JEMEDARI .H.
JF-Expert Member
- Oct 29, 2012
- 341
- 54
Waziri Bernard Membe amesema wasiomtakia mema rais kikwete wananuna ujio wa Raisi wa Marekani Obama hapa Tanzania.
-------------------------
-------------------------
Kwa mujibu wa Benard Membe, viongozi wooote wa East African Community wamealikwa kutokana na ujio wa Obama huku Membe akijaribu kusisitiza kwamba hapo ndipo Kagame anapotakiwa kuja kutoa msimamo wake, bial shaka kutokana na suala la ushauri aliopewa wa kufanya mazungumzo na FDLR!
Aidha, ni kama vile ameshauri wana-Dar es salaam kuangalia upya ratiba zao kipindi ambacho Obama atakuwa Dar kwani ni kama Tanzania/Dar itasimama!!
Source: CLOUDS FM
Leo waziri wa mambo ya nje ametoa kauli tata ikiwa ni mwendelezo wa kauli tata za watawala wa CCM baada ya kuwataka watanzania wasiende DSM kwasasa maana pamejaa. Ameendelea kusema anaomba waende DSM baada ya wageni kuwa wameondoka. Haya ameyasema akiwa anahojiwa na kituo cha habari cha ITV. Nae Kamanda wa kanda maalum DSM Kamanda Kova amewaomba watanzania wawe na ushirikiano na wageni hawa, na kama watasahau vitu kama Laptop, simu na vitu vingine vya thamani amewaomba watanzania wawarudishie.