Membe: Sitogombea Ubunge 2015

Membe: Sitogombea Ubunge 2015

Itafika mahali Tanzania itaongozwa mpaja na Kichaa!
 
Amefanya vizuri kutangaza lakini anatutia hofu maana hakusema baada ya hapo atafanya nini.
 
Nadhani 'AMETANGAZA KUTOKUTANGAZA' namfananisha membe na Mbwa asiye na meno wala kucha,anaota ndoto za mchana.
 
Labda aniloge niwe kichaa ndio atapata kura yangu,gamba gumu lililokataa kuvuka hilo
 
Mbio za Urais zashika kasi. Kila jongoo na mti wake CCM!

He's not a presidential material even by default, Membe.
 
Hapo hakuna wa kupambana na Dr Slaa!!! Aheri aendelee kung'ang'ana na kaubunge kake!!!
 
Siku hizi kuna mambo, naamini hata kichaa anaweza kugombea uraisi kwani mataahira wana mpango wa kuacha kugombea ubunge ambao wameupata tu kwa sababu wanaichi hawana elimu ya uraia, na sio kama kweli wana sifa, ushauri wangu ni kuwa wote wanaoutaka uraisi wapimwe kwanza akili zao
 
Uzuri wa Lowassa kwa kweli ni determination,kujiamini,kupiga kazi,kusimamia anachoikianzisha,kuwadadabisha walio chini yake,tatizo lake tu ni hilo la kupenda pesa kuliko kitu kingine.

Hiyo ni mbinu ya bepari yeyote kuhakikisha anajikusanyia vyovyote awezavyo hata kwa kujionyesha mwema mbele ya wengine. hata iweje mtu huyu hatufai coz mwizi ni mwizi tu haijalishi anaiba kwa staili gani.
 
Huyu jamaa kasoma alama za nyakati anajua he is useless, not electable hata kwenye jimbo. ANAJIHAMI PERIOD! Anaongopa zengwe la Dr. Kitine na ndugu zake Usalama wa Taifa. Hawamtaki at all cost you cannot market an Idiot for the Presidency.
 
Amesahau kitu kimoja kukamilisha sentensi, angesema kama zitto ,hatagombea ubunge,bali atagombea urais mwaka 2015, nadhani lowassa naye atasema...,
 
Hiyo ni mbinu ya bepari yeyote kuhakikisha anajikusanyia vyovyote awezavyo hata kwa kujionyesha mwema mbele ya wengine. hata iweje mtu huyu hatufai coz mwizi ni mwizi tu haijalishi anaiba kwa staili gani.

E.lowasa anang'ang'ana kutoa vimbanzi kwenye macho ya wenzake wakati vya kwake vimemshinda.
 
Benard Membe unayo maswali ambayo Watanzania watahitaji majibu yake kutoka kwako kama unayo dhamira ya kugombea Uraisi ,
1,Ukiwa ni Waziri wa mambo ya nje umeshirikiana na serikali yako kuwadanganya Watanzania kwamba BALALI amekufa na kwenye maombolezo yzke watu wameingia kwa kadi na kuweka rekodi kama si kote duniani kwenye maombolezo watu kuingia na kadi kana kwamba ni sherehe,wakati wanaoingia ni viongozi tu hata ndugu wa marehemu wengine hawakuruhusiwa kuingia,kitu ambacho hata mazishi ya muasisi wa taifa hili haikufanyika hivyo
2, Yule ni kiongozi mwandamizi serikalini [Gavana] kumzika nje ya nchi ilikuwa ni kuficha nini? Na kwanini azikwe nje ya nchi wakati ana kwao na Serikali inaouwezo wa kumrejesha na akazikwa hapa kwao? Serikali ilikuwa inaficha nini?
3,Ulisema unawafahamu walioficha fedha za Tanzania Uswiss kwa majina na kwamba utawataja,mbona hadi leo haujawataja? Unataka tukupe nchi ya Tanzania si utatuuza wote?
4,Ni vipi umelishughulikia suala la mpaka wa Tanzania na Malawi na ni nini hitimisho lake? Wananchi hawajui liko katika hatua gani linatakiwa majibu
Kwa maoni yangu hata kama utajibu hayo maswali wewe ni dhaifu kama kiongozi unaetaka kumrithi haufai kuwa Raisi wa Tanzania kabisa sababu si MUWAZI hatutaki kiongozi wa aina yako hali tuliyonayo tayari tuko ICU halafu tupate tena rais muoga HAUTUFAI
 
daa mzee mwingine wa kuchekacheka anaitaka nchi TUMEKWISHA


Nchi kwa tulikofikia tunahitaji kiongozi mkali,mwenye maono anaejali watu wake na si bora kiongozi wa kuchekacheka na mtu wa taarabu tunahitaji mtu jaairi,enzi ya kuchekacheka na kutoa mipasho haipo tena
 
Hata Edward Lowasa HAUTUFAI kwa sababu wewe na rafiki yako Kikwete mmetutwika mzigo mzito kwa kugeuza Tanesco kitegauchumi chenu na kuendelea kuwanyonya Watanzania kwa bei za ajabu za umeme Ulikuwa unaelewa kila kitu kuwa ile kampuni ilikuwa ya kitapeli lakini ukaibeba wewe na mkuu wa kaya kwa maslahi yenu,sasa hivi unataka Uraisi ili muendeleze mchezo wenu wa kuwafanya Watanzania masikini wa kutupwa nyie mkijitajirisha na raslimali za nchi,Ndio maana mkiulizwa kwanini Watanzania ni masikini mnakosa majibu HAUTUFAI EDWARD LOWASA ngoja tutafute mwingine lakini nyie hapana
 
images

Bernard Membe
Waziri Mambo ya nchi za nje

WAZIRI wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ametangaza kuwa hatogomea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao. Membe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi, alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Mwaka Mpya nyumbani kwake.

  • “Unajua nimekuwa mbunge wenu kwa kipindi cha tatu. Hivi leo ninawaaga rasmi kuwa sitagombea tena nafsi hii ya ubunge,” alisema Membe.
Pia aliwataka wananchi wa mikoa ya kusini, kuwa na subira katika kipindi hiki ambapo Serikali inashughulikia mchakato wa kuvuna gesi asilia.

  • Alisema kuwa ni muhimu kwa wakazi wa mikoa iliyopatikana gesi kutambua kuwa rasilimali zilinazopatikana nchini ni mali ya Watanzania wote na siyo ya mikoa iliyogundulika pekee.

Waziri Membe aliwataka madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, kuacha kutumia vikao vya halmashauri kujadili malumbano yasiyokuwa na msingi akisema kwamba kufanya hivyo ni kipoteza rasilimali za wananchi bila faida. “Salamu zangu za mwaka mpya ni kuwaomba madiwani kuacha kutumia vikao kuwajadili madiwani wenzenu kwa hoja zisizokuwa na maana, badala yake tujenge umoja na mshikamano ili kufanya kazi za kusimamia miradi ya maendeleo,” alisema Membe. Waziri Membe alitumia muda huo pia kuwataka madiwani kujipanga katika kusimamia matumizi ya fedha za miradi ya Halmashauri.

Baadhi ya wakazi na viongozi mbalimbali wa CCM na Serikali mikoa ya Lindi na Mtwara walikusanyika jimboni kwa Membe kusherekea kuadhimisha mwaka mpya. Viongozi walioshiriki katika sherehe hiyo ni pamoja Mbunge wa Mtwara mjini, Hasnain Murji, Godless Kweka ambaye ni Mjumbe wa Nec, wajumbe wa Kamati ya Ulinzi Mkoa wa Lindi ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Ludovick Mwananzila na madiwani pamoja na viongozi wa dini wa mikoa hiyo.
 
Vyama vya upinzani viongeze kasi mikoa ya kusini, maana walioshikilia majimbo wameshaona joto linazidi kupanda na kuamua kutangaza majimbo kubaki wazi kama Membe alivyofanya.
 
Back
Top Bottom