Simba, Ahmed Ally anawasulubu wachezaji na wachezaji wanamsulubu Ahmed Ally, wanasulubiana

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,328
12,625
Mpira unachezwa kichwani kwa mchezaji. Matokeo mabaya uwanjani yanaanzia kichwani na yanarudi na kuishi kichwani kwa mchezaji. Wachezaji hawana kazi nyingine, kazi Yao ni mpira TU na Wana malengo ya kufika mbali kwenye mpira, hivyo hawahitaji vitisho, ahadi nyingi, kejeli, lawama wala kusifiwa sana ili kupata matokeo uwanjani.

Kuna mambo na tabia ambazo zinaweza kusababisha matokeo mabaya kwenye mpira, mionhoni mwao ni:

1. Kushutumu sana na kulaumu wachezaji. Lawama hiwa zinaishi vichwani na miguuni mwa wachezaji kwa muda mrefu.
2. Kusifia sana wachezaji kunasababisha panic anapokosea au kusababisha goli au kucheza vibaya siku hiyo.
3. Kuweka matarajio makubwa sana. Wachezaji wakipewa matarajio makubwa mno ya kufanya vizuri kwenye mechi/mashindano ni sawa kuingia uwanjani kucheza wakiwa na mabegi Yao mgongoni, hawachezi kwa Uhuru na kujiamini.
4. Kuvunja ahadi kwa mchezaji kunarudisha chini jitihada za mchezaji.
5. Malipo madogo kuliko kazi ya mchezaji,
6. Kuingiza tabia mpya na ngeni kwa mchezaji. Kama mchezaji haamini/hajazoea tabia kama ulozi, kuishi kambini, lugha, chakula na tabia ya timu vitasabisha cultural shock kwa mchezaji
6. Kukaa bench kwa muda mrefu
7. Kubadilishiwa Mwl na uongozi unaomjali mchezaji husika.
8. Kutumika mno kila mechi na kila mashindano.
9. Kuumia na ugonjwa (maumivu)
9. Bets: wachezaji au familia au marafiki zao au uongozi wa timu au makampuni ya kubet huwa wanabet (michezo ya kubahatisha) kupata pesa.
kupia matokeo ya timu Yao.
10. Umri mkubwa, umri ukiwa mkubwa hata umfanye nini atacheza hivyohivyo TU.
11. Kocha hafifu

Ahmed Ally anavyozunguuka kuita watu kwenda uwanjani Kuna watia hofu wachezaji ya kupoteza tena mechi na wachezaji wakipoteza mechi wanamtia hofu Ahmed Ally na uongozi mzima, vicious cycle.

Mashabiki wanavutwa na matokeo mazuri sio kispika, wachezaji wenye hofu ya kupata matokeo mabaya ya mechi ya nyuma wanafurahi kucheza mechi yenye mashabiki wachache. Aache kuita mashabiki kuangalia mechi ya wachezaji wanaosemwa na kulaumiwa sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom