Membe: Ngeleja ni tishio urais 2015

Membe: Ngeleja ni tishio urais 2015

kuna machizi duniani...hivi umetumwa kupima upepo au? mwambie huyo NGELEJA akawe Rais wa kijijini kwao.
 
Umepoteza muda kuandika maelezo marefu kumpigia debe Ngeleja! Kama wizara ya Nishati na madini alimshinda ataweza nchi? Alikuwa anasema nguzo za umeme zinatoka Africa kusini kumbe zinatoka Iringa. mzee wa escrow huyo hata ubunge asahau
 
Kumbe ni tishio tu, nilifikiri ndiye mgombea anayefaa! Haya bwana, ni mtazamo wako tunauheshimu! Ila usilalamike wenzako wakianza kutaja matishio yao.
 
uyu jamaa akigombea,chadema waweke jiwe na wasipige kampeni wasubirie kuingia UKULU
 
VITA UCHAGUZI 2015


Bado Hali ni tete ndani ya CCM ,Ila Nani atakaye mrithi JK Ipo wazi na nafasi Hii imemwangukia mbunge kijana Mwenye ufanisi na
Haiba ya kuvutiaa mh William Mganga Ngeleja mmbunge wa sengerema kuendana na kasi iliyopo kwa kumteua mwanasiasa huyu kijana mtaalamu wa fani ya sheria .

Kwanini JK atamwachia Mikoba Hii ni kutokana na Kukubalika na wanachama wengi na watanzania wengi kwa ujumla wao ambao wamehaidi kumpigania Mh Ngelejah endapo atasimamishwa kugombea nafasi Hiyo ambayo inaonyesha wazi ndiye mrithi sahihi hivyo watu wa tanzania wajiandae kushirikiana na mh ngeleja katika mqpambano hayo yenye kuleta tija kwa watanzania kwa ujumla

Vilevile uchapakazi wa Mh Ngelejah Unafanya aaminike zaidi ndani ya chama na kwa wananchi kwa ujumla ,ngeleja anaamini katika kujenga uchumi imara Wenye nguvu utakaopambana na umaskini na Rushwa akijikita kwa kuwekeza zaidi kwenye nishati ya Umeme ambayo itachangia uzalishaji mali kwa kasi zaidi, Mifano iliyo wazi kupitia REA ambayo imechangia kusambaza umeme vijijini kwa upana mkubwa.

Kazi ya ujenzi wa barabara, Licha ya kuwa Jk amejitahidi kwa asilimia 65% na amefanya kwa kiwango cha juu na anastahili pongezi kwa barabara nzuri za kiwango cha Lami zenye kupitika, mh Ngelejah anatamani kuona asilimia 100% ya barabara zote zimekamilika miradi yote na barabara zijengwe imara zenye kudumu, hili linawezekana Kama tutakuwa na mfuatiliaji makini ambaye ni Mh Willium Mganga Ngeleja.

Kitu kinachompa nafasi mh Ngeleja ni uwezo wake mkubwa katika ujenzi wa siasa unganishi isiyo na makundi ndani ya wananchi na vyama vyao vya siasa, akiwa mwenye nia njema, mh.Ngeleja anapenda kuyaunganisha Makundi yote na wananchi waote licha ya utofauti wa rika zao katika jamii ili kujenga nchi na kuondoa ubaguzi.

Halikadhalika mh Ngeleja amejitosa kulipambania swala la kuondolewa kwa vikwazo kwa wafanyabiashara na wakulima wadogo wadogo kwa kuwatoza kodi kubwa ukilinganisha na gharama za uzalishaji hali inayopelekea kuwanyonya wakulima wa hali ya chini pamoja na wafanya biashara wadogo wadogo, wakishindwa kulipa ada ya watoto shuleni ,"Lazima tuyalinde masoko ya ndani ili kuweza kumnufaisha mkulima wa hali ya chini kufaidi jasho lake" mh Ngelejah aliyasema hayo wakati akizungumza na wakulima wa mananasi wilayani Sengerema kata ya Nyampulikano ...katika kuwanufaisha wakulima katika masoko ya ndani.

Kuboresha Afya, hili limekuwa changamoto kubwa kwa Kila kiongozi anayetoka madarakani,mh ndiye mtu pekee atakayewezesha kutumiaa rasilimali zetu kunufaisha wananchi wote kwa ujumla na sio Tu wawekezaji wanufaike na Rasilimali za nchi yao kwa kuwekeza kwenye sector ya Afya katika Hospital ,madawa na maabara yenye vifaa vya kisasa na vyakutosha Hilo linawezekana.

Eneo lingine analitazama kwa jicho la Karibu Ni katika sekta yenye kuchukuaa pesa nyingi kutoka serikalini japokuwa serikali bado haijafikiria kuzuia ulipaji wa ada kwenye sekta ya elimu, Mh ngeleja anajitahidi kuona Ni jinsi gani ELIMU itakavyoweza kutolewa bure na kwa ufanisi mkubwa hasa katika maeneo ya vijijini ambako kumekuwa na ushukaji wa kiwango cha uandikishwaji wa watoto kwa ajili ya Elimu ya Awali kwa kiwango kikubwa kutokana na umaskini.

Vipaumbele vya Taifa, Hapa Mh Ngeleja anatazama kwa umakini mkubwa, kwani anatambua kuwa ili tuendelee Lazima mahitaji yote yatolewe kwa usawa kuliko kuzidisha matumizi ya serikali kwa kununulia mashangingi ya wizara Huku wananchi wakiendelea kutaabika .

Mwisho,nafasi Hii kwa mh Ngeleja ni muhimu sana hasa tukizingatia uwezo wake mkubwa kifikra na kiutendaji. Tanzania Ni nchi yenye amani hivyo mh. Ngeleja anatumaini Kuiona zanzibar ikiendelea kuwa huru katika mipaka yake huru ndani ya Tanzania ili kuweza kukuza uchumi wa Tanzania Bara na visiwani kwani sote Ni ndugu wa asili kabisa ,tunategemeana kizazi hadi kizazi hakuna anayefurahi Leo tukivunjika, hivyo Ni Vyema kuzingatia taratibu za muungano wetu.


SHIME TANZANIA ,NGELEJA TISHIO NA ATOSHA 2015 TANZANIA....

You have no idea,,,,,! Ccm haina mgombea mwenye sifa zaidi ya LOWASSA hao wengine ni vifaranga tuu na vibaraka wanaotafuta kuchumia tumbo na kuridhishana ushemeji kama yo presdent!
 
My God..!! Tahira lingine hili limekuja kwa I'd nyingine..!!

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
kwa hapa tulipofikia, thanks GOD, watu wameishiwa matusi ya kuwatukana waTanzania, na haya tunayoskia ndio ya mwisho, mwisho!
 
Ama kweli nchi hii haina mwenyewe (unclaimed property) mwandishi wa hii post unaweza kutusaidia Ngeleja alipokuwa waziri wa nishati na madini kwa karibu miaka mitano alitufanyia nini Watanzania cha kutufanya tumkumbuke. Kwa kipindi chote alichokuwepo pale alitusaidia nini katika sekta ya madini na alitusaidia lipi katika sekta ya nishati hata leo tufikirie kumpa nafasi ya juu kabisa katika nchi. Tusileteane utani hapa Urais si lele mama, Urais ni zaidi ya ving'ola na misururu ya magari, Urais ni zaidi ya kukagua gwaride na kuchezewa ngonjera. Urais ni pamoja na kuumia wananchi wanapokwenda hospitali na kukosa dawa, Urais ni pamoja na kusononeka pale basi linapo pata ajali na kuua watu zaidi ya 30 kwa mara moja, Urais ni pamoja na kuumia pale Albino wanapouawa hovyo na kukatwa viungo vyao. Urais ni pamoja na kutegua kitendawili cha wafadhili wanapoamua kusitisha misaada ya kibajeti, Urais ni pamoja na kukabiliana na mafisadi na wala rushwa wakubwa wanaoiteketeza nchi. Urais ni mzigo mzito unaohitaji busara za ziada.
 
Duuh.. kama Ngeleja alikuwa anapima upepo kwa mwamvuli amegundua nguvu ya upepo kuharibu mwamvuli lol.. Hakuna hata mmoja so far kwenye comments za hapa aliekubaliana na yeye japo ana haki ya kugombea..
 
Twendeni tu kwa kadiri mda unavoenda mtamsikia John Komba nae anatangaza nia ya kugombea urais
 
Back
Top Bottom