Menu Double Tree au Sea Cliff

jembelamkono

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
2,733
2,011
Habari zenu wakuu,

Leo jioni nategemea kuwa na ugeni mzito kwangu,nimepanga niwatoe dinner kwenye moja ya hotel nzuri hapa Dar.

Binafsi nimefkiria Double tree by Hilton au Sea cliff, sina uzoefu na hotel hizi,ningependa mwenye uzoefu anifahamishe ni ipi kati ya hizi naweza pata chakula na vinywaji kwa bei angalau kidogo.

Pia si vibaya kama kuna anaefahamu sehemu nyingine ambayo naweza pata huduma ya vinywaji na chakula kwa bei nzuri pia tofauti na hizi mbili.

Ahsanteni.
 
Slipway pako vizuri pia, ni jirani na Double Tree Hilton
 
Kuhusu Double Tree ningekushauri umtafute Le super humble man,yeye nadhani anahusika pale kwa njia moja au nyingine,atakupa mwongozo.
 
Kama wageni Wako siyo waroho basi tenga elfu hamsini na tano shs za kitanzania kwa kichwa.
 
Habari zenu wakuu,

Leo jioni nategemea kuwa na ugeni mzito kwangu,nimepanga niwatoe dinner kwenye moja ya hotel nzuri hapa Dar.

Binafsi nimefkiria Double tree by Hilton au Sea cliff, sina uzoefu na hotel hizi,ningependa mwenye uzoefu anifahamishe ni ipi kati ya hizi naweza pata chakula na vinywaji kwa bei angalau kidogo.

Pia si vibaya kama kuna anaefahamu sehemu nyingine ambayo naweza pata huduma ya vinywaji na chakula kwa bei nzuri pia tofauti na hizi mbili.

Ahsanteni.

Nenda nao Alcove, haidary plaza you wont be disapointed.

Restaurant nzuri ilikuwa ya southern sun hotel ila cku hizi uswahili umekuwa mwingi
 
Masanja wali nyama panakufaa maana we ela huna ungekuwa nayo usingeuliza
 
Nenda nao Alcove, haidary plaza you wont be disapointed.

Restaurant nzuri ilikuwa ya southern sun hotel ila cku hizi uswahili umekuwa mwingi
Alcove ilikuwaga kitambo mkuu, sijui kama ipo na inatoa huduma
 
Mkuu unataka uwapeleke hayo maeneo then unakuja kuomba upewe muongozo wa bei hapa???
Bei zinatofautiana kulingana Na aina ya vyakula Na vinywaji watavyotumia!
Kama umeamua weka bajeti ya maana!
 
Nenda koko beach kuna mihogo ya kutosha nabmishikaki ya bukubuku, pande moja la mhogo lazima mgeni aombe poo! Usicheze na manleta skulanta
 
Back
Top Bottom