Membe: Sitogombea Ubunge 2015

Membe: Sitogombea Ubunge 2015

Amehakikishiwa njia nyeupe urais
 
Naona anakwenda kupambana na hasimu wake. Lakini, keshaoteshwa?
 
uchu na uroho wa madaraka, pasipokujua ua pengine wanajua ila hawataki kufanya kile wanachotakiwa walifanyie Taifa.

Membe ni opportunist tu. Anahongeka kirahisi rahisi kama vile alivyohongwa kiwanja huko Arumemru ili amwache mhongaji kwenye madaraka kwenye shirika lililo chini yake. Hana tofauti na kaka yake JK kuhongwa suti.
 
Uzuri wa Lowassa kwa kweli ni determination,kujiamini,kupiga kazi,kusimamia anachoikianzisha,kuwadadabisha walio chini yake,tatizo lake tu ni hilo la kupenda pesa kuliko kitu kingine.

Na hilo ndiyo tatizo kubwa kuliko yote hapa duniani na huko mbinguni ! Note that , hicho ndicho kinachomsukuma kuutaka Urais kwa haki au kwa shari , usimpe kura yako !
 
Hongera kwa kutangaza kupumzika siasa za majimbo.
Ni uamuzi wa busara kuwaachia wengine.
Twasubiri tamko lako kuelekea 2015.
 
mimi kanikera kwenye maelezo yake juu ya GAS anadiriki kuendelea kuwapofusha wanamtwara kuwa gas ni ya watanzania wote, nani? asiyejua hilo kinachotakiwa manufaa yote ya gas hiyo yaanzie MTWARA, kama kuwepo kwa gas hiyo kutawezesha kupatikana viwanda 5, basi cha kwanza kianze kujengwa MTWARA, MH MEMBE maisha yako muda mwingi uko DAR, ndo maana huoni umuhimu wa mikoa ya kusini kupata fursa kama za DAR ili vijana wabaki huko wasitengeneze bomu aliloliona mwenzako LOWASSA. eeeehn wana MTWARA mwenyezi MUNGU awape nini? bahari yenye fukwe nzuri mnayo, bandari yenye kina kirefu mnayo. GAS ,GAS GAS viongozi wenu mliowachagua hawajui muifanyie nini? wenzenu viongozi wao tayari wanajua matumizi yake, kazi yenu mtaoata vibarua vya kuchimba mitaro ya mabomba makubwa kuelekea DAR.
 
[h=2][/h]05/01/2013

781711701.jpg
Bernard Membe
WAZIRI wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ametangaza kuwa hatogomea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.

Membe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi, alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Mwaka Mpya nyumbani kwake.

“Unajua nimekuwa mbunge wenu kwa kipindi cha tatu. Hivi leo ninawaaga rasmi kuwa sitagombea tena nafsi hii ya ubunge,” alisema Membe, ambapo pia aliwataka wananchi wa mikoa ya kusini, kuwa na subira katika kipindi hiki ambapo Serikali inashughulikia mchakato wa kuvuna gesi asilia.

Alisema kuwa ni muhimu kwa wakazi wa mikoa iliyopatikana gesi kutambua kuwa rasilimali zilinazopatikana nchini ni mali ya Watanzania wote na siyo ya mikoa iliyogundulika pekee.

Waziri Membe aliwataka madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, kuacha kutumia vikao vya halmashauri kujadili malumbano yasiyokuwa na msingi akisema kwamba kufanya hivyo ni kipoteza rasilimali za wananchi bila faida.

“Salamu zangu za mwaka mpya ni kuwaomba madiwani kuacha kutumia vikao kuwajadili madiwani wenzenu kwa hoja zisizokuwa na maana, badala yake tujenge umoja na mshikamano ili kufanya kazi za kusimamia miradi ya maendeleo,” alisema Membe.

Waziri Membe alitumia muda huo pia kuwataka madiwani kujipanga katika kusimamia matumizi ya fedha za miradi ya Halmashauri.

Baadhi ya wakazi na viongozi mbalimbali wa CCM na Serikali mikoa ya Lindi na Mtwara walikusanyika jimboni kwa Membe kusherekea kuadhimisha mwaka mpya.

Viongozi walioshiriki katika sherehe hiyo ni pamoja Mbunge wa Mtwara mjini, Hasnain Murji, Godless Kweka ambaye ni Mjumbe wa Nec, wajumbe wa Kamati ya Ulinzi Mkoa wa Lindi ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Ludovick Mwananzila na madiwani pamoja na viongozi wa dini wa mikoa hiyo.

---
via gazeti la MWANANCHI

Source: wavuti.com - wavuti
 
Sasa ni WAZI --- "NITAGOMBEA URAIS nina KAMATI Nzuri NDANI ya NEC-CCM (KIKWETE's FAMILY)"
 
makundi ndo haya mawili tu ama tungojee na mengine? ritz
 
Yaani na Membe awe rais? Hell no. Huenda anataka kuwa mwekezaji kwa vile amechuma sana mafweza.
 
wangepigania na ROHO ZAO hivyo kama wanavyogombea madaraka, MAJANGA YANGEPUNGUA DUNIANI!!!
 
namuunga mkono membe, ni mwanasiasa mwenye uvumilivu wa kisiasa, hana makuu na majivuno kama lowasa
 
Baadae utasikia "wananchi wa jimbo la Mtama wameniomba nichukue fomu ya urais"
 
Dah, naona hizi kambi mbili mganga wao aliwaambia salam za mwaka mpya 2013 ni kuonyesha nia! Haya yetu macho na masikio!
 
05/01/2013

781711701.jpg
Bernard Membe
WAZIRI wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ametangaza kuwa hatogomea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.

Membe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi, alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Mwaka Mpya nyumbani kwake.

“Unajua nimekuwa mbunge wenu kwa kipindi cha tatu. Hivi leo ninawaaga rasmi kuwa sitagombea tena nafsi hii ya ubunge,” alisema Membe, ambapo pia aliwataka wananchi wa mikoa ya kusini, kuwa na subira katika kipindi hiki ambapo Serikali inashughulikia mchakato wa kuvuna gesi asilia.

Alisema kuwa ni muhimu kwa wakazi wa mikoa iliyopatikana gesi kutambua kuwa rasilimali zilinazopatikana nchini ni mali ya Watanzania wote na siyo ya mikoa iliyogundulika pekee.

Waziri Membe aliwataka madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, kuacha kutumia vikao vya halmashauri kujadili malumbano yasiyokuwa na msingi akisema kwamba kufanya hivyo ni kipoteza rasilimali za wananchi bila faida.

“Salamu zangu za mwaka mpya ni kuwaomba madiwani kuacha kutumia vikao kuwajadili madiwani wenzenu kwa hoja zisizokuwa na maana, badala yake tujenge umoja na mshikamano ili kufanya kazi za kusimamia miradi ya maendeleo,” alisema Membe.

Waziri Membe alitumia muda huo pia kuwataka madiwani kujipanga katika kusimamia matumizi ya fedha za miradi ya Halmashauri.

Baadhi ya wakazi na viongozi mbalimbali wa CCM na Serikali mikoa ya Lindi na Mtwara walikusanyika jimboni kwa Membe kusherekea kuadhimisha mwaka mpya.

Viongozi walioshiriki katika sherehe hiyo ni pamoja Mbunge wa Mtwara mjini, Hasnain Murji, Godless Kweka ambaye ni Mjumbe wa Nec, wajumbe wa Kamati ya Ulinzi Mkoa wa Lindi ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Ludovick Mwananzila na madiwani pamoja na viongozi wa dini wa mikoa hiyo.

---
via gazeti la MWANANCHI

Source: wavuti.com - wavuti
ni adui namba one wa taifa la israel. amekuwa waziriri wa mambo ya nje mudawote bila hata kushawishi erikali kufungua ubalozi na ofisi pale tel aviv. hajatembelea israel hata kama kutafuta wawekelezaji. anayaogopa mataifa ya kiarabu kutofanya urafiki na israel eti watanuna. katemelea nchi zote maadui wa israel ila hakutaka kabisaa kukanyaga tel aviv.

sasa mu kama huyu ambaye mataifa ya kiarabu yana influence naye, atafaa kweli kuwa raisi wetu? tena alilaani vibaya sana israel kuwapiga wapalestina katika vita vya operesion shiel! haja laani maroketi ya hamas hata mara moja! hafai kabisaaa kuwa raisi etu bora CCM impatie Nyarandu lazaro!
 
..... Namtakia heri kawtika mambo mengine anayoyatarajia ... natoa wito pia kwa wengine wanaojiona wamechoka watangaze mapema tujue majimbo gani yatakayokuwa wazi...
 
Back
Top Bottom