Meremeta & TANGOLD Revealed!

ndiyo nimesoma sasa hivi, huu ni usanii wa hali ya juu...tutasikia EPA nazo hela zilitumika na Jeshi. Sasa si am-implicate amiri jeshi mkuu kwa kusema hivyo?---->ex-bosi wake BWM
 

Maneno yangu kuwa kifo cha mwalimu kilikuwa ndio mwanzo wa MWISHO wa chama cha ccm ni wazi sasa yaenda kuwa kweli!

Na pia FAMILIA YA MWALIMU SASA NI AIBU tupu na ile sifa ya familia yao kwisha mbali tangia siku na wao walipoamua kumkumbatia MKAPA!

Makongoro amekongoroka na kukataa kumtoa MKAPA kwenye heshima ya kuwemo ndani ya familia ya NYERERE NA HAPO ndipo MKAPA alipopata nguvu za kuhudhuria kiakao cha ccm kilichokuja na hili changa la macho la KIMAFIA!

Kama familia ya mwalimu wangekubali kumvua MKAPA heshima ya kuwa mwanafamilia wa NYERERE basi hata wana ccm wazalendo wangepata nguvu.

Walikataa kufanya hivyo na ndio maana nikasema ccm ILIKUFA SIKU WWALIMU ALIPOKUFA...Kwani kama angekuwa hai basi asingekubali MKAPA AENDELE KUWA NDANI YA FAMILIA YAKE.
 
inavyonikera mimi hii ccm ni kuwa imekosa heshima hata kwa wanachama wake wenyewe waliowachagua.
viongozi wanaoweza kuwavunjia heshima waliowachaguwa kwa kuwaona wanaweza kupokea uongo wa waina yoyote, sidhani kama wanashindwa kufanya maovu mengine yoyote.
hapa walipofikia, viongozi wa ccm wanaweza kufanya jengne lolote, baya zaidi ya hilo, na wasishtuke wala kujali.
 

Hawajui kuwa Muda umewadia. Huwezi kumbana mtu kwenye ukuta siku zote, kuna siku ata-Retaliate, and use whatever means necessary.
 
Hawajui kuwa Muda umewadia. Huwezi kumbana mtu kwenye ukuta siku zote, kuna siku ata-Retaliate, and use whatever means necessary.

Hawa wantuprovek kweli nakwambia....... wamesahau watoto wa pale msikiti wa mwembe
chai magomeni walivowasumbua..........
 
Na Huu Ni Ujumbe Kwa Kina Makongoro,butiku Na Vituko Wengine...kuwa Na Nyie Si Kitu Tena Machoni Petu Wazalendo!
Tena Hata Mwalimu Hana Mpango Tena!
Hilo Jina La Baba Wa Taifa Nyie Mamluki Wa UFISADI YAle Aliyokuwa Akiyapinga Mmepelekea Kuporomosha Umaarufu Wake Na Ndio Maana Hata Huo Mfuko Wa Foundation Wa Butiku Ulikuwa Kapa!
Mnaaibisha!
Mlimpeleka Mkapa Kaburini Kwa Mwalimu Kutambika?
Familia Ya Mwalimu Wanaomkumbatia Makapa Wameidhalilisha Historia Si Tu Ya Tanzania Na Wananchi Wake...bali Mwalimu Mwenyewe!
pamoja na UTU na UBINADAMU!
 
Hawa jamaa ni wasanii. Hakuna jipya hata aje nani. Maana haiwezekani wewe mtu mmoja hata ukiwa malaika huweze kufanya mambo yako kwenye mstari. Pinda hata awe makini vipi watu waliomzunguka ndiyo uleule uozo unategemea nini? Tunaitaji mabadiliko na yawe kote kuoanzia juu hadi chini.

Hivi hawa jamaa hawajui kuwa hili jeshi ambalo wanasema ni usalama wa nchi hela zake ni kodi tunazokatwa kila mwezi then leo mtu anakwambia ni siri! Angalia mambo yao siri hizi mpaka kwenye kununua vitu vibovu Helicopta juzi imeua hawataki kutoa tamko kuwa ni kati ya zile za kifisadi.

Pinda lazima atoe majibu ya kueleweka hii ni aibu kuwa na mzazi anayeongea takataka kwenye chombo kikubwa cha bunge inabidi na familia ziwatenge hawa jamaa maana wanateketeza kizazi kwa kuendekeza matumbo.
 
yaani unapelekwa sehemu ambayo sio yako

Nimekuelewa mkuu...... kuna mengi sana utayasikia toka kwa Pinda. Sidhani kama ni vizuri kukumbushia walichosema watu hapa wakati Pinda ameteuliwa kuwa PM ila kwa mbali sasa inaanza kuonekana.
 
Kama MKAPA BADO ANATAMBULIWA KUWA NI MWANAFAMILIA WA NYERERE LICHA YA KUIUZA NCHI THEN KWANINI TUSISEME MWALIMU NDIYE ALIMTUMA KUFANYA HIVYO NA TO HELL WITH MWALIMU KWANI NA YEYE NI FISADI(MUNGU AENDELEE KUMLAZA PEMA PEPONI)
Kama mwalimu hakuwa fisadi then kwanini alimchagua MKAPA NA YEYE AKAUZA NCHI KAMA MWANAFAMILIA WA NYERERE?
KUSEMA FAMILIA YA NYERERE NA ccm YAO INAYOELEKEA UKINGONI NI MAFISADI NA HATA HAWANA SIFA YA KUWA WANAMAPINDUZI WA TANZANIA MTAKATAA?
 
Brief Details of Mereremeta
Kwa mujibu wa serikali Mereremeta ilifantiwa Usajiri August 19 mwaka 1997,siku ya Jumanne na ilipewa Usjili wa No.registration No. 3424504.

Kwa mujibu wa Taarifa aliyotoa Dr. slaa,Kampuni hiyo ilifanyiwa Usajili October 3 mwaka 1997,ambayo ilikuwa siku ya Ijumma kama Leona lilipewa numbeer ya usajili Certificate of Compliance No.32755.


The reasons for the formation of offshore firms are
1.privacy,
2.asset protection
3. tax savings
4. lawsuit protection
5.flexible business laws
6.Confidentiality


KWa mujibu wa Mkono akihojiwa na Gazeti la Mwananchi alisema Kwamba Serikali imekuwa ikisitita kusema Mmiliki waMeremeta ambaye amechukua pesa nyingi ya Walipa Kodi.Na akiongea na Gazeti la Citizen alisema haya
"I have evidence that this ghost company pocketed a total of Sh181 billion and yet nobody wants to speak about it."


Kama Pinda Kasema anasema Mereremeta ni Kampuni ya Jeshi,

Na kwa kuwa Mheshimiwa Mkono alinukuliwa na Gazeti la The citizen kwamba anafahamu kampuni hiyo ilichukua billioni 181.

Na kwa kuwa hauwezi kufahamu kampuni ilichukua pesa nyingi bila kumjua aliyepewa,Basi Mkono anamfahamu aliyelipwa pesa za Meremeta.

Mkono,Yes I saidTuambie Nani ni mmiliki wa Meremeta sababu unamjua?
 
Hayo majibu yote ni POYOYO za kuwafanya WADANGANYIKA wazidi kukaliwa na wachache vichwani LAKINI tunadhani hatuna mtu wa kutuwakilisha sisi WANYONGE kwani tuliyekuwa TUNAMTEGEMEA ndiyo katoa MAJIBU anayoyaita MAKINI !!!!!! LAKINI HATA HIVYO TUTAFIKA HATA KAMA IKIWEZEKANA KU................................, mwisho wa siku ndio utakaotoa MAAMUZI MBADALA !!!!!!
 
Kama MKAPA BADO ANATAMBULIWA KUWA NI MWANAFAMILIA WA NYERERE LICHA YA KUIUZA NCHI THEN KWANINI TUSISEME MWALIMU NDIYE ALIMTUMA KUFANYA HIVYO NA TO HELL WITH MWALIMU KWANI NA YEYE NI FISADI(MUNGU AENDELEE KUMLAZA PEMA PEPONI)
Kama mwalimu hakuwa fisadi then kwanini alimchagua MKAPA NA YEYE AKAUZA NCHI KAMA MWANAFAMILIA WA NYERERE?
KUSEMA FAMILIA YA NYERERE NA ccm YAO INAYOELEKEA UKINGONI NI MAFISADI NA HATA HAWANA SIFA YA KUWA WANAMAPINDUZI WA TANZANIA MTAKATAA?
 

Huyu Pinda naye ana mawazo mufilisi. Tangu lini jeshi likajishughulisha na mambo ya madini? Ni nani aliyeamua jeshi lijishughulishe na madini? Kwa mslahi ya nani? Hawa mafisadi waliamua kulitumia jeshi labda wakijua Watanzania tukisikia jeshi limehusika basi tutaogopa kuhoji madudu yote yanayohusika na Meremeta. Si ajabu katika madudu ya meremeta hawa wakuu wa jeshi wa sasa na waliostaafu walihusika na ufisadi huo ili wayafumbie macho madudu yaliyotokea.

Watanzania tunataka majibu yanayoeleweka, tumechoka kuibiwa mchana kweupe na mafisadi wanaojivisha ngozi ya uongozi ili waendelee kutuibia Watanzania huku wao wakiwa matajiri wa kupindukia wakati Watanzania walio wengi kila kona ya nchi wakiishi maisha ya dhiki kubwa. Kama hamna maelezo ya kuturidhisha Watanzania na pia kuwafungulia mashtaka wahusika wote wa EPA, Richmond, mikataba ya madini, Kiwira n.k. basi serikali ni bora ijiuzulu na tufanye uchaguzi mwingine.

Hakuna sababu yoyote ya kuendelea kuwa na serikali madarakani ambayo inaonyesha kabisa kwamba imeshindwa kutetea maslahi ya Tanzania na Watanzania.

Kama Mzee Rukhsa aliweza kujiuzulu kufuatia mauaji yaliyotokea Shinyanga wakati akiwa waziri wa mambo ya ndani, basi wewe Pinda na JK na serikali yake yote mnaweza na mnatakiwa mjiuzulu kwa kushindwa kutetea maslahi ya Watanzania. Tumechoka na kauli zenu za ubabaishaji.

Alutta Continua!
 
Jamani we are done. We are finished!!! There is no more hope!!

Pinda amechanganya mambo kiasi ambacho conclusion ni kuwa huyu mtu haelewi bunge ni nini??? Yaani hela ziibiwe wewe useme ni Ulinzi na Usalama??? Kwani Bunge si linapitisha bajeti za Jeshi, Usalama, Polisi blah blah?? Sasa hiyo ni reason kweli??

Halafu EPA amesema labda watadai waongezewe muda, muda wa nini???

Ama kweli nimeweka manyanga chini na kuanzia leo nitakuwa nasoma mambo ya bunge kama Ze Comedy.

May God Bless Us All
 
Well.. tukubali yaishe? je tumezugwa tukazugika...? je tuwazirie nchi kwa sababu wanataka hivyo?

Inachosha na kusikitisha! Ila yana mwisho haya! Hata falme na dola kubwa duniani zilifika mahali zikaanguka!
 

Magwiji ehe!! Tafadhalini sana tena sana acheni kumwita huyu jambazi na fisadi namba moja muungwana!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…