo zilipelekwa kutoka BoT. Baadhi ya watumishi wa benki hiyo wamekuwa wakitajwa kuwa wakurugenzi wa kampuni nyingine tata ya Deep Green Finance Limited, ambayo sasa haipo.
Deep Green Finance Limited ilisajiliwa nchini, ikachota fedha kutoka BoT, kabla ya kufilisiwa bila ya maelezo ya kutosha ya madhumuni hasa ya kuanzishwa kwa kampuni hiyo katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2005.
Kashfa ya Meremeta inaelezwa kuwa kubwa zaidi ya ile ya EPA kutokana na kwamba uwezekano wa kurejesha fedha hizo ni mdogo kutokana na kwamba ziliingia katika mkondo unaoihusisha zaidi Serikali yenyewe na watendaji wake na wafanyabiashara wa kimataifa.
Tayari Kamati ya Rais inayochunguza sekta ya Madini, chini ya uongozi wa Jaji Mark Bomani, imeufuatilia mradi huo kwa kwenda Buhemba na pia kuwaita watendaji kadhaa wa Serikali akiwamo Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, ambaye inadaiwa taarifa hizo zimemshitua.
Kwa mujibu wa Gavana Profesa Ndulu, kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu za malipo ya fedha hizo za Meremeta ambazo ni zaidi ya zile za EPA zilizolipwa kwa utaratibu wa Dhamana za Hazina (Treasury Bonds).
Jaji Bomani aliliambia Raia Mwema hivi karibuni kwamba Kamati yake haitaficha kitu na kwamba baada ya kutembelea Buhemba na kuchunguza mambo yanayohusiana na mgodi huo, itatoa mapendekezo yake katika ripoti.
Baadhi ya wakurugenzi wa Kampuni ya Meremeta ambao wanaelezwa kuwa katika nafasi hizo kutokana na nyadhifa zao bado wanaendelea kushikilia hisa hizo akiwamo Gavana wa zamani wa Benki Kuu, Dk. Daudi Ballali, ambaye ajira yake ilisitishwa na Rais Jakaya Kikwete.
Tayari kuna habari kwamba kumekuwapo na juhudi za makusudi zinazofanywa na baadhi ya watendaji serikalini ambao wanajipanga kuzuia kuanikwa kwa ufisadi huo mkubwa.
Fedha hizo ambazo zilibadilishwa kuwa Dola za Marekani 131,736,628.73 kwa maelekezo yaliyotolewa Desemba 20, 2005, siku moja kabla ya kuapishwa kwa Rais Jakaya Kikwete, zilihamishwa kwenda Afrika Kusini na kuingizwa Nedbank, na nyingine kuingizwa katika akaunti za kampuni ya Tangold na Meremeta.
Taarifa za wakaguzi zinaonyesha kwamba baada ya ununuzi huo wa dhamana, Benki Kuu ilizibadilisha sehemu ya dhamana hizo kuwa dola za Marekani 118,396,460.36 ambazo zilipelekwa kwenye akaunti moja isiyojulikana ya Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini, benki hiyo ikiwa imezipokea fedha hizo kupitia HSB Bank ya New York, Marekani zikitajwa kuwa malipo ya madeni ya kampuni mufilisi ya Meremeta Ltd.
Nyaraka ambazo Raia Mwema imeziona zinaonyesha kwamba sehemu nyingine ya fedha hizo zipatazo Dola za Marekani 13,736,628.73 zililipwa kwa kampuni ya TANGOLD kwenye akaunti ya kampuni hiyo iliyoko Benki ya NBC Corporate Branch, Dar es Salaam.
Mbali ya kamati ya madini na wakaguzi, kwa nyakati tofauti, kuhoji malipo hayo, bado usiri na juhudi kubwa za kufunika masuala hayo zimekuwa zikiendelea kufanywa.
Mwaka jana Mbunge wa Karatu Dk. Willibrod Slaa (CHADEMA), aliliingiza suala hilo katika hoja yake iliyokuja kugonga mwamba baadaye.
Katika hoja yake hiyo, Dk. Slaa alibainisha kwamba Meremeta Ltd. ni kampuni binafsi ya kigeni iliyoandikishwa Agosti 19, 1997 katika kisiwa cha Isle of Man nchini Uingereza na kupewa namba ya usajili 3424504, ikimilikiwa na TRIENNEX (PTY) LTD ya Afrika Kusini yenye asilimia 50 ya hisa za kawaida na Msajili wa Hazina (Treasury Registrar) akiwa na asilimia 50.
Kwa upande wa Tanzania, Dk. Slaa alisema Meremeta ilipewa Hati ya kutimiza masharti (Certificate of Compliance) Oktoba, 1997 lakini akasema kwamba Meremeta ilifilisiwa Uingereza Januari 2006.
Hata hivyo, Dk. Slaa ameeleza kwamba pamoja na kampuni hiyo kufilisiwa nchini Uingereza, hakuna ushahidi kuwa kwa upande wa Tanzania kampuni hiyo imefilisiwa au la kutokana na kutajwa katika marejeo mbalimbali kuwa moja ya makampuni yanayozalisha dhahabu.
Taarifa na takwimu muhimu kuhusu Sekta za Nishati na Madini, ya Julai, 2007, inaonyesha kuwa Meremeta bado inafanya kazi, na inazalisha tani 2.27 za dhahabu. Kama Serikali inasema Meremeta imefilisiwa na mali zake kuhamishiwa TANGOLD hali hii inaelezwa vipi? Taarifa hizi za utata zinaashiria nini? alihoji Dk. Slaa.
Maelezo mengine yanayoibua utata zaidi na ambao Kamati ya Rais inayopitia mikataba ya madini itapata wakati mgumu kuitolea taarifa ni kuhusu Meremeta kudaiwa kuwa ni kampuni iliyoanzishwa kwa lengo la kusaidia JWTZ, Kikosi cha Nyumbu wakati ikiwa imeandikishwa nje ya nchi.
Taarifa ya awali ya wakaguzi waliokagua BoT, Juni 2006, iliibua sakata hilo la Meremeta pamoja na kashfa nyingine lakini haikuweza kufahamika ripoti hiyo ya wakaguzi ilivyoyeyuka na kutoanikwa hadharani kabla ya wakaguzi wengine wa nje kuibua suala la EPA pekee miongoni mwa uchafu mwingi ndani ya BoT na serikalini.
Taarifa hiyo ya wakaguzi ilibainisha kwamba Serikali ilitoa fedha hizo kiasi cha Sh. bilioni 155 kwa njia ya dhamana ya hazina ambayo inatakiwa kulipiwa riba ya asilimia 14.92 kila mwaka lakini hakukuwa na makubaliano yoyote rasmi kati ya Serikali na Meremeta hali inayoibua zaidi utata na kuonyesha hakuna njia yoyote ya kuweza kuzipata fedha hizo.
Ndani ya BoT bado kuna mianya mingi ambayo huenda ikaendelea kuibuka siku hadi siku hususan baada ya Bunge kuonyesha njia kwa kushughulikia sakata la umeme wa dharura uliokabidhiwa kwa kampuni ya Richmond Development LLC ya Marekani, sakata lililosababisha kuanguka kwa mawaziri watatu akiwamo aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
Wakati hayo yote yakiendelea, imefahamika kwamba Kamati ya Rais inayochunguza sekta ya madini, inatarajiwa kukabidhi ripoti yake wiki hii lakini Raia Mwema halikuweza kujua undani wa taarifa hiyo kutokana na usiri mkubwa wa yanayojiri ndani ya kamati hiyo.