Zuia Sayayi
JF-Expert Member
- Mar 28, 2011
- 841
- 139
:ranger::music:
Nawasalimu wana Jamvi,
Kwa taarifa za wazi na kuthibitisha,Waziri wa mambo ya nje Bwana Benard Membe atagombea Urais.
Katika kikao cha siri ambacho aliwaita wazee wa mtama kuwa yeye ndiye Rais,wanamtama wajiandae kumpokea Mrithi wake ambaye ataliongoza jimbo hilo kwa miaka mitano ijayo.
Akiwa kwenye kikao hicho wazee wa Mtama walimuomba Aeleze mrithi wake,Mheshimiwa Membe alisema" tunayekiongozi bora,atakayenirithi naye ni mwamtama kijana mpenda michezo aliyelitumikia Taifa kimichezo bwana Suleinan Methiew Diwani wa Kata ya Vijibweni"
Uchunguzi uliofanyika,baada ya kuwasiliana na wakaazi wa kata hiyo wakasema,"huyu ni diwani wetu kweli na katika kikao chetu cha kamati ya siasa ametuambia anakwenda kwap Lindi vijijini kugombea Ubunge"
Bwana Mathew amewahi kuichezea timu moja maarufu ya hapa Tanzania.
Uchunguzi wangu ulienda mbali zaidi na kuona kuwa katika kata yake ndio mahala ambapo Chadema ni kama imeifuta CCM.
Katika uchaguzi huo wa Desemba 14, kati ya mitaa mitano iliyokuwa ikiongozwa tangu 1961,CHADEMA imepata mitaa minne na CCM kuambulia mtaa mmoja tu.
Kata yake ya Vijibweni,ni miongoni mwa kata zilizonyuma kimiundombinu na hata shule hazina madawati,vitabu na nyumba za walimu.Hiyu ndiye mrithi wa Bernard Membe aliyemuandaa kuwaletea wanamtama maendeleo endelevu.
Ndio wameanza kucheza zile ngoma zao na wale wanyama waoKwa hiyo membe ana uhakika ccm watampitisha pamoja na kelele zote zinazopigwa siyo?
Labda uraisi wa kisiwa cha Chumbe.