Meneja Ahmed Ally afafanua Simba kufanya majaribio

Nyie mnafikaga wapi?

mbona kuna kolo mwenzio anasema eti shibubu ndio mrithi wa chama
sisi tuna mechi tunayosubiri ya kimataifa tuambie nye kimataifa mnasubiri kucheza na Nani? Naomba ratiba zenu za kimataifa
 
Tukija kwenye ukweli hamna club yenye scouting kama yanga bongo Anza kwa job,fei, yassin, chibada hadi kina kagere
Fei Toto alisajiliwa na Singida utd,hamkuwa na FaRaNgA za kumsajili Fri,Bali mfia timu yenu aliwapa,Ni wapi mlimfanyia scouting Fei, achana na blaablaaa.
 
ongezea akina sarpong, sibomana, bigirimana, yikpe, kindoki, bila kumsahau fiston abdulrazak
wamesahau Juma Balinya,walimfanyia scauting na kwa mbwembwe nyingi akaja kutambulishwa kwenye tamasha Lao la KuBwA KuLiKo.Baada ya miezi isiyozidi mitatu.......
 
Anaandika Msemaji Mstaarabu Ahmed Ally katika kurasa ya Instagram

Ni kweli tuna wachezaji watatu tunawafanyia majaribio

Mashabiki wa Simba wamepata hofu kwanini timu yao na ukubwa wao wanafanya majaribio??

Kwanza kabla ya yote niwaambie tuu Wachezaji ambao sisi tunawafanyia majaribio wakienda timu yoyote ya hapa Africa Mashariki watapewa hadi unahodha

Au ingekua wale wengine wangelala Airport kuwasubiri lakini kwa ukubwa wa Simba tukasema hapana njoeni tujiridhishe kiufundi

Sisi hatusajili mtu kwa sababu tuu alifunga goli la Tiktaka

Majaribio ni aina ya mfumo wa Usajili unaokubalika duniani kote na yanampa fursa Mwalimu kumuangalia mchezaji kwa jicho lake mwenyewe (Naked Eye)

Kupitia majaribio Mwalimu anamfanyia tathimini mchezaji kwa kuangalia vitu muhimu kama vile Akili ya mchezaji (Mental health) , Ufundi (Technical) , mbinu ( Tactical) Presha ( Temperament) nguvu (Physic) nini anafanya akiwa na mpira na nini anafanya akiwa hana mpira (With or without a ball)

Vyote hivi huwezi kuvipata kwa kuangalia YouTube au kuhadithiwa na Wakala

Lakini kama haitoshi Majaribio pia yanampa fursa mchezaji mwenyewe kusoma mazingira ya klabu husika Ili aone kama anaweza kufanya kazi hapo au la

Wapo wachezaji wanaosajiliwa moja kwa moja na bado wamefeli hivyo kumnunua mchezaji hai gurentee atafanya vizur na unaemchukua kwa majaribio haina maana hajui Boli

Wana Simba tusiwe na presha na katika hawa ambao wapo kwenye Majaribio hakuna ambae atasajiliwa bila maagizo ya Mwalimu na kwa utaalamu wa Mwalimu wetu akipendekeza mchezaji basi anajua kweli

Tayar tumemuona Sharaf Shibob na Tenena Cheik na leo insha Allah tutamuona Etop David Udoh

Ingekua kusajili mchezaji moja kwa moja ni uhakika Sarpong angekua na top scorer

Tukutane Amaan Stadium tukaishudie timu yetu inatinga Nusu Fainali Inshallah🙏🙏
haka kajamaa tumelamba dume! maneno ya shombo tupu...uto watapata tabu sna
 
Back
Top Bottom