Meneja mkuu wa UDA akutana na waandishi wa habari ukumbi wa maelezo

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
Meneja Mkuu wa shirika la usafiri UDA ndugu Victor Milanzi anazungumza na waandishi wa habari leo kueleza kile anachojua kuhusu tuhuma za Meyor wa jiji ndugu Masaburi yeyote aliyepo karibu na ukumbi wa maelezo tunaomba kutujuza.
 
ni bora na yeye ajieleze kwani meya kamtangaza bila kukutana naye, kulikoni mbona UDA iko chini ya wizara ya uchukuzi na sio chini ya meya ... kapata wapi mamlaka hayo badala ya waziri husika?
 
Hayo maelezo kwa nini asiyatoe kwa tume inayomchunguza badala ya kuwapa waandishi wa habari? Waandishi wa habari wana uwezo wa kumrudisha kazini?
 
Aanatapatapa tu huyo Victor Millanzi ni mfujaji ambaye hana mfano. Muulizeni yeye amewezaje kumiliki ghorofa huko Madale na gari aina ya Prado kwa mshahara gani au kwa vyanzo gani vya biashara alivyonavyo.
 
Humjui Milanzi acha porojo zako
 
Wameshaiua UDA hivi hivi tukiona!hembu fikiri uda kuuzwa kwa 200m ni sawa?wana yard pale bandarini,ubungo bus terminal licha ya magari
 
ni bora na yeye ajieleze kwani meya kamtangaza bila kukutana naye, kulikoni mbona UDA iko chini ya wizara ya uchukuzi na sio chini ya meya ... kapata wapi mamlaka hayo badala ya waziri husika?

UDA inamilikiwa na wabia watatu

1. Simon Agency 52%
2. Serikali/Msajili wa Hazina
3. Halimashauri ya Jiji la Dar
 
Hebu tuwe positive thinkers, meneja kumiliki ghorofa na prado nayo ni issue? Huo ni uvivu wa kufikiri na kufanya kazi. Issue hapa ni ufisadi wake uwekwe mezani, vinginevyo tunakuwa na wivu mzee Mkapa sikumbuki aliuitaje.
 
Mjenda Chilo nimefurahi umeliona hilo.

Mbona watu wanaendesha ma-Prado kwa hela ya mshahara tu sasa iwe Meneja Mkuu!

Acha Milanzi nae aongee waumbuane tujue mbaya wetu ni nani
 
ningejua nisingefungua hii thread.. Mimi nilijua anaengelea strategies za kupanua na kuimarisha kampuni kumbe wanaongelea pesa walizoiba .. Wtf!!!
 
namsubiri akishaongea tuleteen nyuzi na sie tumkaange atueleze mali zake amezipata wapi na kwa mshahra gani na aeleze kila transantion aliokuw akiagizwa na mh iddi simba amezifanyia nini mpuuzi wa haja huyo
 
Pdidy kipi muhimu kwetu?

Sh 200m alizoiba Milanzi au shirika kuuzwa kwa bei chee???

Nitairudia hii thread hata kama ni kesho
 
ni bora na yeye ajieleze kwani meya kamtangaza bila kukutana naye, kulikoni mbona UDA iko chini ya wizara ya uchukuzi na sio chini ya meya ... kapata wapi mamlaka hayo badala ya waziri husika?

Halimashauri ya jiji ni wamiliki wa UDA yaani kama kumbukumbu zangu zitakuwa sahihi, share zao ni kama 51 so ndo maana Mstahiki mayor wa jiji anaonyesha ubavu...
 
Real Man kama wewe ni mpambe Wa Milanzi basi ujue wote mumekwisha kwani kipindi cha kuchezea nauli zetu za daladala kwa ajili ya kujinufaisha wenyewe kimekwisha.
 
Mbona wana JF mumepotea? Tupeni basi yaliyojiri huko Maelezo kuhusu kashfa hii! Wanasiasa kikawaida ndiyo wenye ukumbi Wa maelezo kwa ajili ya kujinadi. Kwa hiyo unapoona Mtendaji wa Kampuni anaenda huko ujue kuna walakini
 
Hebu tuwe positive thinkers, meneja kumiliki ghorofa na prado nayo ni issue? Huo ni uvivu wa kufikiri na kufanya kazi. Issue hapa ni ufisadi wake uwekwe mezani, vinginevyo tunakuwa na wivu mzee Mkapa sikumbuki aliuitaje.
Naona wewe Mjenda Chillo wewe ndiyo siyo positive thinker kwa sababu unadandia basi kwa mlango wa mbele. Kumiliki ghorofa siyo tatizo tatizo ni kuimiliki kwa kipindi hicho hicho ambapo una upotevu Wa sh Milioni 200 Mali ya shirika. Na tunachotaka ni kwamba afanye marejesho ya jinsi alivyo pata hiyo raslimali
 
Back
Top Bottom