Safi sana Mbegu. Lugha yetu ni nzuri sana na nashindwaga kabisa kuelewa kwa nini hatuikuzi na badala yake tunashobokea lugha ya kigeni. Januari alikuwa sawa kabisa na kwa hilo mimi namuunga mkono. Tutaendelea kuathirika na ukoloni mamboleo hadi lini?
Mbegu na NN, nadhani suala pia ni January kutenda anayohubiri. Kwa bahati kidogo nawafahamu wote hawa wawili. Ukiongea nao utaona utofauti mkubwa katika hili suala la Kiswahili vs Kingereza.
Ukiongea na January katika kila maneno 10, saba au zaidi ni kiingereza na wakati mwingine anaenda sentesi mfufulizo bila kuchomeka kiswahili. Kwa uzoefu wangu nimeweza kujua kuwa anafanya hivyo kutegemeana na nani anazungumza naye, na uwezo wa mtu katika lugha.
Ukiongea na Membe katika kila maneno kumi, labda matatu yatakuwa ni kiingereza, na hii ni kwa wote, tangu alipokuwa Canada.
Kwa January kutetea Kiswahili wakati kitabu chake, blog na website zake (
January Makamba.com au
Politics, Society & Things) zinazowalenga wapiga kura wake wa Bumbuli zimeandikwa Kingereza, nadhani ni unafiki wa aina fulani.
Muswada wa Mabadiliko Ya Katiba umeandikwa Kingereza na kusambazwa kwa wananchi, pamoja na wapiga kura wa Bumbuli, waujadili. Kamwe hatukusikia January kuungana na akina Zitto, Lema, Mnyika, UDASA na wengineo waliotaka na bado wanataka kuwa muswada huo uchapishwe kwa Kiswahili kabla ya kuzambazwa kwa wananchi wote. Na serikali ya CCM imegoma kufanya hivyo, na badala yake wanasema wataweka wakalimani.........go figure!!!
Ni nini kimebadilika hadi leo hii January amekuwa mtetezi mkubwa wa Lugha ya Taifa kuliko lugha mbadala iliyopo kwenye kanuni za Bunge?