Membe: Magufuli asiwaendee pupa wafanyabiashara

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,819
117,362
Aliyekuwa waziri wa Mambo ya nje Mh. Membe ameonya kuwa wafanyabiashara wasiendewe kwa pupa.

Ametanguliza kuwa anaunga mkono mikakati ya ukusanyaji kodi lakini isiwe katika hali ya kukatisha tamaa na kudidimiza uchumi.

Membe ameonya hayo kufuatia malalamiko ya wafanyabiashara kulalamika kuwa baadhi ya mikakati inaelekea kuwadidimiza.

Haya yameandikwa katika magazeti ya leo
 
Aliyekuwa waziri wa Mambo ya nje Mh.Membe ameonya kuwa wafanyabiashara wasiendewe kwa pupa.Ametanguliza kuwa anaunga mkono mikakati ya ukusanyaji kodi lakini isiwe katika hali ya kukatisha tamaa na kudidimiza uchumi.Membe ameonya hayo kufuatia malalamiko ya wafanyabiashara kulalamika kuwa baadhi ya mikakati inaelekea kuwadidimiza.Haya yameandikwa katika magazeti ya leo
Wafanyabiashara waachwe watekeleze shughuli zao.
 
Huyu ndiye alikuwa chaguo la familia ya prince,

Yaani angepenya Tanzania ingevunja rekodi kwa kuongozwa na madhaifu wawili kwa miaka 20.

Lakini kwa hili yuko sahihi.
 
Bora wajumbe wa team Lowasa walichomfanyia,maana huyu angekuwa Raisi hii nchi ingekuwa ni shamba la wasioona na siyo la bibi tena
Wakati tunaandika bila Lowassa rais angekuwa Membe wengi mlibeza lakini sasa mnaanza kukubali wenyewe.
 
Washauri wa huyu jamaa kaeni nae chini mumpe busara. Kama ana nia ya dhati kumpa Mh. Rais ushauri Milango ya IKULU iko wazi. Hii tabia ya kuropoka kwa kutumia vyombo vya habari itampeleka pabaya. Au amepaniki baada ya Faili lake la kukwepa Kodi wakati anajenga Hoteli yake Mtwara kumfikiaa mezani Mh. Rais !!???
 
Members atulie watu wafanye kazi,anataka Tanzania iendelee kua ombaomba kwa sababu gani?hao wafanya biashara wameona Tanzania panalipa na kuna faida kuna ubaya gani wao kulipa kodi?mbona wafanyakazi wa kipato cha chini wanakatwa kodi?.Yesu mwenyewe alilipa kodi...hapa ni kodi tu hawawezi waache biashara. Ulaya kodi ni muhimu ndio maana anayekwepa anashitakiwa na kwenda jela maana ni jipu la umaskini.hamna namna walipe kodi tu.
 
Hapa ndipo pro Magufulu watakapomkumbuka EL,waache kumbeza. Bila team ma-mvi kupambana huko Dodoma,Membe angekuwa magogoni.
 
Back
Top Bottom