Mengi: Natishwa

Mpanzi

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
785
500
382_mengi.jpg

MFANYABIASHARA maarufu nchini, Reginald Mengi, inadaiwa, ni kati ya watu wanaotishwa kutokana na sakata la fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow, lililomalizika bungeni wiki iliyopita.

Alipotafutwa wiki hii, kuhusiana na madai hayo ya vitisho, Mengi, katika mazungumzo ya simu na Raia Mwema, alisema kwa kifupi: "Mimi nimemwachia Mungu masuala yote ya usalama na uhai wangu".
Mengi anaelezwa kuwa hatarini kwa maelezo kwamba alifadhili wabunge waliokuwa wakishinikiza kung'olewa kwa watendaji wa Serikali na wanasiasa, wanaotajwa kuhusika na kashfa hiyo.

"Mengi ana mawili. Moja anadaiwa kuwafadhili akina Sendeka (Christopher ole) ili wawe mwiba kwa Serikali. Pili, vyombo vyake vya elektroniki vilikuwa vikiripoti sana mambo hayo. Sasa haya ni mambo yanayomkabili," kilisema chanzo cha gazeti hili.

Wengine, pamoja na Mengi, ambao kwa nyakati tofauti wameliambia Raia Mwema kuwa nao wanatishwa ni pamoja na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila; Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe; Mbunge wa Simanjiro, ole Sendeka na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono.
Wanasiasa na wafanyabiashara hao wanadaiwa sasa kuwindwa na watu ambao wanaelezwa kutofurahishwa na namna walivyosababisha suala hilo kudakwa na vyombo vya habari na umma kiasi cha kuiweka Serikali katika wakati mgumu.

Wakati Kafulila tayari ametoa taarifa katika Jeshi la Polisi kuhusu kutishiwa maisha, Mkono amedai kulishwa sumu wakati akiwa katika ziara ya kibunge nchini Uingereza mwezi uliopita.

Ole Sendeka, mmoja wa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayefahamka kuwa na tofauti kubwa na uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini wa Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wake, Eliakim Maswi, na ambaye yuko karibu sana na Mengi, amedaiwa pia kuwekwa kwenye orodha ya watu walio hatarini.

Alipohojiwa na gazeti hili kuhusu vitisho anavyopokea kutokana na msimamo wake kwenye sakata la escrow, Kafulila alisema yeye alianza kutishiwa maisha tangu alipoanza kupigia kelele suala la mabilioni ya escrow mwanzoni mwa mwaka huu na kwamba hata maisha yake yamebadilika.
Wakati wa Mkutano wa Bunge uliomalizika mjini Dodoma wiki iliyopita, Kafulila anasema alikwenda kushitaki Jeshi la Polisi kutokana na meseji za kutisha alizokuwa akitumiwa kupitia simu yake ya mkononi na watu wasiofahamika.

Katika mazungumzo yake na gazeti hili juzi Jumatatu jioni, Zitto alikiri kufahamu kuhusu hatari inayowakabili na akasema wakati wa Bunge lililopita, hakuwa akila popote zaidi ya nyumbani kwake ambapo dada yake ndiye aliyekuwa akimpikia.

"Nafahamu ni kwa kiasi gani watu walikuwa wakichukizwa na msimamo uliokuwa ukionyeshwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ((PAC) na baadhi ya wabunge na ndiyo maana sasa wako makini kuliko wakati mwingine wowote ule," alisema Zitto.

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma tayari limekiri kupokea taarifa za kutishwa kwa baadhi ya wanasiasa hao na limekiri kwamba linachunguza taarifa hizi.
Tayari Polisi mkoani Dodoma inadaiwa kumshikilia mtu mmoja ambaye hajatajwa jina kwa madai kwamba alikwenda mkoani humo kuwadhuru baadhi ya wabunge.

Taarifa za vitisho dhidi ya Mengi na wanasiasa hao zinaibua hofu kwamba huenda makundi yenye mrengo wa kimafia yameanza kujitanua hapa nchini katika siku za karibuni.

Tayari kuna matukio ya waandishi wa habari na wana harakati kuteswa vibaya kwa kung'olewa kucha na unyama mwingine baada ya kuonekana kuingilia maslahi ya makundi fulani ya watu wenye nguvu na ushawishi hapa nchini.

Chanzo:raiamwema

My take
Hii ni mara ya nne mzee wetu huyu kudai maisha yake yako hatarini. Mara ya kwanza wakati akiwa katika mzozo na wamiliki wa DTV, mara ya pili wakati wa Sakata la ufisadi na mara ya tatu wakati alipogombana na Waziri kijana ambaye hakumtaja.

Serikali impe ulinzi mzee wetu.
 
MTENGETI

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,420
2,000
Wanamtisha kwa kuwa kwa mara ya kwanza bunge lieonyeshwa kupitia itv mhongo kuthibitisha ni muongo? Mbona mim nilionyesha live kupitia ramli? Waje wantishe basi cha moto wakione
 
Ben Saanane

JF-Expert Member
Jan 18, 2007
14,592
2,000
Sijawahi kuona serikali yoyote makini ambayo ni adui kwa wawekezaji wazawa kama serikali ya Tanzania

Mzee Mengi ametukanwa na kudhalilishwa sana na baadhi ya watu wenye dhamana serikalini huku wakilinda kuwanyenyekea wageni.Haiwezekani hata kidogo

Pia ikifikia hatua Mwenyekiti wa Bunge la katiba ambaye ni waziri anatishia ITV kwa kutekeleza wajibu wake ujue kuna serious hostility dhidi ya mmiliki wake
 
Mzee_Wa_Conspiracy

JF-Expert Member
Nov 28, 2014
668
500
Inawezekana kweli maisha yake yapo hatarini, Jamaa amewatapeli watu ardhi zao unategemea nini? Mengi ni mwizi, tapeli na fisadi. yule yumo katika kashfa ya "looting" kule arusha yeye na mdogo wake.

Kwa mujibu wa gazeti la Raia Mwema, Reginald Mengi anasema maisha yake yako hatarini, hii ni mara ya nne mzee wetu huyu kudai maisha yake yako hatarini, mara ya kwanza wakati akiwa katika mzozo na wamiliki wa DTV, mara ya pili wakati wa Sakata la ufisadi na mara ya tatu wakati alipogombana na Waziri kijana ambaye hakumtaja, serikali impe ulinzi mzee wetu.
 
Gagnija

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
9,260
2,000
Sijawahi kuona serikali yoyote makini ambayo ni adui kwa wawekezaji wazawa kama serikali ya Tanzania

Mzee Mengi ametukanwa na kudhalilishwa sana na baadhi ya watu wenye dhamana serikalini huku wakilinda kuwanyenyekea wageni.Haiwezekani hata kidogo

Pia ikifikia hatua Mwenyekiti wa Bunge la katiba ambaye ni waziri anatishia ITV kwa kutekeleza wajibu wake ujue kuna serious hostility dhidi ya mmiliki wake
Wageni wenyewe ndio hawa kina Harbinder.
 
MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,927

Mengi anaponzwa na tamaa zake na ubinafsi uliopitiliza.

Anataka watanzania tuumuunge mkono kila akiwa na ugomvi wake binafsi.

Suala la vitalu vya gesi Prof. Muhongo alishalitolea ufafanuzi wa kina kabisa, kuwa hakuna Mtanzania aliyenyimwa kumiliki vitalu, ila wafuate utaratibu wa kununua hisa TPDC.

Mengi ni mnafiki sana!
 
kbosho

JF-Expert Member
Jun 4, 2012
13,017

you nailed.
 
Waziri mwenye dhamana anapodai kuwa wawekezaji wa Tanzania hawana uwezo wa kuwekeza kwenye gesi hivyo wawekeze kwenye juice ,Matunda na Maandazi unalichukuliaje?
 
Nkoboiboi

JF-Expert Member
Oct 9, 2010
243
195
Kwa mujibu wa gazeti la Raia Mwema, Reginald Mengi anasema maisha yake yako hatarini.

Hii ni mara ya nne mzee wetu huyu kudai maisha yake yako hatarini. Mara ya kwanza wakati akiwa katika mzozo na wamiliki wa DTV, mara ya pili wakati wa Sakata la ufisadi na mara ya tatu wakati alipogombana na Waziri kijana ambaye hakumtaja.

Serikali impe ulinzi mzee wetu.

ZABURI 91:10-11... Atamlinda tu haitaji ulinzi wa mafisadi
 
Mdondoaji

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
5,108
1,225
Sijawahi kuona serikali yoyote makini ambayo ni adui kwa wawekezaji wazawa kama serikali ya Tanzania

Mzee Mengi ametukanwa na kudhalilishwa sana na baadhi ya watu wenye dhamana serikalini huku wakilinda kuwanyenyekea wageni.Haiwezekani hata kidogo

Pia ikifikia hatua Mwenyekiti wa Bunge la katiba ambaye ni waziri anatishia ITV kwa kutekeleza wajibu wake ujue kuna serious hostility dhidi ya mmiliki wake

Mengi is an attention seeker angelikuwa anatishiwa tusingelikuwa tunapishana nae mjini free kabisa bila ya hata body guard? Angelikuwa anahofia maisha yake tusingelikuwa tunapigana vikumbo katika kumbi za starehe tuache hizi dirty politics jamani kama anatishwa aombe ulinzi wa serikali tutamwelewa he is serious.
 
MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,927
2,000
Iringa kwetu hakuna waarabu mbaya zaidi wezi. Hakuna nabisha, Lukuvi mwenyewe na wasiwasi nae kama ni mzawa wa huko kwetu.

Acha ubaguzi wa rangi, dunia sasa ni kijiji, ndio maana hata Marekani rais wake ni mweusi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom