Membe: Ngeleja ni tishio urais 2015

Membe: Ngeleja ni tishio urais 2015

Ukisikia kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa Ndio huku, hapa Naona ni siasa taka za kupata kura za wachunga ngombe
 
tanzania ni nchi ya mizaha mizaha flani hivi!labda rais wa wezi wa escrow...
 
Sengerema tu imemshinda. Hebu orodhesha maendeleo aliyoyafanya hadi leo pale jimboni kwake Sengerema toka awe mbunge. Hebu acha kutia hasira wananchi...
Arudishe kwanza pesa za ESCROW halafu asubiri kitanzi kinakuja....
 
Basi mpeni hata Chenge kama mtaona hivyo. Chenge si mwenyekiti wenu wa kamati ya maadili ya CCM. Nyinyi CCM MNA mambo kweli
 
membe amehusikaje hapo mbona mleta hoja umemtumia mh. Kama toilet paper linalogombaniwa na mende chooni
 
ngeleja huyu huyu aliyekuwa nishati au mwingine?
 
VITA UCHAGUZI 2015


Bado Hali ni tete ndani ya CCM ,Ila Nani atakaye mrithi JK Ipo wazi na nafasi Hii imemwangukia mbunge kijana Mwenye ufanisi na
Haiba ya kuvutiaa mh William Mganga Ngeleja mmbunge wa sengerema kuendana na kasi iliyopo kwa kumteua mwanasiasa huyu kijana mtaalamu wa fani ya sheria .

Kwanini JK atamwachia Mikoba Hii ni kutokana na Kukubalika na wanachama wengi na watanzania wengi kwa ujumla wao ambao wamehaidi kumpigania Mh Ngelejah endapo atasimamishwa kugombea nafasi Hiyo ambayo inaonyesha wazi ndiye mrithi sahihi hivyo watu wa tanzania wajiandae kushirikiana na mh ngeleja katika mqpambano hayo yenye kuleta tija kwa watanzania kwa ujumla

Vilevile uchapakazi wa Mh Ngelejah Unafanya aaminike zaidi ndani ya chama na kwa wananchi kwa ujumla ,ngeleja anaamini katika kujenga uchumi imara Wenye nguvu utakaopambana na umaskini na Rushwa akijikita kwa kuwekeza zaidi kwenye nishati ya Umeme ambayo itachangia uzalishaji mali kwa kasi zaidi, Mifano iliyo wazi kupitia REA ambayo imechangia kusambaza umeme vijijini kwa upana mkubwa.

Kazi ya ujenzi wa barabara, Licha ya kuwa Jk amejitahidi kwa asilimia 65% na amefanya kwa kiwango cha juu na anastahili pongezi kwa barabara nzuri za kiwango cha Lami zenye kupitika, mh Ngelejah anatamani kuona asilimia 100% ya barabara zote zimekamilika miradi yote na barabara zijengwe imara zenye kudumu, hili linawezekana Kama tutakuwa na mfuatiliaji makini ambaye ni Mh Willium Mganga Ngeleja.

Kitu kinachompa nafasi mh Ngeleja ni uwezo wake mkubwa katika ujenzi wa siasa unganishi isiyo na makundi ndani ya wananchi na vyama vyao vya siasa, akiwa mwenye nia njema, mh.Ngeleja anapenda kuyaunganisha Makundi yote na wananchi waote licha ya utofauti wa rika zao katika jamii ili kujenga nchi na kuondoa ubaguzi.

Halikadhalika mh Ngeleja amejitosa kulipambania swala la kuondolewa kwa vikwazo kwa wafanyabiashara na wakulima wadogo wadogo kwa kuwatoza kodi kubwa ukilinganisha na gharama za uzalishaji hali inayopelekea kuwanyonya wakulima wa hali ya chini pamoja na wafanya biashara wadogo wadogo, wakishindwa kulipa ada ya watoto shuleni ,"Lazima tuyalinde masoko ya ndani ili kuweza kumnufaisha mkulima wa hali ya chini kufaidi jasho lake" mh Ngelejah aliyasema hayo wakati akizungumza na wakulima wa mananasi wilayani Sengerema kata ya Nyampulikano ...katika kuwanufaisha wakulima katika masoko ya ndani.

Kuboresha Afya, hili limekuwa changamoto kubwa kwa Kila kiongozi anayetoka madarakani,mh ndiye mtu pekee atakayewezesha kutumiaa rasilimali zetu kunufaisha wananchi wote kwa ujumla na sio Tu wawekezaji wanufaike na Rasilimali za nchi yao kwa kuwekeza kwenye sector ya Afya katika Hospital ,madawa na maabara yenye vifaa vya kisasa na vyakutosha Hilo linawezekana.

Eneo lingine analitazama kwa jicho la Karibu Ni katika sekta yenye kuchukuaa pesa nyingi kutoka serikalini japokuwa serikali bado haijafikiria kuzuia ulipaji wa ada kwenye sekta ya elimu, Mh ngeleja anajitahidi kuona Ni jinsi gani ELIMU itakavyoweza kutolewa bure na kwa ufanisi mkubwa hasa katika maeneo ya vijijini ambako kumekuwa na ushukaji wa kiwango cha uandikishwaji wa watoto kwa ajili ya Elimu ya Awali kwa kiwango kikubwa kutokana na umaskini.

Vipaumbele vya Taifa, Hapa Mh Ngeleja anatazama kwa umakini mkubwa, kwani anatambua kuwa ili tuendelee Lazima mahitaji yote yatolewe kwa usawa kuliko kuzidisha matumizi ya serikali kwa kununulia mashangingi ya wizara Huku wananchi wakiendelea kutaabika .

Mwisho,nafasi Hii kwa mh Ngeleja ni muhimu sana hasa tukizingatia uwezo wake mkubwa kifikra na kiutendaji. Tanzania Ni nchi yenye amani hivyo mh. Ngeleja anatumaini Kuiona zanzibar ikiendelea kuwa huru katika mipaka yake huru ndani ya Tanzania ili kuweza kukuza uchumi wa Tanzania Bara na visiwani kwani sote Ni ndugu wa asili kabisa ,tunategemeana kizazi hadi kizazi hakuna anayefurahi Leo tukivunjika, hivyo Ni Vyema kuzingatia taratibu za muungano wetu.


SHIME TANZANIA ,NGELEJA TISHIO NA ATOSHA 2015 TANZANIA....


NAAMINI HII THREAD UMEIANDIKA WEWE MWENYEWE(Ngeleja).

Bungeni(uenyekiti wa kamati) wamekutimua kwa wizi na upuuzi wako. Kwamba bado unataka wananchi tukuelewe vyema wakati wawakilishi wetu wamekutema?

JIONGEZE Mwizi wewe na fisadi uliyekubuhu.
 
Usinichekeshe...ngeleja awe rais? Labda rais wa kamati y ya Miss tanzania. Ashindane na lundenga.
 
Back
Top Bottom