Membe: Wasiomtakia mema Rais Kikwete wananuna ujio wa Rais Obama!

Kwanini watanzania kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa tunakuwa wanafiki sana, wewe unatembelewa na mgeni, badala ya kumwonyesha hali halisi uliyonayo wewe unajifanya mambo safi huku ukiendelea kuumia. Mmewatoa wauza magazeti, wapiga kiwi, n.k ili iwe nini?
 
Kwani wauza magazeti na wapiga kiwi wanashida gani? Hawa mazuzu wangekuwa na uwezo wangefanya usafi hadi mbuga za wanyama,sijui tuna matatizo gani?!
 
Duh! Viongozi wa Tanzania ni vichekesho vitupu! Hivi waziri mzima unakaa kwenye vyombo vya habari na kuzungumzia mambo ya kuonewa wivu kisa Obama kutembelea Tanzania!!!???? Badala ya kuongelea maendeleo na kuondoa umasikini ambao hawajui ni kwa nini upo Tanzania, wanaongelea mipasho na taarabu kama kawaida!!

Membe! Tunataka habari za maendeleo na si mipasho ya eti raisi wenu anaonewa wivu kisa Obama. Wenzetu wana piga hatua za kimaendeleo nyie mnakaa na kutuletea siasa za vidole juu ambazo hazi saisii lolote!!!

Mpaka maendeleo yakisimama ndio utajua kama ulikua unapiga hatua! Katika mambo ya maendeleo nadhani kiongozi mbovu kuliko wote EAC ni M7.
 
wanashirikisho wengine ndio maana wameanza kutuchoka mapema na kuangalia uwezekano wa kuunda 'kashirikisho' ndani ya shirikisho!

Omujubi,hata kikao cha Uganda wamekifanya kwa timing zao,walijua Kikwete yuko busy na Obama wameamua kufanya kikao chao.
 
Namkumbuka kweli Dr Slaa,Angekuwa Rais wa Tanzania sasa hivi kama si uhuni wa Lipumba wa kuhamishia baadhi ya kura zake kwa Mr Dhaifu pamoja na uhuni wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kushiriki kupora Ushindi wa Dr Slaa.Heshima ya Tanzania ingekuwa imeimarika zaidi kimataifa hasa kwa majirani zetu.Dr Slaa asingekuwa na muda wa kucheka cheka na watu wasioitakia mema Tanzania yetu wala asingekuwa na muda wa kutaka kufanya mambo ili kuwazifurahisha Nchi flani.Chini ya Dr Slaa maslahi ya Wanawanchi na Nchi yangetangulizwa mbele ya jambo lolote lile hasa linapokuja suala la mahusiano na Mataifa mengine.Usalama wa Taifa ungeundwa upya na angewashughulikia wageni wengi walio pata nafasi katika idara nyeti za Serikali na ambao kwa kiasi fulani wanahusika kuweka usalama wa taifa wetu uchi.Kwa ujumla tungeshuhudia uwajibikaji wa hali ya juu ukirejea Serikalini na katika Taasisi na Mashirika yake pamoja na kuongezeka kwa Uzalendo wa Watanzania kwa Taifa lao tofauti na hali ilivyo sasa hivi,Nchi imepoteza kabisa heshima.
 
Wamenuna watuna sana, sisi hatuna muda na kushugulikia eti uchumi, eti reli, kwanza tumemleta wa china, na sasa tunamleta Obama, usisahau kina Bush. na upande wa kinamama hatuko nyuma kuna Booooonge la mkutano, lazima wenzetu wanune sana kwa ujiko wa kimataifa tunaoupata.

- Kwanza nani kati yao nani amepanda mkokoteni wa kuvutwa na farasi? jibu ni hakuna watabaki kununa
- kati yao nani amepanda bembea? jibu ni hakuna watabaki kununa
- kati yao nani ametembelea nchi nyingi zenye nguvu? jibu ni hakuna watabaki kununa

sasa kuwakomesha tumlete kabisa na malkia Elizabeth hapo ndio watapasuka.

RELI, RELI na uchumi kitu gani mbele ya ujio wa Obama? amegoma kwenda kwao amekuja kwetu...

yamewashuka shuuuuuuu......

ila kumbukeni kuna mungu,mi nilijua utampa sifa zote hizo mungu,pity on you
 
ila kumbukeni kuna mungu,mi nilijua utampa sifa zote hizo mungu,pity on you

tumefundishwa mpeni kaisari yaliyo yake na mpeni Mungu yaliyo yake.

nilikuwa najaribu kutafakari kwanini WANANUNA nikaona pengine hizo ni baadhi ya sababu pengine hata na kuwa mwenzao alikwenda FIFA wao hawajafika, mwenzao alialikwa G8 wenyewe hawakuwepo, mwenzao ameonana na meneja wa timu ya waingereza na wao hapana. sababu zinaweza zikawepo nyingi sana...
 
Kazi kweli-kweli!, akili ndogo kuongoza akili kubwa! Maembe ajikombe anavyoweza kwa family member wake jk,urais haupati ng'o!.CCM ijayo ni ya EL, nyie wengine ni washika mapembe tu.
 
Wazir membe amesema wasiomtakia mema rais kikwete wananuna ujio wa obama hapa Mtanzania anaongea clouds fm asubuh hii.

amezungumza akiwa redio ya UNGA? kwa nini huwa hatumii TBCCM? tukimchunguza utakuta nae container la ku GRING mmenielewa?
 
Mheshimiwa waziri ( rais mtarajiwa) alishauri kwa kuepuka usumbufu sasa ukiona kama ushauri haufai, nenda wewe katikati ya jiji jumatatu na jumanne.
........penye bold....sidhani kama upo serious,, kama mh. Membe akipata nafasi hiyo anayoiota, basi tutegemee kutengwa kwa miaka mingine kumi ijayo.
 
Nyoka wa mdimu huyo......kijani tii

RoughGreenSnake.jpg
 
Wazir membe amesema wasiomtakia mema rais kikwete wananuna ujio wa obama hapa Mtanzania anaongea clouds fm asubuh hii.
kama ni kwa manufaa ya Rais tu, tunahaki ya kuchukia lakini kama ni kwa manufaa ya watanzania wote hakuna mtanzania atakayechukia la muhimu ni kuambiwa ni faida gani tutapata?
 
ametumia muda mwingi sana kueleza vipi tutanufaika na ujio wa obama na watu wake,wewe umemsikiliza huyo aliemua kuchukua sentensi moja kati ya nyingi alizoongea membe kama ndio topic aliyokuwa anazungumza,dont you guys have sense of humour???

Alikuja Bush mara kibao. Tena na kukaa TZ kaeibu wiki nzima. Nini tulinufaika nacho kuhusu ujio wake zaidi ya viongozi wetu kujisifia tu??!!!! Kwa taarifa yako manufaa hapangi Obama ndugu yangu. Wapo watu maalum na wenye kauli ya mwishi nini kifanyike wapi.

Usifikiri kuja kwake yapo ya kufaidi zaidi ya wao kuona watavuna wapi rasilimali za MAJUHA. Membe anajua uelewa wa waTanganyika ndio maana anatoa mipasho na vidole juu!!
 
Wazir membe amesema wasiomtakia mema rais kikwete wananuna ujio wa obama hapa Mtanzania anaongea clouds fm asubuh hii.
Hata mimi nakubali; hao vimbelembele na watafuta umashuhuri bandia wanaumia roho sana kwa umashuhuri halisi wa Tanzania. Jeshi la tanzania-JWTZ, ni jeshi mama la ukombozi afrika, hakuna ubishi. Wapigania uhuru wa afrika wote wanajibainisha na tanzania.
Hawa wapigania uhuru bandia kagame na museveni wanajaribu kuipiku tanzania kwa kuanzisha vurugu za kikabila kupata ukuu halafu wanajidai eti ni mashujaa wa ukombozi
 
Wamenuna watuna sana, sisi hatuna muda na kushugulikia eti uchumi, eti reli, kwanza tumemleta wa china, na sasa tunamleta Obama, usisahau kina Bush. na upande wa kinamama hatuko nyuma kuna Booooonge la mkutano, lazima wenzetu wanune sana kwa ujiko wa kimataifa tunaoupata.

- Kwanza nani kati yao nani amepanda mkokoteni wa kuvutwa na farasi? jibu ni hakuna watabaki kununa
- kati yao nani amepanda bembea? jibu ni hakuna watabaki kununa
- kati yao nani ametembelea nchi nyingi zenye nguvu? jibu ni hakuna watabaki kununa

sasa kuwakomesha tumlete kabisa na malkia Elizabeth hapo ndio watapasuka.

RELI, RELI na uchumi kitu gani mbele ya ujio wa Obama? amegoma kwenda kwao amekuja kwetu...

yamewashuka shuuuuuuu......
Mkuu ningekutana na Mwalimu wako wa Kiswahili ningempaita Zawadi. Kwa mafumbo wewe NOMA!.

Wewe chukua nike!.
 
Kumbe hata Membe hafai kuongoza nchi hii...maana kwa kauli hii moja kwa moja hawezi kujadiliana na watawala wa mataifa yenye nguvu kiuchumi kwa ujasiri. Naye anaweza kugawa rasilimali zetu kama njugu kwa wageni.
 
Once a LIBERAL, Always a LIBERAL! Mlitegemea nn zaidi ya mipasho toka kwa hilo kundi la vidole JUU?
 
Back
Top Bottom