Membe vs January Makamba

Issue ipi ambayo haijaongelewa hapa kuzuia kuongelewa personalities? Vyote vimefanyika. Issue imeongelewa na personalities zimeongelewa. Just swallow both and accept a different opinion or point of view.
 
bunge la afrika lugha ya mawasiliano ya wazungu.....

Kwa hiyo mwakilishi kutoka Tanzania akikutana na mwakilishi kutoka Ethiopia au Benin wanaongea kiswahili? Lugha ya waafrika?

Narudia hakuna anayepinga kiswahili kutumiwa kinachosemwa hapa ni mwakilishi ajue lugha zote mbili! Kisichoeleweka hapa ni nini?

Kwa hiyo tutafika mahali tutasema sio lazima Waziri Mkuu ajue Kiingereza? Au Waziri wa Mambo ya Nje kama anajua kiswahili inatosha? Tuache kujidanganya kwamba kuongea kiingereza ni ukoloni. Unatakiwa ujue lugha zote mbili kama mwakilishi ili iwe rahisi kujenga mahusiano na kujifunza kutoka kwa wengine.

Mwakilishi wa Benin akikutana na mwakilishi wa Tanzania sasa hivi wanawasiliana vipi?

Ukishaanza kuweka qualifications tu wengine tutasema mwakilishi ni lazima ajue kusoma financial statements na ku balance accounting books, they are supposed to do that a lot. As long as we are adding qualifications, why not?

Sio lazima kumchagua mwakilishi asiyejua Kiingereza, lakini kumnyima a shot at candidacy is at best undemocratic if not a snoberry smacking of cultural inferiority complex.
 
bunge la afrika lugha ya mawasiliano ya wazungu.....

Hakuna mantiki hapo! Angalia bunge la EU uone ni lugha zipi za mawasiliano zinazotumika.

Kwa hiyo mwakilishi kutoka Tanzania akikutana na mwakilishi kutoka Ethiopia au Benin wanaongea kiswahili? Lugha ya waafrika?
Ndiyo. Kwani wewe unadhani hilo haliwezekani?

Narudia hakuna anayepinga kiswahili kutumiwa kinachosemwa hapa ni mwakilishi ajue lugha zote mbili! Kisichoeleweka hapa ni nini?
Ajue lugha zote mbili mojawapo ikiwa ya Kizungu wakati yeye ni mwakilishi kwenye bunge la Afrika. Kwa nini asijue lugha mbili zote za kiafrika?

Kwa hiyo tutafika mahali tutasema sio lazima Waziri Mkuu ajue Kiingereza?

Kwangu mimi ujuzi wa lugha ya Kiingereza kwa waziri wetu mkuu wala si hoja. Kina Lula hao wala hawajui Kiingereza lakini waliweza kufanya kazi kwa ufanisi na kuheshimika duniani. Lula na wenzake walipoenda sijui Norway au Denmark kuwasilisha maombi yao ya Rio kuwa mwenyeji wa mashindano ya Olimpiki 2016 walitumia Kireno na wakashinda!

Au Waziri wa Mambo ya Nje kama anajua kiswahili inatosha? Tuache kujidanganya kwamba kuongea kiingereza ni ukoloni. Unatakiwa ujue lugha zote mbili kama mwakilishi ili iwe rahisi kujenga mahusiano na kujifunza kutoka kwa wengine.
Kwa waziri wa mambo ya nchi za nje ni tofauti kabisa. Angalia karibu nchi zote mawaziri wao wa nchi za nje wanazungumza Kiingereza.
 
Watawasiliana kwa Kiingereza au Kifaransa au Kireno. Hawatawasiliana kwa Kiswahili. Ikitokea wote hawajui hizo lugha za pili au tatu watawasiliana kwa ishara au hawatawasiliana. Siku ambayo lugha ya kiswahili itakuwa imekuwa na kufundishwa nchi nyingine za Afrika basi itatumika kama njia ya mawasiliano na hakutakuwa na sababu ya kutumia hizo lugha nyingine.
 
Issue ipi ambayo haijaongelewa hapa kuzuia kuongelewa personalities? Vyote vimefanyika. Issue imeongelewa na personalities zimeongelewa. Just swallow both and accept a different opinion or point of view.

umeandika

Hapa January tunampa umaarufu wa bure. Ni sawa nianze kujilinganisha na Dr. Slaa au Tundu Lissu eti tuko sawa. Ni uendawazimu tu. Suala ni kujifunza kutoka kwao basi. Huyu yeye atakuwa anatafuta ligi. Uzuri ni kwamba Yanga ikiomba kucheza na Real Madrid wataingia watu wengi sio kuiona Yanga bali Real Madrid na kwa vyovyote Yanga wataneemeka na mapato hata kama watafungwa 7-0! Tumpotezee huyu.

Sasa hapo kuna issue gani kama si ushabiki wa personality contest to rival a shallow exercise at pageantry.
 
Siku ambayo lugha ya kiswahili itakuwa imekuwa na kufundishwa nchi nyingine za Afrika basi itatumika kama njia ya mawasiliano na hakutakuwa na sababu ya kutumia hizo lugha nyingine.

Hiyo siku haitafika kama sisi wazungumzaji wa hiyo lugha hatutaipa umuhimu. Wengine wakituona tunakazana na kukopi lugha za wazungu kwa nini wao wahangaike na kujifunza lugha yetu? Makes no sense.
 
Watawasiliana kwa Kiingereza au Kifaransa au Kireno. Hawatawasiliana kwa Kiswahili. Ikitokea wote hawajui hizo lugha za pili au tatu watawasiliana kwa ishara au hawatawasiliana. Siku ambayo lugha ya kiswahili itakuwa imekuwa na kufundishwa nchi nyingine za Afrika basi itatumika kama njia ya mawasiliano na hakutakuwa na sababu ya kutumia hizo lugha nyingine.

Kwa nini Kifaransa, Kiingereza au Kireno na si Kiswahili ?

Kiswahili hakifundishwi nchi nyingine za Afrika? Dude, unaijua Afrika?
 
Kwa nini Kifaransa etc na si Kiswahili kwa sababu as of now kiswahili hakitumiki Benin bado. Mpaka tukifikia hapo watatumia lugha hizo za pili.

Kuhusu personality....ningependa usome comments za thread nzima na sio post moja ulioinukuu. Ziko post nyingi na issue zimejadiliwa humo. Am replying using my phone and that makes it hard kureproduce.
 
Masahihisho....kiswahili hakifundishwi katika nchi zote za Afrika. Ethiopia na Benin hawajifunzi kiswahili. Ila, ninachosema hapa ni kwamba bado hatujafika mahali kusema wawakilishi wanaweza kuwasiliana nje ya mkutano kwa kiswahili na wakaelewana vizuri. Yeyote atakayeenda kama mwakilishi ni vyema akajua kingereza kama lugha ya pili.
 
Kireno, Kiarabu, Kiingereza na Kifaransa zinafundishwa nchi zote za Afrika ?
 
Kwa nini Kifaransa etc na si Kiswahili kwa sababu as of now kiswahili hakitumiki Benin bado. Mpaka tukifikia hapo watatumia lugha hizo za pili.

Kuhusu personality....ningependa usome comments za thread nzima na sio post moja ulioinukuu. Ziko post nyingi na issue zimejadiliwa humo. Am replying using my phone and that makes it hard kureproduce.

Kiswahili hakitumiki Benin sawa, na Kifaransa hakitumiki Tanzania.

Swali bado lipo pale pale, kwa nini Kifaransa na si Kiswahili?
 
Ninachukia sana mtu anayefikiri kuwa msomi ni yule anayejua kiingereza vizuri. Ni mpuuzi tena kiongozi wa wapuuzi. Umeona siku hizi matoto yetu yanaongea kiingereza vizuri lakini moja jumla moja hayajui.
 
Watu wana inferiority complex sana tu.

George Bernard Shaw, native speaker aliyepata Nobel na Oscar, anakwambia Kiingereza ni lugha isiyo na structure nzuri, maandishi yake hayafanani na matamko. Huyo native speaker anayetambulika kwa literary criticism na scholastic achievement.

Na zaidi ya hapo ina exceptions kibao katika rules zake kiasi cha kufanya rules zisiwe na maana. No wonder watu wenye kuwa na Kiswahili kama lugha ya kwanza wanaona Kiingereza miyayusho.

Kiswahili hakina matatizo hayo, lakini wenyewe tunakidharau na wala hatujui hayo.
 
Kiswahili hakina matatizo hayo, lakini wenyewe tunakidharau na wala hatujui hayo.

Kiswahili kina hatari ya kupotea. Jaribu tu kusikiliza redio za bongo siku hizi. Watu wanachanganya lugha pasipo hata na ulazima. Kwangu hiyo ni kero tupu. Huko tunakoelekea sasa mwishowe itazaliwa lugha mpya yenye mchanganyiko wa Kiswahili na Kiingereza.

Na haya mazoea ya kuchanganya Kiswahili na Kiingereza yametufanya tusizijue lugha zote mbili kwa ufasaha hususan Kiswahili ambacho ni moja ya lugha rahisi sana kujifunza na kuzijua.
 
Wadau tunatake Swaha for granted. Ukiwa DRC, Burundi, Rwanda, Uganda, and South of Southern Sudan, by Uganda border huko kote kama unajua kiswahili haupotei wala haufi njaa. Lazma utakutana na wadau wanajua kiswahili hata kama cha kuunganisha. Halafu wanakwambia kabisa, hicho kiswahili cha Tanzania kigumu sana. One of the disappointing act of Asha Rose Migiro in UN ni haweki mkazo Kiswahili kuwa adopted as official UN language. It is widely spoken kwenye ukanda wa maziwa makuu.

The joke is Swaha was born in TZ, raised in Kenya, died in Uganda, and buried in DRC. The point ni kwamba hizi nchi zote zinaongea Swaha, but with different fluency.
 
mchango wangu ni kwamba tuna lumbana bure,JM alikua anataka masifa ya bure alichoongea ni nonsenses,alichosema Membe ni cha msingi sio kwamba Membe sio patriotic wa nchi yake,
wana Jf lazima mjue kwamba Kanuni za Bunge zina mtaka anae gombea kwenye hilo bunge la Africa zinasema lazima huyo mtu ajieleze kwa ki engeleza,ni bunge hihlo hilo lililo tunga hizo kanuni,alichatakiwa kufanya JM ni ku move motion kanuni zitenguliwe kuliko pompousness ya kueleza aah et nilifanya kazi Ikulu,Mambo ya nje what for sasa, nilifurai Membe kumzima siwezi nika conclude kwamba ni bifu la kujivua gamba ila live alimtuliza
bravo membe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom