Ahmed Ally: Inonga mgeni rasmi kwenye mechi yetu J'mosi

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Simba SC itacheza mchezo wake wa mwisho wa Kundi B wa CAF Champions League dhidi ya Jwaneng Galaxy siku ya Jumamosi ya March 02, 2024 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kuelekea mchezo huo Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally ametangaza kuwa siku hiyo Mgeni rasmi atakuwa Inonga Baka.

“Mgeni rasmi ni Inonga Baka tumeamua kumpa heshima hii kwa sababu ndio Mchezaji pekee ambaye ameipeleka timu yake ya Taifa (Congo) nafasi ya nne kwenye AFCON, kwenye mechi dhidi ya Jwaneng yeye ndio Mchezaji pekee aliyeipeleka timu yake nafasi ya nne”

"Tukishinda mchezo huu [dhidi ya Jwaneng Galaxy] tutakuwa na faida tatu; ya kwanza tumeingia robo fainali ambayo ni maisha yetu ya kila siku, ya pili tumelipa kisasi, na ya tatu tunaingia kwenye historia ya kuwa timu ya tano Afrika yenye kuingia robo fainali mara nne mfululizo." – Afisa Habari Simba SC, Ahmed Ally

Huo ni mchezo muhimu kwa Simba SC kushinda ili kwenda robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
 
Jamaa huwa ana oengo, nadhani watachonga meno yao ili wawe na pengo mwanya kama inonga au wapale carolite.
FB_IMG_1708949811378.jpg
 
Dah shilingi ilitunyima nusu fainali
 
Attachments

  • FB_IMG_17089618746562490.jpg
    FB_IMG_17089618746562490.jpg
    391.5 KB · Views: 2
Simba SC itacheza mchezo wake wa mwisho wa Kundi B wa CAF Champions League dhidi ya Jwaneng Galaxy siku ya Jumamosi ya March 02, 2024 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kuelekea mchezo huo Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally ametangaza kuwa siku hiyo Mgeni rasmi atakuwa Inonga Baka.

“Mgeni rasmi ni Inonga Baka tumeamua kumpa heshima hii kwa sababu ndio Mchezaji pekee ambaye ameipeleka timu yake ya Taifa (Congo) nafasi ya nne kwenye AFCON, kwenye mechi dhidi ya Jwaneng yeye ndio Mchezaji pekee aliyeipeleka timu yake nafasi ya nne”

"Tukishinda mchezo huu [dhidi ya Jwaneng Galaxy] tutakuwa na faida tatu; ya kwanza tumeingia robo fainali ambayo ni maisha yetu ya kila siku, ya pili tumelipa kisasi, na ya tatu tunaingia kwenye historia ya kuwa timu ya tano Afrika yenye kuingia robo fainali mara nne mfululizo." – Afisa Habari Simba SC, Ahmed Ally

Huo ni mchezo muhimu kwa Simba SC kushinda ili kwenda robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Sababu hazina mashiko ila naiombea simba ishinde ili Tanzania iwakilishwe na timu 2 kimataifa
 
Back
Top Bottom