Membe: Magufuli asiwaendee pupa wafanyabiashara

Membe: Magufuli asiwaendee pupa wafanyabiashara

Mimi nafikiri tusimuattack mtu tuattack point zake, Membe ni mwanadiplomasia ametembea katika maeneo mengi yenye migogoro, anajua athari zake na anajua athari gani zitatokea Zanzibar.Ameweka angalizo ili baadae kikitokea chenye kutokea Mwenyezi mungu aepushie mbali aseme kwamba nilishatoa tahadhari hiyo. Hii inatupa picha kwamba asilimia kubwa ya makada ndani ya ccm hawakubaliani na maamuzi ya kurudia uchaguzi kwa kuwa wanajua nini kitatokea na kivipi chama kitaathirika.
 
Anacholaumiwa nacho Membe hiki hapa

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali iliyopita, Benard Membe amempongeza Rais John Magufuli kwa kasi aliyoanza nayo katika vita dhidi ya ufisadi na kudhibiti mianya ya wakwepa kodi, lakini akamshauri kuwa mwangalifu katika kushughulikia wafanyabiashara.
Membe alisema hayo katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika mapema wiki hii kuhusu, mambo mbalimbali yanayoendelea tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani.
Mwanadiplomasia huyo alisema hatua ambazo Rais Magufuli amekuwa akichukua kuwabana wakwepa kodi ni za msingi, lakini lazima alifanye kwa uangalifu mkubwa ili asiwafukuze wawekezaji ambao kimsingi ndiyo wabia wa maendeleo ya taifa.
“Wafanyabiashara ni watu wa ‘kuwahandle’ vizuri na kwa uangalifu mkubwa kwa sababu wao ndiyo gurudumu la maendeleo ya nchi yoyote duniani,” alisema Membe.
“Tunapozungumzia ajira, tunazungumzia wafanyabiashara ambao ndiyo wawekezaji. Sasa ombi langu ni kwamba Serikali isicheze nao.”
Akitumia ishara ya mkono wake wa kulia, Membe alisema: “(Mfanyabiashara) Ni kama ndege ambaye ili uendelee kuwa naye, ni lazima umshikilie hivi, lakini ukiachia vidole ataruka na kwenda kutaga mahali kwingine.”
Alikuwa akijibu swali kuhusu hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Serikali kuwabana wafanyabiashara wakubwa ili walipe kodi. Katika hatua hizo, Serikali ilibaini zaidi ya makontena 11,800 na magari 2,019 yalipitishwa bila ya kulipia ushuru bandarini na kusababisha Serikali ipoteze Sh 48.77 bilioni.
Pia, ilibaini kuwa kampuni zinazomiliki bandari kavu zilisababisha upotevu wa makontena 349 na hivyo kusababisha Serikali kukosa kodi ya Sh80 bilioni. Serikali ilichukua hatua kwa kubadilisha watendaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Mapato (TRA), kuwasimamisha kazi baadhi na wengine kufunguliwa kesi mahakamani.
Katika kikao na wafanyabiashara Desemba 3, 2016, Rais Magufuli pia aliagiza wafanyabiashara ambao hawakulipa kodi, wafanye hivyo ndani ya siku saba kuanzia siku hiyo.
“Ingekuwa mimi sikupi siku tatu wala siku saba kulipa kodi. Nakupa miezi miwili mpaka mitatu ili uweke sawa mahesabu yako kwa sababu kutunza hesabu siyo jambo rahisi na baada ya hapo nitakwambia tuendelee kuijenga nchi pamoja,” alisema Membe, ambaye pia aliomba ridhaa ya CCM ili agombee urais, lakini akaishia kwenye tano bora.
Membe, ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje kwa miaka tisa, alisema wafanyabiashara wana masikitiko makubwa dhidi ya Serikali na anaona suala hilo litaibuka bungeni kwa kishindo safari hii kwa kuwa wengi hawaridhiki.
Membe alibainisha kuwa moja ya masikitiko ya wafanyabiashara hao ni kupewa notisi ya muda mfupi kulipa kodi wanazodaiwa kukwepa katika uingizaji wa makontena bandarini.
Agusia kilio cha Lowassa
Membe pia aligusia tuhuma alizotoa aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa kuwa wafanyabiashara waliounga mkono wagombea wa upinzani wananyanyaswa na kuandikiwa kodi kubwa.
“Si dhambi wafanyabiashara kufadhili vyama vya siasa wakati wa uchaguzi. Lakini akishapatikana Rais, Serikali ina wajibu wa kuwakusanya wafanyabiashara wote na kufanya nao kazi ya ujenzi wa Taifa na siyo kuwaburuza,” alisema Membe.
Fukuzafukuza
Kuhusu mwenendo wa kutimua na kusimamisha watumishi wa Serikali walio kwenye maeneo yenye harufu ya ufisadi, Membe alisema, “Ni rahisi kumshughulikia mtu usiyemfahamu, lakini siyo rahisi kumshughulikia unayemfahamu”.
Alifafanua kuwa haitakuwa shida kwa Rais Magufuli kuwashughulikia watendaji aliowakuta serikalini ambao kimsingi hakuwateua, kwa kuwa hawafahamu.
“Kwake kufanya hivyo ni rahisi kwa kuwa pia ni rahisi kuwashughulikia watu usiowajua kuliko watu unaowajua, lakini hebu tuone kama atafanya hivyo pia kwa hao aliowateua mwenyewe,” alisema Membe.
 
.....mwana diplomasia huyu haitawezekana kupuuzwa!kamwe!
.....yapo mema kwa taifa letu ayaonayo!
MPOST THREAD TEND TO DIEGEST KWANZA!!/
Nina amini yapo mazuri 80%,na kidogo yenye walakini 20%.
....na si yote kwamba ni ya kipuuzi!
 
Watanzania tusipende sanaaa tusije aibika kama tunavyoaibika sasa wote tuliokuwa tunashabikia serikali ya awamu ya nne. Kama Membe hana haki ya kusema eti tu alikuwako kenye serikali iliyopita hata Magufuli hana haki ya kusema na kutekeleza anayofanya sasa kwani alikuwako pia sio tu awamu iliyopita bali miaka 20 iliyopita!!
 
1 serikali ya Magufuli kimsingi sio ndogo
Nje Magufuli ataenda atake asitake

2 uchaguzi Zanzibar haukapaswa kufutwa wote

3 wafanyabiashara wasiendewe kwa pupa ...............

Vipi Membe ulikua wapi ?? Au ndio fitina za Manguli ccm zimeanza ,naona kama safari yako ya urais 2020 umeianza rasmi ,vipi Magufuli mnataka kumpiga chini ???
Sina maana ya kua napinga anachosema Membe kimsingi inahitaji tafakuri ya kutosha
huyu Membe ametumwa si bure!
 
NAJUA NA NAONA WENGI WAMEANZA KUANDIKA VIBAYA KUHUSU HUYU BWANA NA MANENO YAKE YA KILA SIKU AMBAYO KIUKWELI KWANGU NAONA ANA NIA YA KUTENGANISHA WANACHAMA HUKUU WENGINE WAKIMKUBALI RAISI NA WENGINE WAKIWA AGAINST NAE

NAOMBA NIWAOMBE KAMA WANADAMU TUMPUUZE NA WALIOANGALIA MCHAKATO WA URAIS TANGU MWANZO NAHISI KAMA NI UCHUNGU WA KUKOSA NA KUANZA KUSEMA OVYO ANGEANZA SEMA HAYA LOWASSA..LAKINI AMEKUWA MSTAARABU NA SHANGAA HAWA WALIOFIKA TANO WANALALAMIKA NINI

2)) MKITAKA KUJUA KUNA SHIDA AMA KUNA KITU NDANIYAKE MH HUYU HUYU ALIWAHI KUSEMA ANAMPONGEZA MH RAIS KWA KUSITISHA SAFARI NA KUBANA MATUMIZI

NANUKUU MWANANCHI...NIHUYU HUYU ANARUDI KUMLALAMIKIA RAISI NA USITISHWAJI SAFARI NA UBANAJI MATUMIZI

HUYUHUYU ALISEMA WALIKUWAA WANAPISHANA ANGANI WAKITUA OFISI ZIKO TUPU LEO HII ANAGEUKA AMWONI KUNE KITU FULANI LABDA KILIKUWA EXP....??

NDUGU ZANGUNI LAZIMA MJUE BAADHI YA VIONGOZI WALIACHA NDUGU NA MARAFIKIZAO WIZARANI NA KAMA WAMEBANWA MSITARAJIE WATALALAMIKA HEWANI WATAONDOLEWA..SO NACHOOMBA

TUSIMDHIHAKI MEMBE TUMWOMBEE ABADILIKE IKIFIKA MUDA ATAMWELEWA DK MAGUFULI NI NANI NA ANA DHAMIRA GANI YA MAENDELEO KWENYE HII NCHI
 
w
Huyu membe vp katumwa.
1.baraza kubwa
2.kusfir nje ni lazma
3. Asiwabane wafanyabiashara...
Nan anampa hyo airtime kila siku
wewe membe acha kumzuia Raisi Magufuli afanye kazi yake ya utawala wa nchi usitake abembeleze wafanya biashara amabo asilimia kubwa wamekuwa wanyonyaji ya pato lataifa kwa mda mrefu...wewe mwenyewe ni mfanyabiashara pia una miliki mahoteli huko Mtwara na Lindi una magari kadhaa sasa leo umekutana na kibano cha Raisi Magufuli kinakuuma lipa kodi nawe ufanye biashara bila uoga bhana..
 
Haha CCM bana sio mtoe tamko la kumfukuza uwanachama kama Karume ?? Mmemtimua Mzee Moyo ndio ije kuwa wa Membe ??? Mtimueni bana
 
Swala la kumpuuza Membe, nashauri tukalijadili pale ofisi zetu Lumumba na siyo humu.
 
Arudishe zile za libya kwanza maana nayeye ni jipu
Atwambie na uchunguzi wa kifo cha yule Balozi wa Libya aliyeuwawa na Majambazi uchunguzi ulifikia wapi akiwa Waziri wa Nchi za Nje au ndio Case Closed.
 
Huyu membe mpumbavu sana, angetuuza watanzania wote kama angepenya kwenye tundu la sindano.

mjinga sana
 
Hapa ndipo pro Magufulu watakapomkumbuka EL,waache kumbeza. Bila team ma-mvi kupambana huko Dodoma,Membe angekuwa magogoni.

Uongo ukirudiwa saanaa hugeuka ukweli....

Kiongozi, movie ya dodoma ilipangwa na team mamvi kwa unyumbu wao wakatumika bila kujijua...

Movie ilikuwa mvi akatwe na kumuacha maembe...kwa hasira dhidi ya maembe, ilitegemewa kura za team mvi zingeenda kwa magu na hicho ndicho kilitokea...na hapo ndiyo utaelewa kwa nn wazee(kamati ya maadili) walishiriki kikamilifu kumkata mvi, lengo ni kupata reconciling figure...that figure was magu. Kama strategy hiyo inge fail bado ubabe wa kumpitisha magu ungetumika.
 
Aliyekuwa waziri wa Mambo ya nje Mh. Membe ameonya kuwa wafanyabiashara wasiendewe kwa pupa.

Ametanguliza kuwa anaunga mkono mikakati ya ukusanyaji kodi lakini isiwe katika hali ya kukatisha tamaa na kudidimiza uchumi.

Membe ameonya hayo kufuatia malalamiko ya wafanyabiashara kulalamika kuwa baadhi ya mikakati inaelekea kuwadidimiza.

Haya yameandikwa katika magazeti ya leo
Muulize Mh. Membe kuwa Nyerere aliwafanyaje wahujumu UCHUMI? Acha Magu afanye kazi yake. Au anataka hizo bandari kavu ziendelee? membe ni wa ajabu....kwanini asikae kimya tu?
 
Aliyekuwa waziri wa Mambo ya nje Mh. Membe ameonya kuwa wafanyabiashara wasiendewe kwa pupa.

Ametanguliza kuwa anaunga mkono mikakati ya ukusanyaji kodi lakini isiwe katika hali ya kukatisha tamaa na kudidimiza uchumi.

Membe ameonya hayo kufuatia malalamiko ya wafanyabiashara kulalamika kuwa baadhi ya mikakati inaelekea kuwadidimiza.

Haya yameandikwa katika magazeti ya leo
kama kuwadidimiza ni kuwabana wasiepe kodi na ushuru wa bandari bora wadidimie. sasa huduma za kijamii ni bora kupatikana kwa kodi au harambee za wafanyabiashara fisadi. tena hizo harambee lengo lao kumpa umashuhuri mwanasiasa fulani au kutangaza kampuni zao zisizolipa kodi. membe ni hasira baada ya kuona hajateuliwa popote serikali mpya ya hapa kazi tu. mbona jajapayuka kabla.
 
...kwa kauli hzi za membe nashawishika kuamini kuwa anaathirika kwa namna moja ama nyingine na utawala wa JPM....ama kwa kubanwa figisufigisu zake ......ama kwa kubanwa washkaji zake ambao ni wafanyabiashara...akiwamo (possibly) familia ya prince....maana wao hawawezi kutoka kwenye media na kulalama....membe anaweza kuwa anatumika kifamilia zaidi.....naliona hili hivyo...possibly ndivyo...
 
Back
Top Bottom