Ama kweli nchi hii haina mwenyewe (unclaimed property) mwandishi wa hii post unaweza kutusaidia Ngeleja alipokuwa waziri wa nishati na madini kwa karibu miaka mitano alitufanyia nini Watanzania cha kutufanya tumkumbuke. Kwa kipindi chote alichokuwepo pale alitusaidia nini katika sekta ya madini na alitusaidia lipi katika sekta ya nishati hata leo tufikirie kumpa nafasi ya juu kabisa katika nchi. Tusileteane utani hapa Urais si lele mama, Urais ni zaidi ya ving'ola na misururu ya magari, Urais ni zaidi ya kukagua gwaride na kuchezewa ngonjera. Urais ni pamoja na kuumia wananchi wanapokwenda hospitali na kukosa dawa, Urais ni pamoja na kusononeka pale basi linapo pata ajali na kuua watu zaidi ya 30 kwa mara moja, Urais ni pamoja na kuumia pale Albino wanapouawa hovyo na kukatwa viungo vyao. Urais ni pamoja na kutegua kitendawili cha wafadhili wanapoamua kusitisha misaada ya kibajeti, Urais ni pamoja na kukabiliana na mafisadi na wala rushwa wakubwa wanaoiteketeza nchi. Urais ni mzigo mzito unaohitaji busara za ziada.
MH.WILLIUM MGANGA NGELEJA SULUHISHO BORA MADINI
Itakumbukwa kuwa sekta ya nishati na madini ilishawah kukaliwa na nawazir wengi mno wakuwemo kina Mzee Msabaha,Mzee Daniel Yona na wengine wengi tuu,lakini hao wote walikuwa wanaishia kuwa katika wizara hiyo kwa muda wa miaka 2 na nusu na muda mwingine miwili kamili, ni mawazir watatu tuu akiwemo mh.Rais Kikwete pamoja na mh.Willium Mganga Ngeleja ndio waliokaa kwa muda mrefu kulingana na ugumu wa wizara hiyo,Mh.Kikwete alikaa miaka 6 na mh.Willium Mganga Ngeleja alikaaa miaka 5 na miez 8 kitu kinachoonyesha upambanaj mkubwa kwenye wizara hii na mh.Ngeleja, kwaukweli mambo aliyoyafanya yatabaki kuwa msaada mkubwa kwa Tanzania yetu,yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo mh.Ngeleja aliyafanya alipokuwa ktk wizara ya Nishat na Madini ikiwa ni kwa muda wa miaka 5 na miez 8,:-
1.Itakumbukwa kuwa Ngeleja ndiye aliyepambana kwa hali na mali mpk kuhskikisha kunapatikana maeneo zaidi kwa ajili ya wachimbaji wadogowadogo.
2.Itaendelea kukumbukwa kuwa ngeleja ndie muasisi wa utaratibu wa mfuko maalum wa kuwasaidia wadogo nchini kitu ambacho kinazungumzwa na wachimbaji wadogo mpaka leo,na hata juzi nilipokuwa ziarani Geita nilipata kutembelea maeneo ya wachimbaji wadogo na walimtaja Ngeleja kama mkombozi wao,na daima wataendelea kumtukuza kwa anachokifanya kwani anafanya mambo mazur anapokabiziwa majukum ya kijamii.
3.Mwezi April 2010 mh.Ngeleja alipiga marufuku usafirishaji nje ya nchi wa madini ghafi ya Tanzanite yenye ukubwa unaozidi gramu1,kitu ambacho juzi nilivyokuwa nazungumza na baadhi ya mawazir na baadhi ya viongoz wa juu wa chama walikipenda na kusema Ngeleja anafaa kuingia wazir mkuu wa Tanzania au hata Raisi kama akiamua kugombea
4.Mh.Ngeleja ndie muasisi wa utaratibu wa kutoa hati ya uasili(certificate of origin) kwa wanaouza madini ya Tanzanite nje ya nchi ikiwa ni mkakati wa serikali kudhibiti uuzwaji haramu wa madini ya Tanzanite,kitu amabcho hata Prof.Muhongo anajivunia sasa na kipindi fulani hivi ktk ziara yake mererani yanapopatikana madini ya Tanzanite mh.Muhongo alimtaja Ngeleja kama msaada mkubwa katika hilo...
Mwisho
Watanzania tunapaswa kuwasemea watu kwa mabaya yao na mazuri yao yalio mengi kwani hakuna mwanadam aliye kamili,..Ngeleja kafanya mengi sana sekta ya madini na hayo hapo juu ni kwa uchache wake.