Memorandum of understanding and articles of association

M16_kwaoz

JF-Expert Member
Dec 6, 2017
231
455
Habari wana JF,

Napenda kutoa shukran za dhati kwa msaada wenu katika harakati za kufungua Kampuni haswa kwenye maandalizi ya MOU(MEMORANDUM)na usajili kwa ujumla.Waliotoa maoni ni wengi ila kwa uchache,HARD BODY,RED GIANT NA MBU WA DENGUE wanawakilisha.

Lengo kuu limeshakamilika na sasa kampuni ya YANGUMACHO GROUP LIMITED imeingia mkataba na serikali Kupitia Wizara ya kilimo Kuzalisha mbegu bora za michikichi(TENERA)zipatazo milioni moja katika mkoa wa Kigoma(pia wapo washirika wengine waliomo kwenye mkataba huu ikiwemo FELISA, kila mmoja akiwa na idadi yake ya mbegu).Hii ni utekelaji wa Agizo la Mh. Kassim Majaliwa(Mb),Waziri mkuu JMT la kufufua na kuongeza msukumo wa uzalishaji wa michikichi bora na hivyo kupunguza kiwango cha fedha nchi inazotumia kuingiza mafuta ya mawese kutoka nje ya chi n.k

Karibuni pia kwa wataohitaji. Kampuni ipo mkoani Kigoma(Manispaa Kigoma/Ujiji).
 
Mbegu bora mnazozalisha ukipanda Leo kuanza kuvuna chikichi ni baada ya mda gani?
 
Back
Top Bottom